Tanzia: Afisa Maendeleo ya Jamiii Ilala Bi Rhoda Mwanyangala apata ajali na Kufariki

Tanzia: Afisa Maendeleo ya Jamiii Ilala Bi Rhoda Mwanyangala apata ajali na Kufariki

Kirchhoff

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
5,735
Reaction score
8,541
Jioni ya Tarehe 25/11/2024 imetuletea simanzi mara baada ya Mtumishi huyu Mwema atisa Maendeleo ya Jamiii Segerea Rhoda Mwanyangala kuaga dunia.

Ajali hiyo ilitokea maeneo ya Luguruni akiwa kwenye bodaboda kurejea Nyumbani kwake mara baada ya Gari lililobeba wanafunzi kufeli break muda ambao taa zililizuia kupita

Mungu ailaze Roho yake mahali Pema peponi.

Pole Dkt. Gwajima D kumpoteza mtumishi huyo.

Mazishi ni nyumbani kwake Luguruni Ijumaa.
Screenshot_20241128-163234 (1).jpg
 
Afisa nini alikuwa anatumia usafiri gani?

Alale vyema
Imesemwa ni bodaboda,hizi bodaboda kama mtu unaweza kuziepuka usizipande ni kifo nje nje.

Kuna hizo halafu kuna Bajaj,Morogoro Road yote kutoka Manzese mpaka Kiluvya madereva wake hawana tofauti na wanaoendesha bodaboda kukutia kwenye semi ni kugusa tu
 
Boda boda ni tiket ya kwenda kaburini.

Kwa Tanzania yetu ,Boda boda zinaua watu wengi kuliko hata ukimwi ama kansa
 
Poleni kwa msiba. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu, mahala pema peponi.
 
Boda boda ni tiket ya kwenda kaburini.

Kwa Tanzania yetu ,Boda boda zinaua watu wengi kuliko hata ukimwi ama kansa
Mkuu hilo gari limeua hadi wenda kwa miguu na wauza matunda na watu kadhaa kujeruhiwa takriban 18.

...... Asainipo Mola Mwenyewe
 
Imesemwa ni bodaboda,hizi bodaboda kama mtu unaweza kuziepuka usizipande ni kifo nje nje.

Kuna hizo halafu kuna Bajaj,Morogoro Road yote kutoka Manzese mpaka Kiluvya madereva wake hawana tofauti na wanaoendesha bodaboda kukutia kwenye semi ni kugusa tu
Jinsi ilivyotokea huwezi kulaumu gari imekosa break ikaingia kituoni wakati huo mama wa watu nae ndio anajiandaa kupanda boda hapo arudi kwake..habari zikaishia hapo.
 
Back
Top Bottom