TANZIA: Taarifa kuhusu vifo vya watumishi watano (5) wa Shirika la Reli Tanzania(TRC)

Innalillahi wainna ilayhi rajiuun

ᴮᵉʷᵃʳᵉ ᵒᶠ ᵗʰᵉ ᶜᵒᵛⁱᵈ ⁻ ¹⁹ [emoji377]
 
Kuna Harufu ya Uzembe kwenye huu Msiba, kuna WhatsApp, Simu, Telegram, Simu za Upepo nk nk halafu tupoteze wataalamu kizembe hivi hivi, HAPANA.
Una ripoti ya uchunguzi.? Usiwe mwepesi wa kuhukumu wakati bado hauna ripoti kamili ya kilichotokea.
 
Pumziken kwa Aman, brother kajuna P
TAARIFA YA AJALI YA TRENI YA UOKOAJI NA KIBERENGE NAMBA HDT-3

Dar es Salaam, Machi 23, 2020.

Uongozi wa Shirika la Reli Tanzania - TRC unasikitika kutangaza taarifa ya vifo vya watumishi wake
watano (5) kutokana na ajali ya treni ya uokoaji kugongana na Kiberenge Na. HDT - 3 katika eneo lililopo kati ya Stesheni ya Mwakinyumbi na Gendagenda katika reli inayotoka Ruvu Junction mpaka Mruanzi Junction, tarehe 22 Machi 2020.

Ajali hiyo imehusisha watumishi sita (6) wa TRC ambapo watumishi wane (4) walifariki eneo la ajali na majeruhi wawili (2) walifikishwa katika Hospitali ya Wilaya ya (Magunga) iliyopo Korogwe mkoani Tanga kwa ajili ya huduma za kitabibu, ilipofikia saa tano usiku (23:00) tarehe 22 Machi 2020 majeruhi mmoja (1) alifariki na kufikia jumla ya vifo vya watumishi watano (5) katika ajali hiyo.

Watumishi waliopoteza maisha katika ajali ni;
1. Ramadhani Gumbo – Meneja Usafirishaji Kanda ya Tanga
2. Eng. Fabiola Moshi – Meneja Ukarabati wa Mabehewa ya Abiria kanda ya Dar es Salaam
3. Joseph Komba – Meneja Msaidizi Usafirishaji Kanda ya Dar es Salaam
4. Philibert M. Kajuna – Mtaalamu wa Usalama wa Reli
5. George Urio - Dereva wa Kiberenge

Mpaka sasa majeruhi mmoja (1) Elizabeth Bona ambaye ni muongoza treni anaendelea na matibabu.
Aidha, uchunguzi wa kujumuisha kwa kushirikiana na taasisi nyingine utafanywa ili kubaini chanzo cha
ajali hii, uongozi unatoa pole kwa familia, jamaa, marafiki na watumishi wote wa Shirika la Reli Tanzania kwa msiba huu pia taarifa zaidi zitaendelea kutolewa kuhusu maandalizi ya kuhifadhi miili ya wapendwa wetu.

Bwana ametwaa na Bwana ametoa, jina lake lihidimiwe.

Jamila Mbarouk
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano TRC
View attachment 1396701

POLISI WAZUNGUMZIA AJALI YA WAFANYAKAZI WA TRC:

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Leonce Rwegasira amethibitisha kutokea kwa tukio la ajali ya Wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Mkoa wa Tanga na kusababisha vifo vya watu watano katika Kitongoji cha Mgongola 'B' Tarafa ya Kabuku wilayani Handeni baada ya kiberenge walichokuwa wakisafiria kugongana na mabehewa ya treni.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospital ya Wilaya ya Korogwe huku majeruhi mmoja akiendelea kupatiwa matibabu katika hospital hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Peleni sana.
Yale madude yalivyo chuma chuma hadi kugongana na watu kufa kwa kweli speed ilikuwa kubwa sana
 
Mungu azilaze roho zao mahali pema
IMG_20200323_175446.jpeg
 
Sio mtaalamu wa mambo ya reli lakini ninahisi kabisa na kuamini kuna uzembe mahali,hakukua na mawasiliano na ushirikiano katika utendaji!
May they RIP!Africa risk ni nyingi mno!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TAARIFA YA AJALI YA TRENI YA UOKOAJI NA KIBERENGE NAMBA HDT-3

Dar es Salaam, Machi 23, 2020.

Uongozi wa Shirika la Reli Tanzania - TRC unasikitika kutangaza taarifa ya vifo vya watumishi wake
watano (5) kutokana na ajali ya treni ya uokoaji kugongana na Kiberenge Na. HDT - 3 katika eneo lililopo kati ya Stesheni ya Mwakinyumbi na Gendagenda katika reli inayotoka Ruvu Junction mpaka Mruanzi Junction, tarehe 22 Machi 2020.

Ajali hiyo imehusisha watumishi sita (6) wa TRC ambapo watumishi wane (4) walifariki eneo la ajali na majeruhi wawili (2) walifikishwa katika Hospitali ya Wilaya ya (Magunga) iliyopo Korogwe mkoani Tanga kwa ajili ya huduma za kitabibu, ilipofikia saa tano usiku (23:00) tarehe 22 Machi 2020 majeruhi mmoja (1) alifariki na kufikia jumla ya vifo vya watumishi watano (5) katika ajali hiyo.

Watumishi waliopoteza maisha katika ajali ni;
1. Ramadhani Gumbo – Meneja Usafirishaji Kanda ya Tanga
2. Eng. Fabiola Moshi – Meneja Ukarabati wa Mabehewa ya Abiria kanda ya Dar es Salaam
3. Joseph Komba – Meneja Msaidizi Usafirishaji Kanda ya Dar es Salaam
4. Philibert M. Kajuna – Mtaalamu wa Usalama wa Reli
5. George Urio - Dereva wa Kiberenge

Mpaka sasa majeruhi mmoja (1) Elizabeth Bona ambaye ni muongoza treni anaendelea na matibabu.
Aidha, uchunguzi wa kujumuisha kwa kushirikiana na taasisi nyingine utafanywa ili kubaini chanzo cha
ajali hii, uongozi unatoa pole kwa familia, jamaa, marafiki na watumishi wote wa Shirika la Reli Tanzania kwa msiba huu pia taarifa zaidi zitaendelea kutolewa kuhusu maandalizi ya kuhifadhi miili ya wapendwa wetu.

Bwana ametwaa na Bwana ametoa, jina lake lihidimiwe.

Jamila Mbarouk
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano TRC
View attachment 1396701

POLISI WAZUNGUMZIA AJALI YA WAFANYAKAZI WA TRC:

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Leonce Rwegasira amethibitisha kutokea kwa tukio la ajali ya Wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Mkoa wa Tanga na kusababisha vifo vya watu watano katika Kitongoji cha Mgongola 'B' Tarafa ya Kabuku wilayani Handeni baada ya kiberenge walichokuwa wakisafiria kugongana na mabehewa ya treni.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospital ya Wilaya ya Korogwe huku majeruhi mmoja akiendelea kupatiwa matibabu katika hospital hiyo.

mnapaswa mbadilike, hili shirika mnaliendesha kizamani sana, tumieni sayansi na teknolojia, nchi za wenzetu wanafahamu kabisa train fulani ipo njia fulani hivo inakuwa rahisi kuzi direct, msipobadilika hata hizo train za umeme zitaleta ajali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna Harufu ya Uzembe kwenye huu Msiba, kuna WhatsApp, Simu, Telegram, Simu za Upepo nk nk halafu tupoteze wataalamu kizembe hivi hivi, HAPANA.
...Tena harufu hiyo ya Uzembe in Kali sana! Ninavyojua kiberenge kilivyo, ninavyojua treni ilivyo, ninavyojua njia ya treni ilivyonyooka, treni linalokuja unaanza kulionea kuleee, na hata kama ni usiku taa ya treni unaanza kuiona kulee...inafikiaje hatua ya treni na kiberenge kukutana ghafla na kuua watu wetu Watano bila hats kutoa nafasi hats kwa mmoja wao kuweza kujitupa nje na kujiokoa na ajali hii???...hapa kuna neno na hiyo harufu ya Uzembe inazidi kuongezeka unavyozidi kujiuliza...!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haoooo wamepulizwaaaa
Watatui hawanaa mwezii wametokaa training NJE na makelele kibaoo walipofika wakapandishwa cheo GAFLA
Rip
 
Back
Top Bottom