Taarifa zilizotufikia hivi punde
zinasema mongozaji wa filamu
maarufu nchini George Otieno Tyson
(Pichani) amefariki dunia kwa ajali ya
gari huko Morogoro.
Taarifa hizi ambazo zimethibitishwa
na watu wa karibu yake zinasema
kuwa, mauti haya yamemfika baada
ya gari walilokuwa wakisafiria kupata
ajali na kupinduka walipokuwa
wameenda kwa ajili ya kipindi cha
The mboni show ambacho yeye
alikuwa ndiye muongozaji mkuu.
Wasanii na mastaa mbalimbali
nchini wameoneshwa masikitiko yako
juu ya kifo hichi ikikumbukwa kuwa
ni siku tano tu zimepita tangu
mwigizaji Rachel Haule alipotutoka.
Batuli: - Niongee nini, niseme nini
Mwenyezi Mungu tusamehe sie waja
wako, Yarabbi eeeeeh Mola wng,
R.I.P My brother, My shemeji, My
director......Eeeeeh Mola mpokee
George Tyson wetu, Poleni wasanii
wenzangu, Poleni team nzima ya the
mboni show thembonishow Pole
Monalisa wangu
Rose Ndauka: Ki ukweli sina LA
kusema ila asante baba wa mbinguni
kwa kila jambo. ...mola mpokee
ndugu yetu, kwa mikono salama na
umlaze pema peponi ameen.....R.I.P
George Tyson.
Agness Masogange: R.I.P George
tyson mm siamin bado jmn E Mungu
tuhurumie waja wako!
Flaviana Matata : This is very sad
aisee,Rest In Peace Tyson.Mungu
kakupenda zaidi, - monalisa pole
sana dadangu,Mwenyezi Mungu
awatie nguvu
Wema Sepetu - Kwa mara ya tatu
bila hata kupumzika week...
tunamzika mwenzetu mwingine...
George Tyson.... Dah... Im just
speechless.. RIP brother... Dah sijui
Da Mboni wangu ana hali gani
aisee.... Pole dada akee ... Mungu
akupe nguvu wewe pamoja na team
yote ya
thembonishow .... Pigo
kubwa tena kwa wasanii.... Tunaisha
tu jamani.
Aunty Ezekiel - Mungu wang
Naomba useme na sisi jaman Mungu
baba tuone sisi jaman Naumia siwezi
elezea jaman RIP Tyson wang jaman
Rip director .....Nakosa lakusema
Mohamed Mwikongi : Hakika
yametufika, A film director George
Otieno Tyson naye hatunae tena
duniani.
George Tyson aliwahi kuwa mume wa
mwigizaji Monalisa na kuweza kuzaa
naye mtoto mmoja. Mung ailaze roho
ya marehemu mahali pema peponi.