Mjomba Fujo
JF-Expert Member
- Oct 27, 2012
- 2,602
- 6,754
Uzembe hamna mawasiliano.
Poleni Sana.TAARIFA YA AJALI YA TRENI YA UOKOAJI NA KIBERENGE NAMBA HDT-3
Dar es Salaam, Machi 23, 2020.
Uongozi wa Shirika la Reli Tanzania - TRC unasikitika kutangaza taarifa ya vifo vya watumishi wake
watano (5) kutokana na ajali ya treni ya uokoaji kugongana na Kiberenge Na. HDT - 3 katika eneo lililopo kati ya Stesheni ya Mwakinyumbi na Gendagenda katika reli inayotoka Ruvu Junction mpaka Mruanzi Junction, tarehe 22 Machi 2020.
Ajali hiyo imehusisha watumishi sita (6) wa TRC ambapo watumishi wane (4) walifariki eneo la ajali na majeruhi wawili (2) walifikishwa katika Hospitali ya Wilaya ya (Magunga) iliyopo Korogwe mkoani Tanga kwa ajili ya huduma za kitabibu, ilipofikia saa tano usiku (23:00) tarehe 22 Machi 2020 majeruhi mmoja (1) alifariki na kufikia jumla ya vifo vya watumishi watano (5) katika ajali hiyo.
Watumishi waliopoteza maisha katika ajali ni;
1. Ramadhani Gumbo – Meneja Usafirishaji Kanda ya Tanga
2. Eng. Fabiola Moshi – Meneja Ukarabati wa Mabehewa ya Abiria kanda ya Dar es Salaam
3. Joseph Komba – Meneja Msaidizi Usafirishaji Kanda ya Dar es Salaam
4. Philibert M. Kajuna – Mtaalamu wa Usalama wa Reli
5. George Urio - Dereva wa Kiberenge
Mpaka sasa majeruhi mmoja (1) Elizabeth Bona ambaye ni muongoza treni anaendelea na matibabu.
Aidha, uchunguzi wa kujumuisha kwa kushirikiana na taasisi nyingine utafanywa ili kubaini chanzo cha
ajali hii, uongozi unatoa pole kwa familia, jamaa, marafiki na watumishi wote wa Shirika la Reli Tanzania kwa msiba huu pia taarifa zaidi zitaendelea kutolewa kuhusu maandalizi ya kuhifadhi miili ya wapendwa wetu.
Bwana ametwaa na Bwana ametoa, jina lake lihidimiwe.
Jamila Mbarouk
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano TRC
View attachment 1396701
Ngoja nirudi nikaangalie kama ni kweli!!Poleni kwa msiba.Hiyo statement YAKO ya mwisho kwenye Hilo Tangazo la msiba wa TRC ilitakiwa uiandike hivi "BWANA AMETOA,NA BWANA AMETWAA " na sio 'BWANA AMETWAA NA BWANA AMETOA'
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa vyovyote vile kuna human error inayotokana na kutozingatia protocol au procedure za kufanya jambo flani.Kuna Harufu ya Uzembe kwenye huu Msiba, kuna WhatsApp, Simu, Telegram, Simu za Upepo nk nk halafu tupoteze wataalamu kizembe hivi hivi, HAPANA.
Kuna Harufu ya Uzembe kwenye huu Msiba, kuna WhatsApp, Simu, Telegram, Simu za Upepo nk nk halafu tupoteze wataalamu kizembe hivi hivi, HAPANA.
Ilikuwaje vyombo hivyo viwili vikaruhusiwa kuingia ktk 'section' wakati mmoja? Hakukuwa na mawasiliano?TAARIFA YA AJALI YA TRENI YA UOKOAJI NA KIBERENGE NAMBA HDT-3
Dar es Salaam, Machi 23, 2020.
Uongozi wa Shirika la Reli Tanzania - TRC unasikitika kutangaza taarifa ya vifo vya watumishi wake
watano (5) kutokana na ajali ya treni ya uokoaji kugongana na Kiberenge Na. HDT - 3 katika eneo lililopo kati ya Stesheni ya Mwakinyumbi na Gendagenda katika reli inayotoka Ruvu Junction mpaka Mruanzi Junction, tarehe 22 Machi 2020.
Ajali hiyo imehusisha watumishi sita (6) wa TRC ambapo watumishi wane (4) walifariki eneo la ajali na majeruhi wawili (2) walifikishwa katika Hospitali ya Wilaya ya (Magunga) iliyopo Korogwe mkoani Tanga kwa ajili ya huduma za kitabibu, ilipofikia saa tano usiku (23:00) tarehe 22 Machi 2020 majeruhi mmoja (1) alifariki na kufikia jumla ya vifo vya watumishi watano (5) katika ajali hiyo.
Watumishi waliopoteza maisha katika ajali ni;
1. Ramadhani Gumbo – Meneja Usafirishaji Kanda ya Tanga
2. Eng. Fabiola Moshi – Meneja Ukarabati wa Mabehewa ya Abiria kanda ya Dar es Salaam
3. Joseph Komba – Meneja Msaidizi Usafirishaji Kanda ya Dar es Salaam
4. Philibert M. Kajuna – Mtaalamu wa Usalama wa Reli
5. George Urio - Dereva wa Kiberenge
Mpaka sasa majeruhi mmoja (1) Elizabeth Bona ambaye ni muongoza treni anaendelea na matibabu.
Aidha, uchunguzi wa kujumuisha kwa kushirikiana na taasisi nyingine utafanywa ili kubaini chanzo cha
ajali hii, uongozi unatoa pole kwa familia, jamaa, marafiki na watumishi wote wa Shirika la Reli Tanzania kwa msiba huu pia taarifa zaidi zitaendelea kutolewa kuhusu maandalizi ya kuhifadhi miili ya wapendwa wetu.
Bwana ametwaa na Bwana ametoa, jina lake lihidimiwe.
Jamila Mbarouk
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano TRC
View attachment 1396701
POLISI WAZUNGUMZIA AJALI YA WAFANYAKAZI WA TRC:
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Leonce Rwegasira amethibitisha kutokea kwa tukio la ajali ya Wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Mkoa wa Tanga na kusababisha vifo vya watu watano katika Kitongoji cha Mgongola 'B' Tarafa ya Kabuku wilayani Handeni baada ya kiberenge walichokuwa wakisafiria kugongana na mabehewa ya treni.
Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospital ya Wilaya ya Korogwe huku majeruhi mmoja akiendelea kupatiwa matibabu katika hospital hiyo.