TANZIA: Mchezaji wa zamani wa Simba, Christopher Alex Massawe afariki dunia

TANZIA: Mchezaji wa zamani wa Simba, Christopher Alex Massawe afariki dunia

R.I.P Christopher Alex Massawe, nakumbuka sana mchango wake katika ushindi wa ugenini dhidi ya ZAMALEK ya Misri, daaah! Kocha wa enzi hizo JAMES AGGREY SIANG'A naamin atapokea taarifa hii kwa simanzi kubwa
 
Iko live waTz kwa kweli hii "homa ya kifua" kwa miaka hii imekuwa very serious hasa kwa watu waliokuwa maarufu...tukumbushane jama.
 
mpigaji wa mwisho wa penalty ya ushindi pale misri mwaka 2003,rest in peace brother Massawe.
 
Huyo jamaa alionwa na superspot utd ya south afrika kwenye kagame flani ilifanyika rwanda kama sikosei. Jamaa wakataka kumchukua moja kwa moja bila kufanya majaribio! Bangi hizi jamaa akagoma kwa kuwa wale jamaa walikua na shida sana ya kiungo simba wakawapa matola ambaye alikua tayari umri ushaenda na majeruhi kibao. Ilikuaje akaitosa ile nafasi? Inasikitisha sana na mnapoona watu hawakumpa sapoti kubwa kwenye matatizo yake wala msilaumu sana alikatisha sana tamaa watu. Alikua na uwezo mkubwa sana jamaa na zile rasta dah ilikua anatazamika vzr sana kwenye dimba lkn ndio hivyo tena!..

Yeye alidai Kuna kiongozi wa Simba alibania uhamisho wake, that's why kwa hasira akaamua kuacha game.
 
Ananikumbusha mechi kati ya Simba na Yanga mwaka 2005 uwanja CCM Kirumba kombe la Tusker aliingia kutokea benchi baada ya Victor Costa kutolewa kwa kadi nyekundu

Iilibidi kocha afanye mabadiliko ya kumtoa winga Akilimali Yahaya na Christopher Alex akaingia kuimarisha ulinzi na akacheza pamoja na Boniphace Pawasa beki za kati pembeni akiwepo Said Sued na Nurdin Bakari.

Aisee maisha yanaenda haraka sana pumzika kwa Amani Christopher Alex.

Nikikumbuka siku hiyo umesimama kwenye mstari na rasta zako unamsubiri Akilimali atoke na wewe uingie kama nakuona tena. Wewe mbele nyuma yako sisi.
 
Back
Top Bottom