TANZIA: George Tyson Afariki - Msiba mwingine Tasnia ya Filamu

TANZIA: George Tyson Afariki - Msiba mwingine Tasnia ya Filamu

Daaaah jembe limetutoka jamani R.I.P George... muanzilishi wa hizi bongo movie
 
Ile movie inaitwa GIRLFRIEND,aiisee this is more than sad news pole monalisa,pole mtoto wake Sonia na sasa kifo kimewatenganisha rasmii mana mlishatengana.

Yeah sasa monalisa anaweza kuolewa tena kanisani kifo kimewatenganisha.
 
Alikuwa anamuwekea kiwingu kuingia tena altareni,maana kashaolewa na slim ndoaa yaa kiislam akaachwa na ya kanisani ilimshinda sasa hv ataolewa tena.
Yeah sasa monalisa anaweza kuolewa tena kanisani kifo kimewatenganisha.
 
Alikuwa anamuwekea kiwingu kuingia tena altareni,maana kashaolewa na slim ndoaa yaa kiislam akaachwa na ya kanisani ilimshinda sasa hv ataolewa tena.

Daaah wangekuwa wote bado sasa monatungemuita mjane
 
Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema mongozaji wa filamu maarufu nchini George Otieno Tyson (Pichani) amefariki dunia kwa ajali ya gari huko Morogoro. Taarifa hizi ambazo zimethibitishwa na watu wa karibu yake zinasema kuwa, mauti haya yamemfika baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali na kupinduka walipokuwa wameenda kwa ajili ya kipindi cha

The mboni show ambacho yeye alikuwa ndiye muongozaji mkuu. Wasanii na mastaa mbalimbali nchini wameoneshwa masikitiko yako juu ya kifo hichi ikikumbukwa kuwa ni siku tano tu zimepita tangu mwigizaji Rachel Haule alipotutoka.

Batuli: - Niongee nini, niseme nini Mwenyezi Mungu tusamehe sie waja wako, Yarabbi eeeeeh Mola wng, R.I.P My brother, My shemeji, My director......Eeeeeh Mola mpokee George Tyson wetu, Poleni wasanii wenzangu, Poleni team nzima ya the mboni show thembonishow Pole Monalisa wangu

Rose Ndauka: Ki ukweli sina LA kusema ila asante baba wa mbinguni kwa kila jambo. ...mola mpokee ndugu yetu, kwa mikono salama na umlaze pema peponi ameen.....R.I.P George Tyson.

Agness Masogange: R.I.P George Tyson mm siamin bado jmn E Mungu tuhurumie waja wako!

Flaviana Matata : This is very sad aisee, Rest In Peace Tyson. Mungu kakupenda zaidi, - monalisa pole sana dadangu,Mwenyezi Mungu awatie nguvu

Wema Sepetu - Kwa mara ya tatu bila hata kupumzika week... tunamzika mwenzetu mwingine... George Tyson.... Dah... Im just speechless.. RIP brother... Dah sijui Da Mboni wangu ana hali gani aisee.... Pole dada akee ... Mungu akupe nguvu wewe pamoja na team yote ya thembonishow .... Pigo
kubwa tena kwa wasanii.... Tunaisha tu jamani.

Aunty Ezekiel - Mungu wang Naomba useme na sisi jaman Mungu baba tuone sisi jaman Naumia siwezi elezea jaman RIP Tyson wang jaman Rip director .....Nakosa lakusema

Mohamed Mwikongi : Hakika yametufika, A film director George Otieno Tyson naye hatunae tena duniani.

George Tyson aliwahi kuwa mume wa mwigizaji Monalisa na kuweza kuzaa naye mtoto mmoja. Mung ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
 
jamani hii bongo movie kuna nini tena tangu kanumba mpaka saivi imekua ni balaa R.I.P Tyson
 
Back
Top Bottom