Taratibu woga umeanza kuwaondoka wananchi

Stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Posts
37,630
Reaction score
47,434
Wakati nikiwa katika harakati mjini hapa kwenye bandari ya salama.

Nikakutana na kundi kubwa la abiria , konda na dereva wa gari la abiria wakiwa wamemzunguka ofisa mmoja wa polisi.

Kutaka kujua kinachoendelea nikajifunza kwamba ile gari ya abiria ilikamatwa kwa kosa la kupakia abiria kwenye taa za barabarani.

Trafiki akawa hataki kumuandikia kosa lake dereva ila akataka awashushe abiria gari libakie pale alipomkamata.

Abiria kuona vile wakaamua wote kushuka na kumfuata kiongozi wa wale trafiki ili kujaribu kumtetea dereva maana waliona alikua anaonewa kwani hakufanya kosa hilo na pia wakataka amwandikie kosa lake pale na wao waendelee na safari yao.

Binafsi nilishitushwa mno na hali ile ya abiria wa basi zima kushuka na kumtetea dereva na konda wake kwa uonevu wa askari wa trafiki na nikalichukua jambo lile kama tahadhari kwamba, kidogo kidogo kutokana na ukali wa maisha Raia wameanza kukosa uvumilivu wa uonevu kwa wenye mmalaka.

Hii iwe kama a wake up call kwamba huko tunakoelekea kama tusipokua makini tutakuja shuhudia tusiyoyatarajia.

Ni vyema watawala wakatijahidi kuwaboreshea wananchi maisha yao kwani ukali wa maisha utawafanya washindwe kuhimili mikiki na kutoka nje kutaka kuondoa kila aina ya jambo wanodhani ni sababu ya wao kuwa na maisha magumu.

Hii ichukuliwe tu kama ushauri kwa wahusika na wala sio uchochezi wa namna yeyote ile.
 
Nikakutana na kundi kubwa la abiria , konda na dereva wa gari la abiria wakiwa wamemzunguka ofisa mmoja wa polisi...
Hakuna watu mandezi kama abiria wa kitz, siti ya watu wanne wanawekwa watano hakuna anaejali
 
Kwa hiyo abiria wa Arusha kwa Costa za Maji ya chai - Kikatiti-Boma ng'ombe - Moshi ni mandezi?
 
Hakuna watu mandezi kama abiria wa kitz, siti ya watu wanne wanawekwa watano hakuna anaejali
Biashara ya usafirishaji ni ngumu sn watu hatujui tu, unanunua tairi ya laki 3 kwenye coster wiki imepasuka na abiria wanataka gari sn muda wote na salama
 
Hata no matukio tu. Bongo za kibongo zikokatika singizi nono.
Hakuna MTU wa kuamka wala kuamsha mwenzake.
 
Wakati nikiwa katika harakati mjini hapa kwenye bandari ya salama.

Nikakutana na kundi kubwa la abiria , konda na dereva wa gari la abiria wakiwa wamemzunguka ofisa mmoja wa polisi...
Kupakia abiria kwenye mataa!?

Halafu abiria wakatetea na kuonekana mashujaa!

Ikitokea ajali ninyi ndio mtashusha nyuzi huku kuwalaumu askari na kuwasahau hao mashujaa wenu wavunja sheria

Sent from my SM-G5500 using JamiiForums mobile app
 
Wakati nikiwa katika harakati mjini hapa kwenye bandari ya salama.

Nikakutana na kundi kubwa la abiria , konda na dereva wa gari la abiria wakiwa wamemzunguka ofisa mmoja wa polisi.

Kutaka kujua kinachoendelea nikajifunza kwamba ile gari ya abiria ilikamatwa kwa kosa la kupakia abiria kwenye taa za barabarani.

Trafiki akawa hataki kumuandikia kosa lake dereva ila akataka awashushe abiria gari libakie pale alipomkamata.

Abiria kuona vile wakaamua wote kushuka na kumfuata kiongozi wa wale trafiki ili kujaribu kumtetea dereva maana waliona alikua anaonewa kwani hakufanya kosa hilo na pia wakataka amwandikie kosa lake pale na wao waendelee na safari yao.

Binafsi nilishitushwa mno na hali ile ya abiria wa basi zima kushuka na kumtetea dereva na konda wake kwa uonevu wa askari wa trafiki na nikalichukua jambo lile kama tahadhari kwamba, kidogo kidogo kutokana na ukali wa maisha Raia wameanza kukosa uvumilivu wa uonevu kwa wenye mmalaka.

Hii iwe kama a wake up call kwamba huko tunakoelekea kama tusipokua makini tutakuja shuhudia tusiyoyatarajia.

Ni vyema watawala wakatijahidi kuwaboreshea wananchi maisha yao kwani ukali wa maisha utawafanya washindwe kuhimili mikiki na kutoka nje kutaka kuondoa kila aina ya jambo wanodhani ni sababu ya wao kuwa na maisha magumu.

Hii ichukuliwe tu kama ushauri kwa wahusika na wala sio uchochezi wa namna yeyote ile.
Hao polisi walikuwa na Bunduki, vifaru, na gari za washa washa??
 
Sio Ukraine na Poland
Nchi zote zilizokuwa zinafuata sera za kijamaa / sociolism wananchi hawajitambui.

[emoji817]% kubwa hawajitambui na hawajui kudai haki zao
 
Uko sahihi kabisa, maana mfumo wa kijamaa hutengeneza waoga na wasujudu viongozi. Na wananchi wengi hauaminishwa kuwa viongozi ndio wenye akili na suluhu ya matatizo yao. Na ukiwa na mtazamo tofauti na mfumo huo kukutana na kifo, kwenda jela, kuhujumiwa shughuli zako za kukuingizia kipato ni jambo la kawaida kabisa. Na ukidai haki yako wananchi waliomezeshwa uoga hukuona kama mchochezi.
 
Nchi zote zilizokuwa zinafuata sera za kijamaa / sociolism wananchi hawajitambui.

[emoji817]% kubwa hawajitambui na hawajui kudai haki zao
Mambo yanabadilika mkuu;

Nimeshtushwa sana na guts za hao abiria kumzunguka afisa wa polisi na kumtetea dereva.

Hilo sio jambo dogo hata kidogo.

Ni ishara ambayo haitakiwi kupuuzwa.
 
Ishu Kama hii mara ya mwisho nami nimeshuhudia imefanyika Njombe 2011 lakin mpaka leo hakuna jipya.

Watanzania wataamkaje na waamke ili iwe nini na tupo uchumi wa kati?
Tatizo kubwa la Mbongo Kama hampendi Kiongozi alioko madarakani muda wote anaishi kwa fantasies kuwa Wananchi wataandamana wamtoe madarakani.

Au zitatokea vurugu kubwa sana na majanga ili nchi imshinde Rais.

Muda wote unakuwa unatamani yatokee mabaya.

In short, Dar kwa Hilo Ni Jambo la kawaida na hufanyika kila siku.

Dar usafiri Ni shida sana na kero kubwa.

Na Mara nyingi watu huwa wanataka kuwahi kazini au nyumbani.

Ukimkamata dereva, halafu abiria wakaona unaongea naye sana huku wao umewaweka pembeni lazima watashuka kuja ku-shout.

Na hapo watataka option Kama:
  • Either Kama dereva ana kosa ,waaandikiwe fine waondoke
  • Kama hawajalipa nauli, wanashuka na kupanda gari jingine
 
Wajuaji huwa hamkosekani kila mahali.
 
Wakati nikiwa katika harakati mjini hapa kwenye bandari ya salama.

Nikakutana na kundi kubwa la abiria , konda na dereva wa gari la abiria wakiwa wamemzunguka ofisa mmoja wa polisi.

Kutaka kujua kinachoendelea nikajifunza kwamba ile gari ya abiria ilikamatwa kwa kosa la kupakia abiria kwenye taa za barabarani.

Trafiki akawa hataki kumuandikia kosa lake dereva ila akataka awashushe abiria gari libakie pale alipomkamata.

Abiria kuona vile wakaamua wote kushuka na kumfuata kiongozi wa wale trafiki ili kujaribu kumtetea dereva maana waliona alikua anaonewa kwani hakufanya kosa hilo na pia wakataka amwandikie kosa lake pale na wao waendelee na safari yao.

Binafsi nilishitushwa mno na hali ile ya abiria wa basi zima kushuka na kumtetea dereva na konda wake kwa uonevu wa askari wa trafiki na nikalichukua jambo lile kama tahadhari kwamba, kidogo kidogo kutokana na ukali wa maisha Raia wameanza kukosa uvumilivu wa uonevu kwa wenye mmalaka.

Hii iwe kama a wake up call kwamba huko tunakoelekea kama tusipokua makini tutakuja shuhudia tusiyoyatarajia.

Ni vyema watawala wakatijahidi kuwaboreshea wananchi maisha yao kwani ukali wa maisha utawafanya washindwe kuhimili mikiki na kutoka nje kutaka kuondoa kila aina ya jambo wanodhani ni sababu ya wao kuwa na maisha magumu.

Hii ichukuliwe tu kama ushauri kwa wahusika na wala sio uchochezi wa namna yeyote ile.
gang unatetea dala2 kupandisha abiria kwenye traffic light? maajabu haya.
 
Back
Top Bottom