Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,584
- 6,136
Ubinafishaji sio kitu kibaya babu tatizo ni njisi serikali yetu inavyojiingiza kichwa kichwa. Dunia inasonga mbele.Ukitegemea kuwa sera za ujaa zitakuwa na nafasi huko tunakokwenda, unakosea sana.
Hakuna asiyejua unalolisema. Ila kuna vitu ambavyo KAMA NCHI inabidi viwe chini ya TAIFA. Ukisema HOTELI za kitalii ziwe za TaIFA hapa kweli unachemka. Lakini vitu kama JESHI, POLISI, MAJI, UMEME, ELIMU .... kwa ufupi sehemu zisizo na FAIDA na ni muhimu kwa taifa inabidi ziwe za serikali na ikibidi basi serikali lazima iwe inaongezea hela ili kupunguza mzigo kwa walipa kodi. Kuna vitu faida yake huja miaka ijayo na si leo. Kukosekana kwa umeme na maji ya kutosha inaweza kuwa chanzo cha kupoteza investment nyingi sana Tanzania. Nyerere asingelifanya SHULE BURE, leo hii mie ningelikuwa nalima TUMBAKU. Leo shule za kulipia...... kesho itakuwaje? Na hii ndiyo unasema dunia ya sasa inayosonga mbele ehh? USA na UK shule unalipia kiasi gani? Hata chakula shule ni sawa na bure. Hao Mabepari wenyewe unakuta wanajenga METRO ambayo INAWALETEA HASARA ila kwa sababu watu wanawahi kazini na kupunguza magari mjini, hii inaleta FAIDA kwa taifa kwa siku zijazo. Haya yapo leo na wanaendelea vizuri tu. Msiwe watu wa kukimbia kuwajibika kwa jina la KUBINAFISISHA.
Ningelikuwa KIKWETE leo hii umeme ungelikuwa wa SERIKALI na ningeliita WAHANDISI wote wafanye juu chini ili tuwe na umeme na bei iwe poa. Kama Wazungu waliweza, hata sisi tutaweza. Tatizo letu tunacopy na ku-past kila kitu bila kukiweka katika mazingira yetu. Tangu Mkapa kawafundisha Kubinafsisha basi wote mmeujua. Je Mabenki sasa mnakula KUKU ehh?? Hakuna njia ya mkato. Mafisadi watatula kama kuna cha serikali au si cha serikali so longer sheria hazifuatwi. HEbu soma artical ya Mwanakijiji juu ya RA na mipango yao ya RICHMOND. Dawa ni HARD WORK nakufuata sheria kwa viongozi na raia. Anyway NGOJA tukubaliane tupishane.