Taratibu woga umeanza kuwaondoka wananchi

Taratibu woga umeanza kuwaondoka wananchi

Huu nao ni ujinga wa Watz! Hivi unawezaje kumtetea dereva mpuuzi anayekiuka taratibu na Sheria za barabarani??. Wameshindwa kuandamana tupate katiba mpya au KUPUNGUZA gharama za maisha? Afu wanakuja kuandamana au kuzuia askari kutimiza wajibu wake?. Upuuzi
 
Mambo yanabadilika mkuu;

Nimeshtushwa sana na guts za hao abiria kumzunguka afisa wa polisi na kumtetea dereva.

Hilo sio jambo dogo hata kidogo.

Ni ishara ambayo haitakiwi kupuuzwa.
Mkuu Gari umepaki wapi? Angalia usije Pata degedege bongo mistuko mingi mno
 
Jambo hili halihusiani na ukali wa maisha
Wakati nikiwa katika harakati mjini hapa kwenye bandari ya salama.

Nikakutana na kundi kubwa la abiria , konda na dereva wa gari la abiria wakiwa wamemzunguka ofisa mmoja wa polisi.

Kutaka kujua kinachoendelea nikajifunza kwamba ile gari ya abiria ilikamatwa kwa kosa la kupakia abiria kwenye taa za barabarani.

Trafiki akawa hataki kumuandikia kosa lake dereva ila akataka awashushe abiria gari libakie pale alipomkamata.

Abiria kuona vile wakaamua wote kushuka na kumfuata kiongozi wa wale trafiki ili kujaribu kumtetea dereva maana waliona alikua anaonewa kwani hakufanya kosa hilo na pia wakataka amwandikie kosa lake pale na wao waendelee na safari yao.

Binafsi nilishitushwa mno na hali ile ya abiria wa basi zima kushuka na kumtetea dereva na konda wake kwa uonevu wa askari wa trafiki na nikalichukua jambo lile kama tahadhari kwamba, kidogo kidogo kutokana na ukali wa maisha Raia wameanza kukosa uvumilivu wa uonevu kwa wenye mmalaka.

Hii iwe kama a wake up call kwamba huko tunakoelekea kama tusipokua makini tutakuja shuhudia tusiyoyatarajia.

Ni vyema watawala wakatijahidi kuwaboreshea wananchi maisha yao kwani ukali wa maisha utawafanya washindwe kuhimili mikiki na kutoka nje kutaka kuondoa kila aina ya jambo wanodhani ni sababu ya wao kuwa na maisha magumu.

Hii ichukuliwe tu kama ushauri kwa wahusika na wala sio uchochezi wa namna yeyote ile.
 
Huu nao ni ujinga wa Watz! Hivi unawezaje kumtetea dereva mpuuzi anayekiuka taratibu na Sheria za barabarani??. Wameshindwa kuandamana tupate katiba mpya au KUPUNGUZA gharama za maisha? Afu wanakuja kuandamana au kuzuia askari kutimiza wajibu wake?. Upuuzi
Piga virungu tu hao
 
Back
Top Bottom