TANZIA: Bi. Asha B. Makame afariki dunia

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906


Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Zanzibar, Asha Bakari Makame amefariki dunia leo huko Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.

Taarifa zilizothibitishwa na wanafamilia pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa umoja huo visiwani Zanzibar, Salama Aboud Talib zinasema kiongozi huyo alikuwa ametoka nchini India kwa matibabu.

Naibu Katibu huyo amesema kuwa baada ya Makame kutoka India kwa matibabu, alipitia Dubai kwa mwanae, mahali ambapo mauti ilimkuta mapema leo.

Mbali na wadhifa huo ndani ya UWT, Asha Bakari Makame ameshawahi kuwa Waziri wa Wanawake na Watoto katika serikali ya awamu ya tano visiwani Zanzibar iliyokuwa chini ya Rais Salmin Amour.

Mbali na wadhifa huo, mwanasiasa huyo ameshawahi kuwa mwakilishi katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na aliwahi kuwa mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba.



 


Aliyewai kuwa Mwakilishi wa bunge maalum la katiba na Waziri wa wanawake na watoto Zanzibar na Makamu wa Jumuiya ya wanawake wa CCM ametangulia mbele ya haki huko Dubai baada ya kurejea matibabu yake huko India.

Mwenyeenzi Mungu amsamehe makosa yake na amlaze mahali pema. Amin
 
Unamkumbuka yule mama wa Zanzibar aliyesema Serikali ya Zanzibar haiwezi kupewa watu waiongoze kwa vikaratasi wakati wa BMK?
Huyo ni bingwa wa mipasho bungeni alikuwa anaitwa Asha Bakari, kwa mujibu wa ITV amefariki dunia huko Dubai.
Apumzishwe kwa amani
 
Nimekosa neno la busara la kusema kwa huyo mama pamoja na kwamba mtu akifa huwa tunafuta madhambi yake yote ila ile kauli yake ndo inayofanya maalim seif asipewe Nchi hadi leo

"Na mie siamini kama kafa kwa mujibu wa ITV hadi niione maiti yake"
 
innalillah wainnaillah rajiu'un, poleni wafiwa na allah ( s.w ) awazidishie subira katika kipindi hiki kigumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…