TANZIA: Ivan Ssemwanga (ex wa Zari) amefariki dunia usiku huu

TANZIA: Ivan Ssemwanga (ex wa Zari) amefariki dunia usiku huu

Mume uliyezaa nae watoto watano ukamuacha solemba, tamaa ya ujana ikakushika japo umri ulikutupa ukaja kufanya uasherati na kula raha na Diamond na kusahau kuwa ulipaswa uvumilie mlee watoto na wenzio.

Leo hii kwenye post yako unamwita great man na kumpa sifa kedekede marehemu Ivan baada ya kufariki kwani ulikuwa wapi kusema haya wakati hajafa?

Hili liwe funzo kwa wanawake mnaoacha waume zenu na kwenda kurukaruka na kula starehe iko siku watu mnaowaacha watakufa na kuwaacha ktk hali ambayo mtaumia sana. Sasa hivi Zari anatamani amuombe msamaha Ivan ila hawezi tena anatamani aseme neno lkn tayar amechelewa.

Hakuna wakati mgumu hapa duniani kama kudaiwa kihisia na marehemu
Sifa za marehemu hajaanzisha Zari
 
kweli nimeona umuhimu wa subra.sasa hivi angekula urithi wake kwa raha zake .sasa hivi sijui anaendaje kudai vitu vya marehemu hata kama ni kwa ajili ya wanae.ndo maana wanawake wengi huwa wanavumilia ndoa kwa ajili ya watoto wao
Kumbe na wewe unamawazo ya kimasikini namna hii. Unadhani Zari anafikilia urithi yule ana hela zake na biashara zake.
 
Zari ameanza kumendea mali za Ivan ila Baba yake mzazi Ivan kasema kwao pesa sio tatizo ila wanamshangaa Zari anayelilia mali wakati alikimbia familia na watoto na kumuacha Ivan na stress kibao.

Familia imesema Zari atarithi mali za huko madale alipokimbilia, wamesema wanazuiya mali zote za Ivan watoto wakikua watawakabidhi ila hawataki hata kumuona huyo Zari.
 
kweli nimeona umuhimu wa subra.sasa hivi angekula urithi wake kwa raha zake .sasa hivi sijui anaendaje kudai vitu vya marehemu hata kama ni kwa ajili ya wanae.ndo maana wanawake wengi huwa wanavumilia ndoa kwa ajili ya watoto wao
kwani watoto hawatopata urithi ? sasa yy angejuaje kama Ivan ndio ataanza kufa na sio yy zari ? alafu kuishi na mtu kwa sababu unasubiri afe upate urithi sioni kama ina logic
 
Ila Yule bwana alikuwa muungwana kwa kweli....Yaani mtu amekuchukulia ex wako, unamlelea mtot na anakuja Hadi kufanya shooting mjengoni kwako ...wala hajawahi hata kupost lugha chafu kuwatusi maskini ...mungu atamlipa hapo kwa huo ubinadam tu.....
Bibi kizee kuna jambo hapa hebu funguka aliyefanya hilo jambo
 
Mume uliyezaa nae watoto watano ukamuacha solemba, tamaa ya ujana ikakushika japo umri ulikutupa ukaja kufanya uasherati na kula raha na Diamond na kusahau kuwa ulipaswa uvumilie mlee watoto na wenzio.

Leo hii kwenye post yako unamwita great man na kumpa sifa kedekede marehemu Ivan baada ya kufariki kwani ulikuwa wapi kusema haya wakati hajafa?

Hili liwe funzo kwa wanawake mnaoacha waume zenu na kwenda kurukaruka na kula starehe iko siku watu mnaowaacha watakufa na kuwaacha ktk hali ambayo mtaumia sana. Sasa hivi Zari anatamani amuombe msamaha Ivan ila hawezi tena anatamani aseme neno lkn tayar amechelewa.

Hakuna wakati mgumu hapa duniani kama kudaiwa kihisia na marehemu
Hivi kama ni Zari angelikuwa ametangulia mbele ya haki ulitegemea Ivan angeliandikaje kuhusu Zari?
Ungelikuja hapa kumuita mnafiki? una hakika Zari ndio chanzo cha kuachana na Ivan?
Mimi kwa uzoefu wangu wa watu kuwaona watu wenye pesa huwa ndio chanzo cha kuachana na wanawake wao...wengi huwa ni wanyanyasaji wanawake.....
Nafikiri ni vgumu kusema Zari ni chanzo ikiwa hakuna ushahidi wa kujua hilo...
 
bilashaka atakuwa team sepenga uyo, maana kaongea maneno makali kama yeye alikuwa ana share na zari vile kwa ivan
 
Unafiki ni kitu kibaya sana kuna watu humu wanajifanya wanajua sana mahusiano ya Ivan na Zari yalikuaje, sababu za Ivan na zari kutengana na kila mmoja kuendelea na maisha yake wanajua wao wawili walioko nje kujifanya wanajua ni mbwembwe na Unafiki.halafu kingine Ivan hakuwa MTU mjinga kiasi cha kutoacha wosia na Mali zake kwa Ajil ya watoto wake, na kingine kwa hela aliyonayo Zari siyo mwanamke wa kwenda kulilia urithi kwao na Ivan.tuache Unafiki wabongo huwa tunajifanya kujua kila kitu Jitu linaishi kwa Dada ake halina mbele wala nyuma linashadadia maisha ya Ivan na Zari na umbea kibao tubadilike mfyuuuuuuuu
 
Yaani mtu kafa leo leo tena nchi nyingine lakini wabongo washapata taarifa za mirathi na urithi. Acha watu wabebe michanga, mawe mpaka nyasi zote tu watanzania tuko busy na umbea tu
 
Yaani mtu kafa leo leo tena nchi nyingine lakini wabongo washapata taarifa za mirathi na urithi. Acha watu wabebe michanga, mawe mpaka nyasi zote tu watanzania tuko busy na umbea tu
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] sichekei msiba ila hii komenti imenivunja
 
Nasema haya kutokana na sababu nitakazo zihainisha hapa chini ila ukweli kifo cha Ivan Semwanga chanzo chake nimapenzi sababu kuu ni Zari!
Ukiangalia tangu waachane na Zari Ivan hakuikubali ile hali na alijitahidi kumbembeleza Zari ila Zari hakutaka!
Na Ivan alitegemea Zari angerudi waendelee na maisha! ila baada ya kuzaa na Diamond Ivan alizidi kuishiwa tumaini la kuwa na Zari kwani alimpenda mno!!
f1dbd0bde9f1028cb0efea353f7df2ca.jpg
e9423d9d6a983a0fc2403ea78aad2ea9.jpg
bd0818ff6c03ba4e88094d6b44d624bc.jpg
ff1baf9bd030eafc8a956c069aaf1b22.jpg
e48bbcc8d2d62587134f9802e9e63bd8.jpg

Katika hizi picha alikuwa akituma ujumbe kwa Zari! Rudi mama kama pesa ipo huku!pia ukumbuke Diamond alipost kuwa amenunua Hammer kesho naye aaapost ana Hammer3 hii yote nikuwa alimpenda sana Zari!

Pia katika kuachana Ivan hakuwahi kupost picha yoyote akiwa na mwanamke! aliamini hakuna mwanamke wakumchallenge Zari hivyo hakuona sababu yakujidhalilisha kwani alijua Zari ni mzuri sana, hivyo hakaona ajipe muda!na alitamani arudi ila maamuzi haya, hayakuwa upande wake!! kwani Zari alishamchoka!. Hivyo umauti huo umetokana na msongo mkubwa wa mawazo!. Nina hakika Mungu akimfungulia Zari kutafakari juu ya kifo cha Ivan atatambua yeye ndiye aliyesababisha!

Mara nyingi tukiwa katika mahusiano ya muda mrefu hutokea tunachokana na kutamani yavunjike hata kama tunawatoto!kutokana na maudhi madogo madogo!ila ujidanganya nakusema bora tuachane ila wakiondoka! baada ya wiki utamani kuwarudisha ila mara nyingi uogopa watu watanionaje!!mbaya wakienda ambapo hatuwezi kuwaona tena kama kufariki basi hapo ndipo huwa tunapatwa msongo wa mawazo!! na hasa kama wametuachia watoto!.

Taadhari ikikutokea usijixhanganye katika pombe tumia muda kukaa na familia na kuwa busy na watoto baada ya muda tafuta mwenza japo atakuwa halingani na yule na nivigumu kumpata kama yule!na mhalalishe mbele ya familia yako ili upate muda wakukaa naye ndani kuliko kutumia muda mkiwa hotelini!maana ukirudi kitandani kwako hali itaanza upya!

Hivyo nirudi katika mada kifo cha Ivan Semwanga kimesababishwa na msongo wa mawazo ya mapenzi juu ya Zari.
 
Kumbe na wewe unamawazo ya kimasikini namna hii. Unadhani Zari anafikilia urithi yule ana hela zake na biashara zake.
Mkuu huyo Zari unaemtetea tayari wanagombania mali na wakwe zake huko, tatizo mnajifanya mnawajua watu kama mnakaa nao kumbe mnawaona kwenye social media.[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Maradhi ya moyo ni hatari sana na asilimia kubwa huchangiwa na msongo wa mawazo unapozidi au kuweka kitu moyoni kitu ambacho kwako kilionekana nij jeraha so kila ukikikumbuka moyo hupata jeraha. Ivan alishindwa kujicontrol pindi alipotengana na Zali na aliona maisha kwake hayana thamani naamini wengi tuko hvyo so kuna wakati tunaowapenda kwa dhati ndio wanasababisha yetu mauti naipa poule familia yote ya Ivan Ssemwanga katika kipindi hiki kigumu cha msiba na Tumuombe Mungu ampunguzie adhabu ya kaburi kwani wote ni waja wake na kwake tutarejea. Bwana anetoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Ameeen. R.I.P Ivan Ssemwanga.
 
Back
Top Bottom