Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Zanzibar leo Mei 8, 2025, imeweka historia ya kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa kwanza wa Sheria za kazi, Mkutano huo ulioandaliwa na Taasisi ya Tanzanite CEO Roundtable - Zanzibar Chapter kwa kushirikiana na Kamisheni ya Kazi Zanzibar (ZLC), mkutano huo wa siku moja umefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip.
Viongozi mbalimbali wa Serikali, Wakuu wa Taasisi, Wawekezaji, na Wataalamu wa Sheria wamejadili mustakabali wa kazi na ajira katika mazingira ya uchumi unaobadilika kwa kasi.
Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini ambaye ndio mgeni rasmi amesema kuwa hatua za kuimarisha uchumi wa buluu zinahitaji mabadiliko ya kina katika sera na sheria za ajira.
“Hatua za kimkakati za kuiweka Zanzibar katika mnyororo wa thamani wa bahari, usafirishaji na uvuvi duniani zitakuja na mabadiliko makubwa,” amesema Balozi Togolani na kuongeza kuwa:
“Hili litahitaji mabadiliko kwenye sera zetu, mazoea na mitazamo ya Wazanzibari kuhusu ajira, kazi, na uongozi wa wafanyakazi.”
Alisisitiza kuwa uwekezaji mkubwa kutoka nje utaambatana na ongezeko la Wafanyakazi wa Kimataifa, hivyo ni muhimu kuweka Sheria nzuri zitakazoleta mwanga pamoja kuangalia suala la kuhudumia sekta mbalimbali kama utalii, mafuta na gesi kwa utofauti wake.
Kwa upande wake, Kamishna wa Kamisheni ya Kazi Zanzibar, Rashid Khamis Othman amesema kuwa mkutano huu unakuja kwa wakati muafaka ambapo Zanzibar inahitaji kujipanga upya kwenye mfumo wake wa ajira. "Mkutano huu ni jukwaa muhimu la kutathmini changamoto zilizopo sasa katika ajira,” .
Khamis ameongeza kuwa “Tunasisitiza haja ya kuimarisha majadiliano ya kijamii kwa kushirikiana na mifumo tuliyonayo ili kuhakikisha sheria zinakuwa jumuishi na za kisasa.”
Mkutano huu umebeba kaulimbiu “Future-Proofing: Innovative Solutions on Workforce Demands and Labor Laws”, ikiwa ni wito wa kujenga mifumo imara inayoweza kuhimili changamoto za sasa na baadae hasa katika soko la ajira linalobadilika kutokana na teknolojia na mahitaji ya kisekta.
Yunus Mwarab, ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzanite CEO Roundtable - Zanzibar Chapter amesema kuwa mkutano huu unaakisi dhamira ya kujenga mazingira ya kazi yaliyo shirikishi na yatakayokuwa na maslahi kwa wafanyakazi.
“Kupitia jukwaa hili, tunajenga ushirikiano madhubuti kati ya viongozi wa sekta binafsi na ya umma,”.
Yunus amesema kwa mara ya kwanza wamefanikisha jukwaa hili kwa ushirikiano mkubwa na serikali “Leo ni hatua muhimu katika kuhakikisha kwamba sheria za kazi zinawiana na mahitaji ya kiuchumi ya sasa.”
Ajenda zilizojadiliwa zimegusia maeneo ya usuluhishi wa migogoro kazini, akili ya kihisia katika kuongeza tija, teknolojia katika menejimenti ya rasilimali watu, na mazingira rafiki ya kazi.