Taqwa Foundation Yatoa Msaada wa Vifaa vya Skuli kwa Watoto Yatima, Ikiwasaidia Kujenga Mustakabali Bora

Taqwa Foundation Yatoa Msaada wa Vifaa vya Skuli kwa Watoto Yatima, Ikiwasaidia Kujenga Mustakabali Bora

Joined
Oct 26, 2024
Posts
5
Reaction score
0
DSC_0269.JPG


Na Zurima Ramadhan, Zanzibar

Jamii imetakiwa kuungana kwa pamoja kuwasaidia watoto yatima ili kujenga upendo na mshikamano baina yao.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Taqwa Foundation Zahra Issa Kassim wakati wa ugawaji wa vifaa vya skuli kwa watoto yatima huko Mpendae Wilaya ya Magharibi B.

Amesema kila mmoja analojukumu la kumsaidia yatima ili aweze kuishi katika maisha bora kama watoto wengine.

Msemaji wa Jumuiya hiyo Mwalim Muhammed Omar amesema lengo la jumuiya hiyo ni kuwasaidi watoto yatima wajane na wasojiweza ili kujikimu kimaisha.

Mlezi wa jumuiya hiyo Salma Khamis Salum amesema wameamua kuwasaidia watoto hao kwa kuwapa vifaa vya skuli ili kusoma katika mazingira mazuri na kutimiza malengo yao.

Naibu mlezi wa jumuiya hiyo Imadat Yussuf Juma amesema ni vyema kwa ndugu wa watoto hao kutowapeleka katika vituo vya kulelea watoto yatima ili kupata malezi bora na kukua katika maadili mema..

Mjumbe wa Jumuiya hiyo Juma Amour Khamis ameitaka jamii kushirikiana kwa pamoja katika kuwalea yatima ili kujikimu kimaisha pamoja na kupata radhi za Allah (sw).

Nao baadhi ya wazazi na watoto yatima wameishukuru Jumuiya hiyo kwa kuwapatia vifaa hivyo kwani vitawasaidia katika masomo yao.

Jumuiya ya taqwa foundation imetoa vifaa mbali mbali vya masomo ikiwemo fomu za skuli,mabuku, peni ili kuwasaidia watoto yatima katika harakati zao za kimasomo.
 
Back
Top Bottom