Tanzania's Police Force is rotten

Tanzania's Police Force is rotten

Mkuu BAK, nakushukuru sana kwa kuiweka uzuri sana issue hiyo.

Mimi nataka kwenda mbali zaidi, tena kwa kikubwa tu. Jamani mambo ya kuleta siasa sasa tuseme BAAAASIII. Sikiliza, hivi ni kweli jamani " kuna maafisa wachache wa Police ndio wanaochafua sifa nzuri ya Jeshi la Police?" Hivi kuna maaskari wangapi ambao wanaweza kusema 'kwa kumuogopa Mungu' na kwa ukweli kabisa kuwa, HAWAJAPOKEA RUSHWA? Kuna Police kweli ambaye hajapokea RUSHWA katika Tanzania hii! Kweli kabisa hajapokea RUSHWA kabisa?

Kama wapo nachelea kusema hata 1% ya askari katika jeshi hilo hawafiki. Askari ambaye hajapokea RUSHWA ni yule aliye CCP Moshi basi. AU yule anayeanza kazi sasa anajifunza kutega mitego, baaasi. Jamani si tunaishi nao? Tunakunywa nao? Tukipelekwa vituo vya Police si tunakumbana nao? Askari Police kabisa kabisa, ana zaidi ya mwaka mmoja kazini, halafu eti hajapokea RUSHWA? Kama wapo basi ni hiyo 1%.

Yale mawazo ya baadhi ya Wabunge kuwa jeshi la Police livunjwe na liundwe upya yana mantiki na siyo ya kupuuzwa. Jeshi hili lina muundo wa kikoloni halina hekima ya utumishi kwa UMMA. Hili ni jeshi la kulinda Bwana Mkubwa.

Hivi unajua kwa nini FFU wanakuwa wakali sana wanapopambana na raia? Kwa sababu, FFU hawana nafasi ya kuomba wala kupokea RUSHWA. Wanapokutana na raia ni mkong'oto tu. Wanaishi makambini, wamefichwa kama mbwa mkali anayefungiwa ndani, mnyama kama huyu akifunguliwa tu mtu wa kwanza anayekutana naye ni kung'ata tu. No maneno.

Anagalia jinsi Askari Traffic walivyo na urafiki na madereva! Anagalia maafisa upelelezi walivyo wapole wanapokuja kwako kwa mara ya kwanza, kisha ukawakatia kidogo [ingawa huwa wapole pale tu ukiwa na kitu, kikiisha wanabadilika] Jeshi la Police ni ''mbwa wa watawala'' kazi yake ni kulinda ''makazi'' ya bwana. JESHI LA POLICE LINANUKA RUSHWA.
 
Mkuu wemma unachosema ni kweli kabisa. Ndani ya jeshi la polisi hakuna aliye safi kuanzia walio ngazi za chini hata wale wa ngazi za juu wengi wao wanajihusisha na wizi, ujambazi, kupokea rushwa kubambikia kesi wananchi kwa kesi ambazo haziwahusu na ghasia nyingine chungu nzima zinazofanywa na polisi hao hadi kufikia Watanzania kupoteza kabisa imani na jeshi hilo. Jeshi hili utendaji wake unafanana sana na jeshi la wadhalimu la Serikali dhalimu iliyokuwepo Afrika kusini miaka michache iliyopita. Inasikitisha sana lakini huo ndio ukweli halisi.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom