Tanzia: Msanii Mashaka (Ramadhani Ditopile) wa Kaole Sanaa Group afariki dunia

Tanzia: Msanii Mashaka (Ramadhani Ditopile) wa Kaole Sanaa Group afariki dunia

Naona umekazana kumuita "Mzee Mashaka". Mashaka hakuwa mzee. Ni kijana aliyepata mvi mapema.
Mzee tusibishane namjua zaidi ya wewe umjuavyo katika runinga mzee wetu..
DADY%20H%2020181020_190918.jpeg
 
R.I.P Mashaka. Ulitendea haki yale maigizo yako.

Hadi machozi yalikuwa yanawatoka watazamaji. Watazamaji wakaanza kumchukia Zawadi.
 
Nilisikia alikua na udugu na Ditopile Mzuzuri Ukiwaona
 
Sifahamu aisee ila ni mtu wa Morogoro huyu hajawai kunambia kama ana undugu na Ditopile
Ni mdogo wake Ukiwaona Ditopile Ramadhani Mwinshehe Mzuzuri.

Kwenye kijiwe chetu cha kahawa kipindi flani Ilala Bungoni kuna wakati akatuambia asili yao kabisa Oman. Ubishi ukazuka lakini yakapita maadam barza imepata burdani!

Alikuwa na mdogo wake pia, anakulakula 'poda' ila Mtu wa stori pia kijiweni.

Ila uzuri wa kahawa bana ukiwa na buku unazungusha ofa na kashata juu! Hapa nilipo buku hata maji ya dhahabu hupati.

Cc Pohamba
 
Pumzika kwa amani Mashaka.

Uliitendea haki tasnia ya uigizaji.
 
Mkuu, Mashaka ni baba wa kunizaa. Wewe unauhusiano gani naye, mpaka uanze kubiashana na mimi?
Nawajua watoto wake na mashaka wengi tu ila namjua zaidi Abdul,Mashaka alikuwa anaishi kibo karibu na kwa kina msuva,familia yake alikua anaishi na mke wake,mama yake mkwe ambaye ni mzee sana na huyu bibi mwanzo kabisa alifichwa taarifa za msiba za mzee Mashaka kutokana na hali yake ya ugonjwa na nyumba ya mzee mashaka marehemu kuna kigeti kidogo chekundu na ndani nyumba nzima kuna marumaru nyeupe,kuingia nyumbani kwake unaanza vyumba kwanza then sebule ipo mwisho ikiwa pamoja na meza ya kioo na mzee huyu alikuwa mlemavu wa mguu aliparalize ila mungu mkubwa alimponya hili ila alibaki na kilema cha mguu cha maisha...
Hizo ni dondoo tu kuonyesha jinsi gani huyu mtu mimi namjua vizuri sana na hata nkikutajia mimi ni nani na ukienda kutaja tu jina langu kwa Mrs mashaka(bibi Warda) atakuthibitishia kwamba jinsi gani nnavyomjua vizuri,turudi kwenye point hata kma wewe ni mwanae kweli unaongea mbele za watu kwamba mzee mashaka hakuwa mzee dunia si itakushangaa hii maana mimi Nina around 35 na mashaka kanipita mara mbili umri!
 
Sana, kuna dada mmoja aliitwa peace sijui yuko wapi, akina tabia. Wakati huo maigizo yakikuwa na mvuto kuliko bongo movie
Peace alikwishafariki kitambo, zaidi ya miaka 15 iliyopita. Tabia naye alifariki wakati wa mabomu ya Gongo la Mboto...
 
Halafu zawadi na wenzie wakamchuna mpaka basi.
Akafulia na akaanza kulijua jiji.
zawadi alikuwa na mdomo hahahahaha alikuwa anamlaza jamaa nje mara atoke na mabwana hovyo yaani ni fujo wakat mwanzo anatafutwa na mama mashaka alikuwa mstaarabu alipo olewa sasa.
 
Back
Top Bottom