Taratibu za kampuni kupata namba ya lipa kwa Mpesa/tigo pesa

Taratibu za kampuni kupata namba ya lipa kwa Mpesa/tigo pesa

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Habari wakuu.

Nipo mbali na ofisi za hii mitandao. Naomba kujua taratibu za kampuni kupata namba za lipa kwa mpesa/tigopesa. Natanguliza shukrani.
 
Kupata lipa kwa mpesa au hiyo nyingine ya tigo ikiwezekana na selcom fika katika shop husika mfano vodashop ukiwa na leseni ya biashara kutoka TRA pamoja na kiambatanisho kimoja wapo au zaidi kati ya hivi leseni ya udereva, kitambulisho cha taifa/Uraia, kitambulisho cha mpiga kura, kitambulisho cha Mzanzibari mkaazi au namba ya NIDA.

Mengine utapata utaratibu katika shop husika ili kumbuka leseni ya biashara pamoja na viambatanisho hivyo ni muhimu maana hizo lipa ni kwaajili ya watu wenye biashara zilizo registed TRA
 
KWA HUKU MOSHI,KAMPUNI ZA SIMU HUWA ZINATUMA VIJANA MITAANI KWAAJILI YA KUSAJILI HIZO HUDUMA ZA LIPA KWA - PESA
KWA WAFANYABIASHARA AIDHA MADUKA, BAR, HOTEL, PHARMACY AU HOSPITAL.
 
Naomba kuuliza wakuu,,Kuna mtu alinisajilia Line ya lipa kwa simu,tayari nilishatumiwa sms kuhusu kukamilika kwa line yangu na kubadilisha pasword lakini kupata ile Namba ya Malipo imekua changamoto,,Je Nikienda Vodashop wanaweza kuiona Kwenye system???
 
Siku hizi naona mawakala nao wamekuwa wajanja sana,ukienda kutoa pesa wanakwambia usiingie kwenye toa pesa,ingia lipa kwa Tigo Pesa/M-Pesa, andika kiasi flani,kama una elfu 63 wanakwambia andika elfu 62 halafu hapo wewe anakukabidhi elfu 59
 
Hivyo ni kwa wale wanaokwepa makato ya mpesa au tigo pesa lakini kama unalipa bidhaa ni free mandela
 
Back
Top Bottom