luckWill
Member
- Dec 21, 2015
- 34
- 96
Ninaandika haya nikiwa bado siamini kama ni kweli ni mimi leo hii ninaye pitia magumu haya ambayo yamesababishwa na mtu nilie mchukulia rafiki kama ndugu yangu.
Rafiki huyu kaniponza paka hivi sasa navyo andika hapa :-
ZAKAYO alinikuta nikiwa nikiwa na kazi yangu tu nilipo ajiriwa na alikuja akiwa anaomba hifadhi japo kwa muda aweze kupata kodi ya kulipia sehemu anayo ishi Kwakua mwenye nyumba wake kamfungia mlango.
Bwana ZAKAYO hatukuwa na mawasiliano ya kuonana mara kwa mara zaidi ya kuwasiliana kupitia mitandao ya kijamii tu na kila mtu akiendelea na harakati zake.
Miaka ya nyuma alikwama katika biashara zake alizokua anafanya mkoa fulani nyanda za juu nakuomba niweze kumpokea mkoa niliopo aje aweze kujaribu fursa ukanda huu, nami bila hiyana nkamkubalia ombi lake na akaja nkampokea na nikampa ofa pia ya kumlipia fremu ya biashara kwa kuanzia aweze kujipanga lakini alivyo kuja tayar alikua na mawazo mapya ya kusogea mjini zaidi ambapo alisema kapata rafiki aliemuunganisha na MC mashuhuri jijini aende akafanya kazi kwake, nami nikamkubalia na kusitisha kodi ile niliyokua nmemlipia nashukuru mwenye fremu alikua muelewa na kurudisha kiasi chote.
Na alipo kuja tena kwangu kwa mara hii ya pili baada ya kukwama tena Nilimkaribisha kwangu kwa moyo mmoja na kumudumia kwa chakula na gambe za hapa na pale bila shida yoyote kati yetu paka siku alipo mtambulisha rafiki etu ambae pia kwangu mimi nilipotezana nae muda mrefu sikuwa na mawasiliano nae ila namfahamu tumuite YUDA.
ZAKAYO na YUDA Waliishi kwangu kwa muda bila kuwaomba hata senti ya umeme wala maji kwakua niliamini ni wanachangamoto wanapitia na mi ka rafiki mzuri sina budi kuwabeba kwa chochote kinacho patikana tuna share Siku nikikosa tunalala tukiamini ipo siku mambo yatajipa
PICHA HALISI
Siku moja nikiwa katika kazi zangu mkoani napokea simu ya ZAKAYO Akinitaarifu kuwa YUDA amekamatwa na polisi nyumbani kwangu na amepelekwa kituo cha polisi kimoja hapa Dar kwa kosa la walilodai la wizi na shambulio la mwili kwa mtu aliekua mpenzi wake na ndugu zake wamefungua kesi wakidai fidia kuwa kaumizwa na pamoja kulipa gharama ya simu yake aliyokua nayo siku ya tukio.
ZAKAYO Anampa simu YUDA Na ananiomba niweze kumuazimia kokote kias cha Tsh 1,000,000 ili aweze kumalizana na ndugu zake na mpenzi wake na aweze kuachiwa ili taratibu za malipo ziendelee nje ya polisi na kuhaidi kuwa anamtuma ZAKAYO Kwao kwenda kuchukua simu Iphone 14 aliyotumiwa na kaka ake alieko Canada ili niweze kuiuza na kurudisha hela hio ambayo ilikua ya ofisi ninapo fanyia kazi.
Nami bila kutumia akili na kujua kua nasaidia niliweza kutuma kiasi hicho cha fedha ili rafiki zangu watoke na process zingine ziendelee kwa huyo mpenzi wake.
Kweli aliweza kutoka na akanishukuru sana kwa wema wangu na kusema wangeipeleka simu hio (iphone 14) dukani nilipokua nafanyia kazi ili iweze kutaftiwa mteja na mimi niweze kurudisha kiasi kile ofisini.
Tangu siku hio simu haikuletwa ofisini na nilivyorudi kutoka mkoani sikuwakuta nyumbani kwangu, nikafanya jitihada za kuonana nao na kuwasiliana ili atlist niweze kulipwa deni hilo kwani wanajua fika ni ya ofisi na kwa upande wangu nauguliwa na mwanangu kwa muda mrefu kusema ntaji balance niweze kurudisha deni hilo.
UKWELI WAJULIKANA
SIku moja nikiwa katika sehemu ya manunuzi ya nyumbani nakutana na mpenzi wake YUDA aliesemekana kaumizwa vibaya na kuibiwa simu yake ikiwa ni wiki tu tangu tukio litokee namuona akiwa mzima wa afya na simu yake akiwa nayo naijua kwakua ni mimi niliemuuzia simu ile, nampa pole na kumdadisi ni nini hasa kilitokea nae anakua na mshangao kwa kusikia taarifa hizo na kusema kua YUDA hawajawasiliana ni miezi sasa na walishaa achana kitambo na wala hakuna tukio lolote lilitokea kwake.
Nilipata ganzi iliyochanganyika na hasira laiti angetokea mmojawapo kati yao ZAKAYO AU YUDA Nahisi ningeandika mengine.
Nilipogundua tayari nmetapeliwa na kuamua kuwatafta niliambulia meseji za kejeli na kuishia ku blockiwa kotekote paka sasa nisijue wapi pa kuwapata marafiki wazandiki zangu hawa.
Mwaka umeanza na majuto mengi yaliyo changanyikana na hasira nyingi kwa kuwaamini watu niliowaona kama ndugu
Na popote walipo niwape pongezi tu kwa kunipitisha katika majaribu haya.
Niwape pole kwa uandishi mbovu lakini naamini ujumbe umefika na kuna la kujifunza katika kuwaamini watu tunao waita marafiki zetu.

- Sina kazi tena ya kuniingizia kipato
- Nakimbia kwangu kisa kodi
- Nauguliwa na mwanangu