TANZIA: Mchezesha Muziki maarufu nchini DJ Rico, amefariki Dunia

TANZIA: Mchezesha Muziki maarufu nchini DJ Rico, amefariki Dunia

Way back pale Bills alikua anatuchonganisha kwa kupiga ngoma za 2pac hapo tulikua tunaingia kucheza wale mashabiki wa 2pac alafu anakata anawaleta wa mashabiki wa Natorious ilikua kama sasa ivi watoto na hizi wanazoita team na alikua anahakikisha anaweka usawa wa idadi ya ngoma ilikua noma sana.
Pumzika Rico hii safari yetu sote tupo stand tunasubiri usafiri wetu tunaibuka sio muda.
 
Tulitoka mavumbini na mavumbini tutarudi,R.I.P the Legend
Kabisa. Nashangaa mtu anauliza amefia nini kama yeye ataishi milele. Maisha yetu yako mikononi mwa Mwenyezi Mungu. Sio kwa umahiri wetu tutaongeza hata sekunde
 
Ni.huzuni sana. Mungu awape nguvu na awatiefaraja familia ya DJ RICO. Gone too soon.

Mazishi itakuwa siku ya Jumatatu.
 
Too Sad ....mimi nimemfahamu 90s enzi za Bills akiwa sehemu ya kundi la madj waliojiita The Powerful 4 (nguvu 4) waliotikisa nchi kisawasawa akiwa na DJ JD, DJ HABIB na DJ G Lover ....alikuwa anajua kupiga aina nyingi za muziki kama House, R&B , Hiphop,oldies na hata Bolingo ....ni moja ya djs wanaojua kutumia mic na kuongea kiingereza fasaha ....amefanya kazi East Africa Radio kwa muda mrefu kabla hajaamua kudeal na issues zingine ....nilikuwa nakutana nae mara nyingi Triple 7 alipokuwa anapiga .....pumzika kwa amani brother ....
Mkuu mara ya mwisho Ricco kupiga Tripple 7 lini?
 
Nilimfahamu those days way back 2002-2003... Akipiga studi bekaz namanga msasani wakitokea ea radio yeye, Dj bush baby,marehemu Dj faridah
 
Nilimfahamu those days way back 2002-2003... Akipiga studi bekaz namanga msasani wakitokea ea radio yeye, Dj bush baby,marehemu Dj faridah
Yes ...maana around 2000 -2001 Powerful 4 walihama Bills kwenda Mambo Club (maisha club zamani) ....nyomi la Bills likahamia Mambo club ....
 
Mungu aipokee roho ya maehemu aipumzishe kwa amani Amina.
 
Inasikitisha
Imeniuma kwasababu ninamfahamu

R.I.P Rico

Poleni sana familia, wote na wadau wa 777.
 
Sikumbuki mkuu ....ila mara nyingi nikipita pale utamkuta kaunta ...

Ok kumbe kaunta.
Nilifikiri naye alikuwa anashiriki kurusha Watu.

Ila Dj wa Tripple 7 anaweza sana

Yeye ndie aliyekuwa anapiga miziki ya pale kuanzia mchana hadi wanafunga. Na ndani pia huwa anapiga baada n.k

Hapo kaunta ndipo yake ya muziki yanakuwepo kwa mwishoni pale
 
Kutoka kwa DJ JD Whatsap ....

Habari

Ndugu zangu mimi naitwa John Dillinga. Nina imani kuwa mpaka sasa taarifa za msiba wa ndugu yetu DJ Rico zimeshakufikia.

Jana wawakilishi kwa upande wa ma DJ tulikwenda nyumbani kwa marehemu Chang'ombe, tulifanikiwa kukaa na ndugu wa marehemu ili kujua taratibu za msiba na sisi kama ma DJ wenzake majukumu gani tutayachukua na kuyafanya; ikiwemo kupewa taarifa kuwa mazishi ya ndugu yetu DJ Rico yatafanyika siku ya Jumatatu katika makaburi ya Kinondoni.

Kwa upande wa ma DJ michango ya kufanikisha shughuli hiyo ya mazishi inaendelea kuchangwa kutoka katika vikundi tofauti vya ma DJ.

Kwa wale ambao mna kumbukumbu mtakumbuka kuwa DJ Rico aliwahi kuwa mmoja wa kundi la kwanza la maDJ wa 4 lililokuwa likijulikana kama The Poweful 4 likiwakilishwa na DJ RICO, DJ G LOVER, DJ HABIB na DJ JD. Kwa mapenzi yetu kwa mwenzetu DJ RICO, leo IJUMAA na kesho JUMAMOSI pale CLUB LEGENDS tutasherekea maisha ya *DJ RICO (SPECIAL TRIBUTE TO DJ RICO)*

Kwa wewe ambaye unatamani kuchangia msiba wa ndugu yetu na unamfahamu, kwa urahisi utaupeleka wapi mchango wako?
Nakukaribisha *CLUB LEGENDS SPORTS BAR & GRILL* kuanzia sa kumi jioni, kutakuwa na daftari maalum kwaajili ya michango hiyo.

Kwa niaba ya CLUB LEGENDS, *THE POWERFUL 4,* vikundi mbalimbali vya ma DJ na ma DJ wote naomba niwashukuru sana kwa kusimama pamoja nasi katika kipindi hiki kigumu na nawakaribisha sana Club Legends leo Ijumaa na kesho Jumamosi katika SPECIAL RESPECT & TRIBUTE TO DJ RICO.

*REST IN PEACE BROTHER AND THE LEGEND*

UKIWEZA TAFADHALI SHARE UJUMBE HUU NA WADAU WENGINE
 
Back
Top Bottom