mangelengele
JF-Expert Member
- Nov 4, 2014
- 1,293
- 1,100
Mkuu umeandika kiutu uzima hasa. Sisi sote ni wadhambi na tunajikwaa katika mambo mengi, tunahitaji neema na rehema za Bwana. Huu siyo wakati wa kumnyooshea kidole marehemu, tutafakari njia zetu huku tukimlilia Mungu atuwezeshe kulala katika tumaini; Biblia inasema 'heri ya wafu wafao katika Bwana ...'.
Tukumbuke kuwa wafiwa wanayo majonzi makubwa ya kuachwa na mpendwa wao, wanahitaji kupewa maneno ya faraja siyo kejeli kuhusu maisha ya marehemu.
CAM amelala mauti hadi parapanda ya mwisho itakapolia ambapo waliokufa katika Bwana watafufuliwa kwanza kisha walio hai kufumba na kufumbua watabadilishwa nao watamlaki Bwana mawinguni. Basi farijianeni kwa maneno hayo.
Poleni sana wafiwa Mungu awapatie nguvu katika kipindi hiki kigumu. Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe, amina.
Amina mkuu, tatizo jukwaa limevamiwa na wanafunzi ambao hawajui maisha ni nini. Kila cku tunasikia malalamiko humu, mara nguvu za kiume, mara nimesalitiwa, halafu lo wanajifanya wamepona ukimwi! Ndo maana tunasali na kumlilia Mungu kila mtu kwa imani yake ili atuepushe na dhahama za dunia hii, na mojawapo ni magonjwa. Kulingana na style yetu ya maisha kuna magonjwa mengi tu yanaweza kutupata na hayana tiba tena makali kuliko huo mf. Kisukari, stroke, kansa, figo, ini n.k haya pia ni magonjwa hatari, ni mara ngapi hatufwati kanuni za kiafya na vyakula? Lkn hawaoni km Mungu anaturehemu? Hvyo ni swala la sisi kumuomba mungu usiku na mchana atupe afya njema na Mungu pekee ndo anaweza kuthubu kuzungimza kauli km zile na co cc wanadam ambao hatujui km kesho tutafika.