TANZIA: Mwenzetu Heaven Sent kafiwa na baba yake mzazi mchana wa leo

TANZIA: Mwenzetu Heaven Sent kafiwa na baba yake mzazi mchana wa leo

Wanajamvi.

Kwa Masikitiko makubwa napenda kuwaataarifu Member mwenzetu Heaven Sent kafiwa na Baba ake Mzazi leo hii.

Kwa Mujibu wa Heaven anasema mzazi wake ameamka salama akiwa anajiandaa kwenda kazini alijiskia vibaya akasema acha apumzike kidogo ataenda baadae.

Gafla hali yake ikabadirika ikabidi akimbizwe Hospitalini Madktari walivyompima wakasema Presha iko juu.

Wakiwa wanaendelea kumpatia huduma hali ilizidi kuwa mbaya zaidi
hatimae Mzee akakata roho.

Raha Ya Milele Umpe Eeh Bwana, Na Mwanga Wa Ulimwengu Umwangazie, Apumzike Kwa Amani. Amen.
Pole sana ndugu yetu Heaven Sent, Mungu ampumzishe baba yetu kwa amani
 
Pole sana Dada Heaven sent. Sote tupo njia moja baba katangulia nasi tutafuata. Mwenyezi Mungu ailaze pahala pema peponi InshaAllah.
 
pole sana dada kwa kupoteza nguzo muhimu katika maisha in shaa allah allah (t.w) awape subira katika kipindi hiki kigumu.
 
Back
Top Bottom