Tanzia: Muigizaji Rachel Haule afariki dunia

Tanzia: Muigizaji Rachel Haule afariki dunia

your wrong kifo akina umaarufu wala kabwela kudanja ni kudanja tu

Sijasema kifo kina umaarufu...elewa logic ya post nzima, umaarufu ina maana una 'hali' nzuri kulinganisha na mama anayeshika jembe ili mkono uende kinywani huko vijijini..kuwa Dar kuna maana uko karibu na huduma za afya zenye kiwango kikubwa. Ukilinganisha hali hizo mbili, kama bado tunaweza kumpoteza mama na motto kwa ajili ya uzazi hapa Dar, imagine wangapi tunapoteza huko 'machokodo'!
 
uwii mmenilizaa kwa maranyingine tena.juz hapo muhimbil alifariki mpwa wang na watoto mapacha mara baad ya kijifungua.yote hiyo ilisababishwa na uzembe wa madaktar.
 
Umaskini ndiyo unaochangia vifo vingi vya akina mama na watoto.. Hospitali zetu hazina vifaa vya kutosha...

Ni kweli unachosema mkuu Bangoo ... lakini hali hiyo ni mbaya zaidi huko vijijini.
 
Last edited by a moderator:
Vifo vya kina mama na watoto wachanga vinavyotokana na uzazi...I don't think we are doing enough to reduce them! Sasa kama Dar hapa mtu maarufu anafariki kwa uzazi na hospitali zote zipo hizi...je mke wa 'mlalahoi' vijijini ndani ndani huko atapona!? Nini wajibu wetu na sisi wanaume!? Tupo tupo tu..wake/dada/shangazi/binti zetu wanakufa tu! RIP Recho.

uzazi wa siku hizi unamatatzo sana tafiti zinaonesha wanawake wengi nowdays wanazaa kwa operation sijui hosp zimegeuza mtaji ?anyway ni mipango ya mungu RIP Rechal so sad dah!
 
Yaani Bongo ujauzito kwa akina mama ni kama death penalty, ina maana huyo Daktari wake hakuwa anafahamu kama mgonjwa wake ana matatizo kipindi chote cha ujauzito wake?. Kwa kweli bado tuna safari ndefu!.
 
zamani ilikuwa mtu kujifungua kwa oparesheni na wachache sana wanawake walikuwa na nguvu sana ya kusukuma saivi kila mtu oparesheni duuuuu kizazi hiki laini mno
 
Halafu mbona siku hizi operation zimekuwa common sn nini tatizo? yani mkeo akifika hosptl akisumbua kidogo tu tayar wanakwambia sign hapa,KULIKONI?

Nilimpoteza rafiki yng mwaka jana pale Lugalo, Jesca daaa kama utani vile.RIP dada Recho na my best Jesca.

mmmh pole sana uzazi wa sikuhizi jaman yani kama ni ndugu yako mjamzito siku zake za kujifungua zimefika ni kumuomba mungu kwakweli !
 
tasnia hii imevamiwa na Israel mtoa roho!!
 
Wakati madaktari walipogoma kupigania mazingira mazuri ya kazi, wengi tuliwalaumu. Leo vifo vya wazazi na watoto vinapotokea, tunaendelea kuwalaumu madaktari......sijui TUKOJEE!! Tusisahau kumwomba Mungu, maana yule mshitaki wetu halali yuko kazini wakati wote! Ee Mwenyezi Mungu tusikie na Utuokoe!
Poleni wafiwa na wote tulioguswa na vifo hivi!
 
RIP, inasikitisha sana kuona vifo vya mama wajawazito vinaendelea. Mimi naona tuwe tunapewa statistics kila mwaka ya vifo vya watoto na akina mama wajawazito kama tunavyopewa statistics za kilomita za barabara zilizojengwa ili tujue performance ya serikali kulinganisha na nje nyingine. :shock::shock::shock:
 
attachment.php

R.I.P. Recho. mia
 

Attachments

  • RECHO.jpg
    RECHO.jpg
    67 KB · Views: 3,158
uzazi wa siku hizi unamatatzo sana tafiti zinaonesha wanawake wengi nowdays wanazaa kwa operation sijui hosp zimegeuza mtaji ?anyway ni mipango ya mungu RIP Rechal so sad dah!

Nashindwa kukanusha moja kwa moja...lakini pia nachelea kukubaliana nawe dada Munkari ... kutokana na maendeleo ya kisayansi na technolojia, imewezekana kuestablish trend jinsi ambavyo mja mzito aliye kwenye labor anaprogress ili kuzaa. Na hivyo mzalishaji (Daktari, nesi, mkunga, etc) anaweza kumonitor progress hiyo, na kuna viashiria wakati unamonitor progress kuwa huyo mja mzito anaprogress vizuri na atazaa katika muda muafaka au la. Hii pia inakuwezesha kuamua kuintervene kama kumuanzishia mama 'maji ya uchungu' ili kuaccelerate labor unapoona haprogress inavyotegemewa. Lakini pia kumonitor process kunasaidia kujua kuwa mama hatajifungua kawaida na hivyo kuitaji operation (Caeserean section). Na hii ni muhimu kuokoa wote...mama na motto (hasizaliwe kachoka akachelewa kulia akapata ulemavu wa ubongo na/au viungo). Ndio maana unaona siku hizi operations zinafanyika sana pindi unapoona inastahili..sio biashara!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom