Tanzia iliyochelewa: Dkt. Edith Kitambi

Tanzia iliyochelewa: Dkt. Edith Kitambi

Red...
Kwa nini unasema maneno ya ovyo?

Hiyo ndiyo tafsiri yako ya taazia yake?

Nakuwekea taazia nyingine usome labda itakusaidia:

Sheikh Mtoro,
Dunia ni ndogo sana.

Siku nne kabla ya Eyshe kufariki alinipigia simu na alikuwa na kawaida ya kunipigia simu sana na tukizungumza muda mrefu khasa alipokuwa kalazwa hospitali.

Basi tulizungumza na akaniomba kuzungumza na mke wangu na walizungumza kwa muda mrefu pia.

Eyshe tumejuana shule St. Joseph's Convent 1969 yeye akitokea St. Xavier na tulikuwa very close.

Kwa kuzaliwa Eyshe alikuwa amenitangulia mwaka mmoja yeye kazaliwa 1951.

Maisha yalitutenganisha kila mtu akenda njia yake.

Miaka ikapita.

Siku moja kiasi cha kama miaka kumi na zaidi iliyopita Dr. Ramadhani Dau akanipigia simu kutoka Geneva nikiwa Tanga akanambia kuna mtu hapa anasema anakujua sana na angependa kuzungumza na wewe.

Alikuwa Eyshe na Dr. Dau alikuwa kampelekea zawadi kitabu cha Sykes akiwa hajui kuwa mimi na Eyshe tunafahamiana.

Hapo ndipo palipoanza mawasiliano yetu yaliyodumu hadi kifo chake na ni Eyshe ndiye aliyenifunza kutumia Skype kupiga simu.

Mwaka 2011 nilikuwa Berlin kiasi cha mwezi mmoja. Eyshe akanipigia simu kunialika nende nikamtembelee Geneva.

Nilikwenda baada ya kupita Amsterdam kwa mmoja wa ndugu zake, Bi. Haki.

Kwa hakika Bi. Haki ni dada yetu sote na nilipomwambia kuwa nakwenda Geneva kwa Eyshe alifurahi sana akanambia kuwa kila akizungumza na Eyshe heshi kunitaja.

Wakati huo mimi nilikuwa natokea The Hague kwa kaka yangu Prof. Mgone.

Eyshe tulikuwa hatujaonana muda mrefu sana tariban miaka 35 ukitoa siku nilipokwenda kumpa pole alipofiwa na mama yake na yeye akaja Dar es Salaam kuzika.

Ninachotaka kukuambia ni kuwa Eyshe alikujakuwa mcha Mungu wa kupigiwa mfano.

Katika ukaribu wetu miaka hii kumi iliyopita Eyshe alinieleza mengi katika maisha yake na akataka tuandike kitabu.

Kuna nyakati katika hii miaka alikuwa akishangaa sana wakati nikimsomea vipande katika shajara (diary) yangu ambamo nimemtaja mathalan siku moja nilimwambia tarehe fulani uliniaga unakwenda Dodoma.

Nikamwambia kuwa hiyo ni ''entry,'' katika shajara yangu ya 1969, basi alishangaa sana.

Hakika utoto una raha zake.

Kuna hulka za binadamu hazibadiliki.

Alipokuja kunipokea Geneva, ''train station,'' nilimuona ni Eyshe yule yule tuliyejuana udogoni.

Kuanzia kiatu chake hadi nguo zake amevaa, ''designer,'' nguo makhsusi kwa watu makhsusi zinazouzwa katika maduka makubwa.

Utanashati wake katika mavazi ulikuwa pale pale juu ya kuwa miaka ilikuwa imesogea.

Eyshe akifanyakazi ILO na alikuwa, ''fluent in French.''

Muda wote niliokuwa Geneva nikimuona akizungumza Kifaransa na wajukuu zake na hata na wahudumu katika migahawa aliyokuwa akinipeleka.

Siku moja Geneva alinichukua, mgahawa mmoja akiwa na binti yake anaitwa Jamila pamoja na wajukuu zake Kauthar na Rawdha.

Akanambia angependa mimi nimueleza mwanae, Bi. Jamila yeye alikuwaje tulipokuwa tunakua Dar es Salaam ya 1960.

Nilijua kuna kitu anataka mwanae ajifunze kutoka kwake. Basi mimi nilimweleza Jamila jinsi nilivyomjua mama yake na vipi tulivyokuwa shule.

Nilimwambia kuwa katika wasichana wazuri pale St. Joseph's Eyshe alikuwa mmojawao.

Nikamwambia pia alikuwa na kipaji cha kucheza dansi vizuri sana na cha michezo na timu yao ya Mkoa wa Dar es Salaam Basket Ball ilichukua kikombe 1968 (picha ya timu hii ninayo yuko Eyshe, Baby Ernest na Jennifer Gordon na hawa wote waliondoka Tanzania kwenda kutafuta maisha Ulaya).

Nashindwa kuiweka picha hii hapa kwa kuwa wasichana wote wako katika, ‘’shorts,’’ yaani kaptula. Huko ndiko tulikotoka.

Nilimweleza Jamila mengi na nikamwambia kuwa Eyshe ndiye aliyenifanya mimi niache mpira kwa muda niende kucheza Basket Ball.

Sisi tulikuwa ‘’co- education,’’ na timu ya Basket Ball tukifanya mazoezi pamoja na wasichana.

Siku tunaagana alinichukua mgahawa mwingine na kabla ya hapo tulikwenda kwenye ''mall,'' akamnunulia mke wangu zawadi na akanipa salamu akasema, ''Mwambie Riziki mimi ni nduguye,'' (Riziki ni mke wangu).

Siku nilizokaa pale Geneva kwa kweli nilifurahi sana na siku nyingine tukivuka mpaka wa Switzerland kuingia France akinipeleka kwenye mgahawa alioupenda.

Alitaka kulipa hoteli yangu nilipofikia nikamwambia hapana mimi natoka kwa Wajerumani nimefanya kazi na wamenilipa mapesa ya kutosha.

Hii hoteli alinichagulia yeye na akanambia iko karibu ya msikiti na akasisitiza kuwa niswali Fajr jamaa hapo msikitini na alinipeleka hadi msikitini niuone.

Eyshe alikuwa hasikizi muziki hata tukiwa kwenye gari yake na akanambia haangalii hata televisheni ila vipindi vya Qur'an.

Namshukuru Allah kwa kunikutanisha na Eyshe tukiwa watu wazima na namshukuru Allah kwa kumkuta ndugu yangu ameikamata dini kisawasawa.

Lakini Eyshe, ‘’way back then 2011,’’ alinidokeza kuwa alikuwa mgonjwa.

Ukisoma hapo chini emal aliyonitumia 2014 wakati mimi nakwenda Hijja utaona anasema kuwa emal yangu ilimpita kwa kuwa alikuwa kalazwa hospitali.

Allah amghufirie madhambi yake na amlipe pepo Firdaus. Amin.

Soma emal moja aliyoniandikia wakati nakwenda hija 2014 Eyshe Max

<eyshem@yahoo.com>:

To Mohamed Said 10/22/14 at 12:40 AM

As salaam Aleykum,
I am sorry sikuona email yako in time before you left.

Nilikuwa hospital, I hope all went well and that Allah akutakabaliye Hajj yako.

Hajj Mabroor wa Dhambi maghfur - Aamin.

You will let me know your experience, I know you have already done Hajj but this one is something else.

View attachment 2774134
Eyshe Abbas Max amefariki na kuzikwa Geneva

Apumzike Kwa Amani Dada Edith.
Shikamoo Mzee wangu.Niliamua Tu kukuchokoza nipate upande mwingine wa shilingi😁. Binafsi Mimi ni miongoni mwa wasomaji wa kila sentesi unayoandika.Kwangu Mimi nakuchukulia kama encyclopedia.Nimejifunza mengi Sana kutoka kwako,umenifanya nikaipenda JF.
swali langu kwako...
Nini Siri ya kuishi Maisha marefu yenye kila Aina ya exposure na still uko down to earth!?
 
Apumzike Kwa Amani Dada Edith.
Shikamoo Mzee wangu.Niliamua Tu kukuchokoza nipate upande mwingine wa shilingi😁. Binafsi Mimi ni miongoni mwa wasomaji wa kila sentesi unayoandika.Kwangu Mimi nakuchukulia kama encyclopedia.Nimejifunza mengi Sana kutoka kwako,umenifanya nikaipenda JF.
swali langu kwako...
Nini Siri ya kuishi Maisha marefu yenye kila Aina ya exposure na still uko down to earth!?
Red...
Mkorofi sana wewe mtu.

Toka asubuhi wewe wa kwanza kunichekesha.

Hii exposure na umri nadhani ni majaaliwa ya Mwenyezi Mungu.

Hakika wenzangu wengi wamenitangulia.
 
Pole sana kwa msiba wa mtu wako wa karibu uliyemfahamu enzi za uhai wake.
 
Pole sana kwa msiba wa mtu wako wa karibu uliyemfahamu enzi za uhai wake.
 
Nimesoma kuhusu kifo cha Dr. Edith Kitambi leo keshafariki muda mrefu na watu wameandika kama kumbukumbu.

Kwangu mimi ikawa ni msiba mpya na machungu yake naomboleza wakati wenzangu weshapoa.

Nilimfahamu Edith University of Wales Cardiff mwaka wa 1991 sote tukiwa Postgraduate Students kutoka Tanzania.

Alinizoea zaidi alipojua kuwa mimi na Ledgar Tenga aliyekuwa mchezaji wa Yanga na Timu ya Taifa ni marafiki.

Tenga ni kaka yake.

Alikuwa bint mzuri wa tabia na sura.

Nakumbuka yeye ndiye aliyenipa jina la "Sheikh" pale Cardiff na likaniganda kiasi jina langu likafa na wanafunzi kutoka Tanzania wote wakawa wananiita, "Sheikh."

Ukisikia Sheikh basi hakuna mwengine ila mimi.

Sababu ya jina hili ni kuwa ilikuwa kila Jumamosi kuna mahali nadhani ilikuwa club wanafunzi wengi wakienda kucheza disco na kujiburudisha na vinywaji.

Cardiff ni mji mdogo sana ukifananisha na London na miji mingine ya Uingereza kama Liverpool hivyo hata sehemu za starehe si nyingi watu hukutana mahali pamoja siku zote.

Ikawa siku zinapita wanafunzi wenzangu hawanioni kujumuika na wao.

Ulaya kwa mgeni ni mahali pa upweke sana ingawa mimi nilikuwa nimeshafika Uingereza kabla na napaelewa kwa kiasi kidogo.

Siku moja Edith akaniuliza kulikoni?

Nikistarehe sana kuzungumza na Edith sababu yeye tofauti na wengine wote alikuwa akisema Kiswahili kwa "accent" ya Dar es Salaam kabisa, utasema mwanamke wa Kizaramo wa Kariakoo.

Nilipata kumuuliza imekuwaje akaniambia kuwa yeye lau ni Mchagga lakini kazaliwa na kukulia Dar-es-Salaam.

Ikawa sasa hata tukiwa na party za Watanzania 9 Desemba au Sabasaba hanioni kucheza muziki na Edith akitaka kuninyanyua kucheza namtuliza kwa kumwambia Sheikh hachezi dansi.

Yeye akiishia kucheka.

Na Edith akifanya hivi kwa kutumwa na wenzake ili wapate kucheka kwa kumuona sheikh anamwagika kwenye "dance floor."

Miaka ile kulikuwa na bendi kutoka Kenya, "Virunga," "Mazembe" ambazo miziki yake ikipendwa na kuvuma hadi Ulaya katika jumuiya za watu weusi.

Nakumbuka hawa Virunga walipata kufika Cardiff na wanafunzi kutoka Kenya wakawa wanauza tiketi za dansi.

Kulikuwa katika party zile muziki wa Judy Baucher sina hakika na hili jina yeye alikuwa na nyimbo za "blues" hizi zikiwatoa fahamu vijana wengi khasa mashairi yake ya mapenzi.

Nyimbo hizi zilikuwa lazima zipigwe.
Party za Watanzania zikinoga sana.

Vijana wa Kizungu walikuwa haziwapiti wakiwapenda sana dada zetu zaidi wanavyojua kucheza.

Ulaya ukialikwa party unakwenda na kinywaji chako.

Edith masikini akipenda kunitania nami siku zote nikimchekesha kwa kumwambia mie mzee na sheikh siwezi kucheza muziki afanye staha.

Tukazoeana sana nikawa nimepata pia daktari kidogo nikijisikia namwendea.

Edith alikuwa anafanya shahada ya pili katika Public Health.

Nakumbuka alipata kuniambia kuwa kwa tatizo nililokuwanalo la tumbo atanitibia kwa njia ya "food elimination," na akaniwekea orodha ya kutokula vyakula fulani kimoja baada ya kingine kwa muda mfupi niangalie tatizo langu kama litaendelea au la.

Nilipona.

Alipata siku moja kunipa mhadhara mzima wa ukimwi.

Akaniambia ni tabu mtu kupata ukimwi akiwa kajituliza lakini ni rahisi kuugua akiwa kinyume chake.

Akanieleza kuwa yeye katibia wagonjwa wengi na hili kaligundua kutokana na utafiti wake katika "lifestyles."

Nilimwacha Dr. Edith Kitambi Cardiff lakini nilipata kurudi tena Uingereza, London kwa muda mfupi nilimtembelea nyumbani kwake.

Baada ya hapo sikupata taarifa zake hadi leo zaidi ya miaka 30 kupita nasikia amefariki.

Nitaingia Maktaba kuangalia picha za Cardiff nikipata picha yake In Shaa Allah nitaiweka hapa.

View attachment 2773081
Kulia Mwandishi na anefuatia ni Dr. Edith Kitambi
Thanks mkuu
 
Naomba kujua uhusiano wa mwanamuziki dully sykes na hiyo familia ya wapigania uhuru.
Mama...
Wewe si wa kwanza kujaribu kuwafuta Sykes katika historia ya Waafrika wa Tanganyika na harakati za uhuru.

Unaweza kuandika historia ya vijiji vya ujamaa bila ya kumtaja Nyerere?

Jibu ni wazi kabisa haiwezekani.

Unaweza kuandika historia ya uhuru wa Kenya bila ya kuwataja Wakikuyu na Mau Mau?

Haiwezekani.

Ndivyo ilivyo kwa Sykes.

Huwezi kuandika historia ya uhuru wa Tanganyika bila kuwataja Sykes.

Hapo juu ni taazia.

Sykes anaingije katika taazia ya Dr. Edith Kitambi?

Ingekuwa historia ya Wissman na Deutsch-Ostafrika na African Association na TANU ningewataja Sykes.

Hili nimeliweka mwisho kwa makusudi.

Mimi nimo katika Cambridge Journal of African History na nimo katika Dictionary of African Biography na kilichoniingiza humo ni kutafiti na kuandika historia ya Sykes kuanzia mwishoni mwa 1800 hadi mwanzoni 2000.

Ningekuwa naandika dini nisingeweza kuwa katika viwanja hivyo.

Lakini kitu kimoja tambua hata ikiwa hupendezewi kama wengi walivyokuwa hawakupenda kabla yako, mchango wa Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika hauna mfanowe.

Sykes ndiyo walioasisi Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) 1933 baada ya kuasisi African Association 1929.

Historia hii inakuudhi?
 
Naomba kujua uhusiano wa mwanamuziki dully sykes na hiyo familia ya wapigania uhuru.
Super..
Dully ni Abdulwahid Ebrahim (Ebby) Abdulwahid Kleist Sykes.

Mjukuu wa Abdul Sykes.
 
Back
Top Bottom