TANZIA: Mchezaji wa zamani wa Simba, Christopher Alex Massawe afariki dunia

R.I.P Christopher Alex Massawe, nakumbuka sana mchango wake katika ushindi wa ugenini dhidi ya ZAMALEK ya Misri, daaah! Kocha wa enzi hizo JAMES AGGREY SIANG'A naamin atapokea taarifa hii kwa simanzi kubwa
 
Iko live waTz kwa kweli hii "homa ya kifua" kwa miaka hii imekuwa very serious hasa kwa watu waliokuwa maarufu...tukumbushane jama.
 
mpigaji wa mwisho wa penalty ya ushindi pale misri mwaka 2003,rest in peace brother Massawe.
 

Yeye alidai Kuna kiongozi wa Simba alibania uhamisho wake, that's why kwa hasira akaamua kuacha game.
 
Ananikumbusha mechi kati ya Simba na Yanga mwaka 2005 uwanja CCM Kirumba kombe la Tusker aliingia kutokea benchi baada ya Victor Costa kutolewa kwa kadi nyekundu

Iilibidi kocha afanye mabadiliko ya kumtoa winga Akilimali Yahaya na Christopher Alex akaingia kuimarisha ulinzi na akacheza pamoja na Boniphace Pawasa beki za kati pembeni akiwepo Said Sued na Nurdin Bakari.

Aisee maisha yanaenda haraka sana pumzika kwa Amani Christopher Alex.

Nikikumbuka siku hiyo umesimama kwenye mstari na rasta zako unamsubiri Akilimali atoke na wewe uingie kama nakuona tena. Wewe mbele nyuma yako sisi.
 
RIP massawe,TB inamaliza watu kwa kweli,tubadilike tabia

TB gani hiyo inamaliza watu? Tubadilike tabia kivipi dada Vicky, TB inaambukizwa kwa njia ya hewa, sasa tusiruhusiwe kupumua?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…