TANZIA: Taarifa kuhusu vifo vya watumishi watano (5) wa Shirika la Reli Tanzania(TRC)

Hakuna kitakachosalia chini ya Jua,Wapumzike kwa Amani Marehemu Wote na wapate Nafuu majeruhi.Serikali imepoteza watu muhimu sana.
 
Poleni Sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hv ni kweli viberenge/sijui vimbweta vinakimbia speed kama Range au Benzi ama vinatembea kama Kobe ufafanuzi pls kwa anayejua....
 
Tuliumbwa kwa udongo na mavumbini tutarejea raha ya milele uwape eee bwana 😭

Mwaka 2001 mkoani Tabora ilibaki kidogo sana kiberenge kinipitie kwa kurudia kandambili zangu nilizovua katikati ya reli kabla ya kuingia kwenye treni ule msisimko na woga nilioupata siku ile umejirudia tena baada ya kusoma hii habari. 😢
 
Kuna Harufu ya Uzembe kwenye huu Msiba, kuna WhatsApp, Simu, Telegram, Simu za Upepo nk nk halafu tupoteze wataalamu kizembe hivi hivi, HAPANA.
Kwa vyovyote vile kuna human error inayotokana na kutozingatia protocol au procedure za kufanya jambo flani.
Mtu mmoja tu anaweza kuanzisha mtiririko wa matukio (sequence of events) yanayo sababisha na wengine kufanya makosa kisha ajali hutokea.

Unaweza kukuta mtu kavurugwa na jambo la kifamilia au kiuchumi au mgogoro kazini kisha anakosa umakini au anapuuzia, au amefanya kazi akiwa amechoka, au mtu kalewa, au amefanya kazi masaa mengi na muda unaoshauriwa kitaalamu.

Somo la Human Performance linazingatiwa sana katika usafiri wa anga ndio maana ajali chache sana sekta hiyo.
Kutokana na asili ya usafiri wa reli na zaidi hapa kwetu safari ni chache ilitakiwa ipite miongo minne (miaka 40) kabla haujasikia ajali za train zisizo husisha kugongana na magari, pikipiki na watembea kwa miguu.
 
Shirika halitawajibika

Treni ilikuwa kwenye njia yake

Ndivyo tulivyokaririshwa toka udogoni
 
Ilikuwaje vyombo hivyo viwili vikaruhusiwa kuingia ktk 'section' wakati mmoja? Hakukuwa na mawasiliano?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…