"UPOPO" ninayaelewa yote hayo uliyoeleza hapo.
Mikataba huvunjwa au hurekebishwa dunia nzima kama yapo matatizo ya waliowekeana mkataba. Hakuna kisichorekebishwa kati ya mataifa, na hata watu au mashirika iwapo kuna mahitaji ya kufanya hivyo.
Hata hiyo ndoa, msipoelewana, mkataba hauwezi kuwafunga milele. Ndoa itavunjika, hata kama ni kwa mbinde, na maisha yataendelea.
La mhimu hapa, ni namna mnayouvunja mkataba. Mnaweza mkakubaliana mkae chini mtafute njia sahihi ya kuuvunja bila ya mtifuano, au muuvunje kwa mtifuano na kila mmoja wenu ni lazima atatoka na alama chafu, lakini mtaendelea na maisha yenu.
Unajua, wakati mwingine ni nafuu kuuvunja mkataba na kukubali chochote kitakachotokea kuliko kukubali uendelee kuumia ukiwa ndani ya mkataba kandamizi.
Kama hakuna njia inayoweza kufuatwa katika kuvunja mkataba bila ya maumivu, inabidi ukubali maumivu hayo ya mda, kuliko maumivu ya mda mrefu yatokanayo na kuwepo kwa mkataba.