TANZIA: Aliyewahi kuwa Rais wa pili wa Zanzibar, Mzee Aboud Jumbe afariki dunia

Nadhani kunajambo alisahau yakuwa alikuwa kiongoz na aliapa kuzikubali sheria na katiba huku akiwa ameshika Quran sasa nilazima ajuwe atazikwa kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi zakuwazika viongozi. RIP mzee

Death is a private matter and it's between the deceased and his/her family. Serikali huwasiliana na familia/wafiwa kabla hawajafanya chochote na serikali hueshimu uamuzi wa familia.
 
Siasa za nchi hii zimesababisha watu muwe wanafiki sana. Sasa ndiyo nini kusababishiana malumbano yasiyo na tija humu? Marehemu ameshafariki muombeeni tu na siyo kufyatuka fyatuka.
 
R. I. P
 
Mkuu dangadunguri..
Sijakuelewa apo naomba unipe shule kidogo

kifo chake kilisababishwa na 'saratani ya damu' na 'alidhofu ghafla na viungo vyake kupoteza uwezo' huo ndio ulikuwa mwisho wake
 
Apart from udini kuna upuuzi mwingi tu aliufanya...! Just imagine alivyoharibu historia ya Tanganyika na hatimaye Tanzania as if huo uhuru aliuleta single handedly!!!

sio yeye tu jamani, au hamjawahi kufika huko bara nyieeeeeeeee? bora mwenzenu amegundua kuwa Dar sio bara ipo ndani ya maili 10 ameamua kusogeza nchi kwao
 
Na aliefanya mpaka mzee Jumbe akateseka namna ile kwa kifungo kile cha dhuluma,huyo mtu atalipa na atapata adhabu kali kwa MUNGU.

adhabu alianza kuionja hapahapa duniani kabla hajafika kwa hakimu wa mahakimu, alinyofolewa roho na 'saratani ya damu' akiwa 'amedhofu kwa ghafla sana' si maneno yangu, nikatika hotuba ya aliyekuwa mkuu wa nchi kipindi hicho
 
Kwani Magufuli yeye ni MUNGU?

hahahahahaa. eti Magufuli anaweza kumpoteza mtu, Tanzania kwa unafiki ni hatari, hakuna kitakachobaki juu mgongo wa ardhi hata kimoja, vile uonavyo mtu anashikwa na haja ndogo akasahau kila kitu kinachomzunguka hadi haja ndogo itoke, basi ujue hana anachoweza bila kwa idhini yake Muumba, likikufika ni Qadar yake na mtihani kwako
 
Mkuu dangadunguri..
Sijakuelewa apo naomba unipe shule kidogo

escotter
kuna uzi unazungumzia kifo cha mzee mtukufu, inasemekana kuwa 'saratani ya damu' ndiyo iliyomdhoofisha 'ghafla' huko UK ilhali hapa aliondoka buheri wa afya. inasemekana kuwa jinamizi la ubinafsishaji alioutaka 'mtoto mwema' halikumpendeza mzee wetu, sasa itakuwaje 'saratani ya damu' ilimuondoa duniani, akamtangulia jumbe miaka 15 mbele
 
Huyajui kama hata alipofariki Nyerere BADO aliendelea kuwa kizuizini Mji Mwema?

Wanafiki wanaomboleza ....ooh Chama kitamuenzi ....Wakati huyu alikuwa anatumikia Kifungo cha maisha ...kizuizini...,pale MJIMWEMA ilikuwa jela unajua rais akifungwa...anazuiliwa KWENYE Jumba ....
MFUNGWA KAFARIKI
 

taratibu ngomeu, hapa hapahitaji hasira saaana manake hutaelewa kitu, vuta subra utajibiwa kwa hoja madhubuti juu ya UDINI wa Nyerere, tuliza munkari hutaweza kujifunza
 
Wanafiki wanaomboleza ....ooh Chama kitamuenzi ....Wakati huyu alikuwa anatumikia Kifungo cha maisha ...kizuizini...,pale MJIMWEMA ilikuwa jela unajua rais akifungwa...anazuiliwa KWENYE Jumba ....
MFUNGWA KAFARIKI
Familia yake iwafukuze hao wapuuzi!Jumbe kafa akiwa kama mhaini ingawa ndiye Rais aliyeifanyia mema sana ZNZ kuliko Rais yyt yule

Hata hii Baraza la Wawakilishi ni yy alilianzisha mwaka 1980!Kabla ya hapo Jeshi ZNZ chini ya Kanal Bakar na baadae Brigedier Himid Mansour liikuwa linakugongea mlango na wakikuchukua huonekani tena!

Vigogo kama Dr Hanga;Dr Sherif,Mdungi Ussi,Ubwa Halj na wengineo hadi leo hawajulikani walipo presumed died!Prof Abdulrahman Babu yy alikuwa na bahati ya kutorokea Uingereza

Jumbe ndiye alianzisha utawala wa kisheria ZNZ
 
Huyu Maalim Sief huyu,
Mwenye kelele tele, anayeandamanisha watu kwa kudai mamlaka kamili za Zanzibar, hali yeye ndo "alimtia ndani" Mzee Jumbe kwa jambo hilo hilo?
Ama kweli dunia hadaa.......na kuishi kwingi ni kuona mengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…