TANZIA Tanzia: Msanii wa kundi la Jagwa Music, Jack Simela afariki

TANZIA Tanzia: Msanii wa kundi la Jagwa Music, Jack Simela afariki

junky

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2017
Posts
413
Reaction score
978
Msanii maarufu wa kundi la Jagwa Music ambaye alikuwa nyota wa kundi kwa sauti yake tamu na Nzuri bwana Jack Simela ametutoka kwa ajali ya gari aliyoipata mkoani Morogoro kwa kugongana na Scania.

Hii ni pigo kwa mashabiki wa Mchiriku sio tu Tanzana bali duniani kwa ujumla sababu Jack Simela alikuwa na mashabiki wengi Copenhagen, Berlin, Ulaya na hata Marekani kwakuwa Kundi la Jagwa Music mara nyingi walikuwa wanaitwa kufanya ziara kwenye nchi mbalimbali za barani Ulaya

-Saidi michape
-kondakta

Ni baadhi ya ngoma nazikimbuka za Jagwa Music ambazo Simela alizinogesha ..

FB_IMG_15443422572933233.jpg
FB_IMG_15443422665189882.jpg
FB_IMG_15443422190253332.jpg
FB_IMG_15443421216253938.jpg

Mmoja kati ya wasanii wa kundi la Jagwa Music, Jackson Kazimoto maarufu Jack Simela amezikwa Desemba 10, katika makaburi ya Bigwa mkoani Morogoro.

Baba wa msanii huyo, Leonard Kazimoto amesema kuwa msanii huyo, mjomba wake na wenzake watano walifariki dunia wakiwa njiani kwenda makaburi ya bigwa kwajili ya mazishi ya shangazi wa msanii huyo.

“Wakati tunaenda kuzika tulitoka wote hapa maana msiba ulikuwa Mwembesongo wao walikuwa saba wote waliingia kwenye gari lao dogo walipitia barabara kuu ya Moro/ Dar sisi tulipita barabara ya zamani ya Dar, tulipofika makaburini ilituchukua muda kuwasubiri maana tulitaka Jack amzike shangazi yake na pia Ibrahimu Karata naye amzike mama yake ila tulipoona hawatokei tukazika.

“Kumbe walikuwa wamepata ajali eneo la nane nane maarufu kwa jina la Jordan na wote sita wamefariki dunia isipokuwa mmoja amelazwa yupo hoi hospitalini,’’ amesema.

Amesema waliporudi nyumbani walishangaa kuona vilio vikizidi walipohoji ndipo wakaambiwa kuna msiba mwingine Jack, Ibrahim na wenzao wengine waliokuwa kwenye gari ndogo waligongana na gari kubwa.

Naye shangazi wa msanii huyo, Yasinta Kazimoto amesema alimlea msanii huyo aliyezaliwa 1986 tangu alipokuwa na miaka nane baada ya mama yake mzazi kufariki mwaka 1994.

“Nilimlea vizuri hadi mwaka 2004, alipokuja kuchukuliwa na meneja wake, Gola tangu alipomuona alipokuwa akiimba kwenye moja ya maonyesho ya Jagwa Manzese mkoani hapa hadi sasa mauti yemamkuta ameishi katika kundi la Jagwa kwa miaka 13, alikuwa mtu safi alinipa zawadi kila aliposafiri sikupata naye tabu katika malezi yake,’’ amesema Shangazi yake.

Ameongeza kwamba msanii huyo ameacha watoto watatu, Saidi (18), Nuru (17) na Leonard (4).

Meneja wa mwanamuziki huyo, Abdallah Salehe maarufu meneja Gola amesema kifo cha msanii huyo aliyehitimu elimu ya msingi Shule ya Mwembesongo mkoani hapa ni pigo kubwa kwa tasnia ya muziki wa mchiriku na kwa kuwa yeye ndiye aliyekuwa amebaki kuubeba muziki huo.

“Jack ndiye alikuwa amebaki kuubeba muziki wa mchiriku kifo chake ni pigo kubwa kwa muziki huo, kwani uwezo na uvumilivu wake baada ya wasanii wengi kuliacha kundi la Jagwa ndiyo ulikuwa ukibeba kundi hilo kote ndani na nje ya nchi walipokuwa wakifanya maonyesho yao,’’ amesema Gola.
 
Msanii maarufu wa kundi la Jagwa Music ambaye alikuwa nyota wa kundi kwa sauti yake tamu na Nzuri bwana Jack Simela ametutoka kwa ajali ya gari aliyoipata mkoani Morogoro kwa kugongana na Scania.

Hii ni pigo kwa mashabiki wa Mchiriku sio tu Tanzana bali duniani kwa ujumla sababu Jack Simela alikuwa na mashabiki wengi Copenhagen,Berlin hata Marekani kwakuwa Kundi la Jagwa Music mara nyingi walikuwa wanaitwa kufanya ziara kwenye nchi mbalimbali za barani Ulaya

-Saidi michape
-kondakta

Ni baadhi ya ngoma nazikimbuka za Jagwa Music ambazo Simela alizinogesha ..

View attachment 961310View attachment 961311View attachment 961312View attachment 961313View attachment 961314View attachment 961315

Wazee wa kambi popote
 
Msanii maarufu wa kundi la Jagwa Music ambaye alikuwa nyota wa kundi kwa sauti yake tamu na Nzuri bwana Jack Simela ametutoka kwa ajali ya gari aliyoipata mkoani Morogoro kwa kugongana na Scania.

Hii ni pigo kwa mashabiki wa Mchiriku sio tu Tanzana bali duniani kwa ujumla sababu Jack Simela alikuwa na mashabiki wengi Copenhagen,Berlin,ulaya na hata Marekani kwakuwa Kundi la Jagwa Music mara nyingi walikuwa wanaitwa kufanya ziara kwenye nchi mbalimbali za barani Ulaya

-Saidi michape
-kondakta

Ni baadhi ya ngoma nazikimbuka za Jagwa Music ambazo Simela alizinogesha ..

View attachment 961310View attachment 961311View attachment 961312View attachment 961313View attachment 961314View attachment 961315
Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahala pema peponi japo simfahamu huyu msanii
 
Back
Top Bottom