TANZIA:Kuu wa shule za LAKE SCHOOLS za Singida afariki Dunia.

TANZIA:Kuu wa shule za LAKE SCHOOLS za Singida afariki Dunia.

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
5,252
Reaction score
8,003
Katika usiku wa kuamkia leo Mkuu wa shule za LAKE SCHOOLS zilizopo nje kidogo ya mji wa Singida Mwl Makala amefariki dunia, Taarifa kamili za sababu ya kifo chake bado hazijafahamika.Mkuu huyo siku ya jana alikua mzima wa afya njema kabisa ambapo alikuepo katika semina za maandalizi ya usimamizi wa mtihani wa kidato cha sita utakaoanza hapo kesho tar 04/05/2015.Kwa mujibu wa mhabarishaji wangu ni kwamba juzi siku ya Ijumaa marehemu alisema alihisi kama kuna radi imempitia, kifuani lakini alienda kupima na vipimo vyote havikuonesha tatizo lolote na alikua mzima kabisa mpaka mauti yalipomfikia usiku wa kuamkia leo.Namkumbuka sana marehem nilipokua naye kazini mwaka 2010 kstka shule ya Murigha girls mkoani Singida, alikua MTU mtaratibu sana. Habari ziwafikie ndugu,jamaa na marafiki wote wa marehemu pamoja na wadau wote wa Elimu Tanzania kwani tumepoteza mpiganaji muhimu sana.Inalillah waillayh rajiun!,Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimiliwe amina!
 
yule mzee keshamtoa kafara.

Yote anayajua Mungu mkuu! Japo hata mimi huyo mzee mmiliki wa shule aliwahi kunidhulum kabla sijaenda kutafta rizki kwingine.Tusiseme sana Mungu ndiye mjuzi wa kila jambo.
 
Yote anayajua Mungu mkuu! Japo hata mimi huyo mzee mmiliki wa shule aliwahi kunidhulum kabla sijaenda kutafta rizki kwingine.Tusiseme sana Mungu ndiye mjuzi wa kila jambo.

R
I.P
manake yule mchaga alitakaga kunichinja kweupe.
 
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.AMINA.
 
Bwana Mahanju yule sister mkatoliki, muhaya (mkuu wa shule) mkorofi ulimuacha pale muligha secondary? nakumbuka bwana Makala alikuwa vice-head master jina tu kwa yule mama wa kihaya!
 
Back
Top Bottom