TANZIA: Ephraim Kibonde afiwa na Mke wake Sara Kibonde

TANZIA: Ephraim Kibonde afiwa na Mke wake Sara Kibonde

Mtangazaji maarufu Ephraim Kibonde amefiwa na mkewe usiku huu katika hospitali ya Hindu Mandal. Bwana ametoa Bwana ametwaa. Amen.

======

Mke wa Mtangazaji wa Clouds Fm katika kipindi cha Jahazi, Ephraim Kibonde amefariki.
View attachment 806825
Kwa mujibu wa Mtangazaji mwenzie Gadner G. Habash amesema Mke wa Kibonde aitwae Sara Kibonde amefariki usiku huu akiwa anapatiwa matibabu ktk hospitali ya Hindu Mandal. R.I.P

Pole sana Kaka yangu na Kiongozi wangu wa Kitaaluma pia Ephraim Kibonde kwa Kuondokewa na Mpendwa Mke wako Sarah. Binafsi naungana nawe katika Kipindi hiki Kigumu na namwomba Mwenyezi Mungu akutie nguvu, akupe rehema na uvumilivu pia. Kikubwa tumshukuru Mwenyezi Mungu na tumuombee sana Mpendwa wetu Sarah ili apokelewe vyema huko aendako.

Nimepokea taarifa hii kwa mshtuko mkubwa mno, najua maumivu uliyonayo Kaka ila jikaze na yote tumshukuru Maulana.
 
Eeh ,bro Kibs wakiwa na mkewe pale London pub au escape one,utadhani ndio wanaanza uchumba ,binafsi bro Kibs alikua MC ktk harusi yangu,na mkewe Sarah alinitengenezea Keki na vyote walifanya kishikaji tu km rafiki yao ,nasikitika niko mbali ila msiba umeniuma sana huu
Mkuu kama kuna uwezekano wa kuja kutoka huko mbali hudhuria huu msiba
 
Pole sana Ephraim,nakumbuka takribani miezi 4 imepita sasa tangu siku ile tuliopishana na wewe pale Hindu mandal nje ukiwa umemshikilia mke wako ukielekea kwenye gari,Mungu akutie nguvu katika kipindi hiki kigumu...
 
Back
Top Bottom