Kwanza ile sauti tu ya mkulu inatosha kuwaondolea furaha wananchi wote
Sauti mbaya kabisa kuwahi kutokea...
You want a romantic tone.
Ahaaa haaa haaa
Sisi kina mura tunasemaga, wee mama rhobhi ebu tenganisha mamiguu nirenge (in mura voice).. ahaaa haaa haaa
Hatunaga sweet voice popote pale.
But all in all, we WANTED such a guy MAANA nchi uliza, kila kukicha watu wanapiga madili tu, halafu Mimi hata buku nilikuwa sipati wakati wengine wanapiga hela ya MAANA. Tuvumilie tu, MAANA hata awamu iliyopita kelele zilikuwa nyingi SANA eti serikali ilikuwa LEGELEGE. Na watu wakaenda mbali ZAIDI kwamba JESHI LISHIKE HATAMU YA UONGOZI. Lkn tunashuku hilo la JESHI halikutokea, amekuja kiongozi wa kiraia ambaye anayafanyia KAZI kikamili yale yoote ambayo yalilalamikiwa sana na waTanzania wengi. Kinachonishangaza, ni pale ninapoona watu wakilalamika na kusahau yale yoote yaliyopita. SASA sijajua, ni wale waliokuwa wakinufaika na mfumo uliopita ndiyo wanaolalama, au ni ile kasumba ya binadamu "hakuna jema". MAANA lazima tukubali kuwa binadamu ni kiumbe wa ajabu SANA, na hata ukisoma kwenye vitabu, vinasema kuna kipindi hata aliyewaumba aliwahi kusema hivi niliwaumba hawa kwa sababu gani? Pengine alijuta kutokana na matendo wanayofanya. Unawapa kila kitu lkn bado hawaridhiki. Wanalalamika tu.
Tumuache tu RAIS afanye KAZI, MAANA huo uhuru ambayo watu wanausema tumekuwa nao kwa miongo kama mitatu hivi, lkn bado haikutusaidia, bado nchi ni masikini kwa uzembe na kutowajibika na rushwa na wizi vyote hivyo vikifanyika chini ya KIVULI CHA UHURU.
RAIS ANAkuwa mkali hivyo kwa sababu anataarifa kamili na usahihi wa kiwango kikubwa watoto jinsi nchi hii ilivyokuwa inaliwa na baadhi ya wenzetu kwa kushirikiana na wageni. Nchi ilikuwa shamba la bibi, watu wanachukuwa bila kufanywa lolote. SASA bibi kapata mjukuu mwenye nia njema ya kulinda mali. Tumuunge mkono na kumtia moyo azidazidishe hizi jitihada za KUJENGA uchumi na kulinda raslimali.
Hizo tafiti zisiwatie kiwewe, MAANA uhalisia wake unatia mashaka, mfano NCHI INAONGOZA KWA FURAHA DUNIANI, HALAFU KWA UPANDE MWINGINE IKO JUU KATIKA ORODHA YA NCHI AMBAZO RAIA WAKE WANAJIUA DUNIANI. MIMI BINAFSI SIJAELEWA. Nilitegemea wasio na furaha ndiyo waongoje kujiua na WENYE furaha wasiwe na sababu ya kujiua MAANA wana amani ya sura, roho, nafasi na AKILI. Hivyo hawana sababu ya kujiua.
Lingine ni vita ya uchumi, tusishangae kupata sifa mbaya hasa toka kwa mabepari. Na hilo halishangazi, MAANA hata Nelson Mandera aliwahi kuwa kwenye ORODHA YA MAGAIDI ya Marekani. Unaweza ukashangaa kwamba hivi naye Mandera alikuwa akiua watu!!? Jibu ni la, kwa sababu alikuwa akipinga sera za ubaguzi wa rangi wa makaburu. Hivyo jambo hilo liliwaudhi mabepari na ndiyo maana wakamwita Mandera gaidi. Ni majuzi tu rais wa Marekani aliyepita Obama akalitoa jina hilo kwenye ORODHA YA ugaidi na kusema ni aibu na dunia haitatuelewa kuwa na jina Mandera kama gaidi. Kwa hiyo maadam KUNA dalili za wazi za vita ya uchumi dhidi ya mabepari tutegemee mengi sana ya kutuvunja moyo na hata kutuchafua.
CC:
mulisaaa