MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,252
- 8,003
Katika usiku wa kuamkia leo Mkuu wa shule za LAKE SCHOOLS zilizopo nje kidogo ya mji wa Singida Mwl Makala amefariki dunia, Taarifa kamili za sababu ya kifo chake bado hazijafahamika.Mkuu huyo siku ya jana alikua mzima wa afya njema kabisa ambapo alikuepo katika semina za maandalizi ya usimamizi wa mtihani wa kidato cha sita utakaoanza hapo kesho tar 04/05/2015.Kwa mujibu wa mhabarishaji wangu ni kwamba juzi siku ya Ijumaa marehemu alisema alihisi kama kuna radi imempitia, kifuani lakini alienda kupima na vipimo vyote havikuonesha tatizo lolote na alikua mzima kabisa mpaka mauti yalipomfikia usiku wa kuamkia leo.Namkumbuka sana marehem nilipokua naye kazini mwaka 2010 kstka shule ya Murigha girls mkoani Singida, alikua MTU mtaratibu sana. Habari ziwafikie ndugu,jamaa na marafiki wote wa marehemu pamoja na wadau wote wa Elimu Tanzania kwani tumepoteza mpiganaji muhimu sana.Inalillah waillayh rajiun!,Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimiliwe amina!