Taarifa zinasema Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi ya Kusini ya KKKT Dr. Gabriel Nduye amefariki dunia leo kwa ajali ya gari.
Imeelezwa kuwa Mchg. Dr. Gabriel Nduye amepata ajali baada ya gari lake kugongana na lori katika kijiji cha Ng'anda Njombe alipokuwa akirejea kutoka kwenye semina ya Kiinjili iliyofanyika kijijini hapo.
Habari zaidi kuhusiana na tukio hilo zitafuata.
Poleni wanafamilia, washarika, jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huo, pumzika kwa amani Baba Mchg. Dr. Gabriel Nduye
Kuna majimbo ya makanisa yana umaskini sana dayosisi inampa mtumishi wake gari namba C ya mwanzoni huko kweli!!!! na juzi juzi hapa huyu Mkuu wa KKKT kapewa chuma mpyaaa.