Ni kweli kazi yao ni kutoa leseni na kutoza faini pia lakini ww tu fika ofisini ujitetee ukiwambia kuwa ulikuwa hufahamu namna ya kulipia leseni na unapenda kutoa michango ya maendeleo na hapo hapo uwaambie kuwa mtaji wako ni mdogo huwez kupata hata cash hyo wanayoidai kama faini na endapo ikitokea ukaipata utakuwa umefunga biashara hautakuwa na pa kuanzia tena... Ongea nao yataisha hao hawana ubaya zaidi kama tra maana manispaa ikishindikana unazuiwa kufanya biashara kwenye wilaya yao lakn tra ndo wabaya zaidi wakiamua wanakufilisi sekunde moja tu.
NB: Inategemea na kadirio la manispaa hiyo ktk leseni maana zinatofautiana viwango vya tozo wilaya zngne ni Tsh,20,000 , 50,000 , _200,000 na kuendelea. Ongea nao ila uwe mpole ukiwa unaongea nao usijfanye mjuaji sana ila chunga haki zako tu usikandamizwe wala kuonewa maana kuhoji na kutoa maoni ni haki yako na wewe ndo boss wao kama mteja so simamia haki usitetereke.