FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 38,920
- 44,970
Nimegundua sasa ni kwanini watu wananunua viwanja kisha wanaendelea kutumia hati zenye majina ya watu wengine bila kubadilisha majina.
1.) Hivi inakuwaje mtu anunue kiwanja milioni 50 kisha report ya valuation iseme kwamba kina thamani ya 200mil.?! Kama kweli kinathamani hiyo kwanini mtu auze mulioni 50? Hatukatai wapo watu wanadanganya bei kwenye mikataba, lakini bei za valuation hata ukisema utafute madalali wahangaike na hicho kiwanja mwaka mzima huwezi pata mnunuzi, maana bei ya valuation lazima iangalie na hali halisi ya soko kwa wakati husika, jitu linakaa tu ofisini linaanza kupiga hesabu za kufikirika eti hapa ni laki 2 kwa square meter, hapa lazima kifanyike kitu, huu ni mkanganyiko unaoshawishi sana watu kutoa rushwa na kuwaneemesha valuers.
2.) Manispaa napo wanataka 3% huko sijui, huko utapeleka document kiroba kizima, na hapo utalipa mwanasheria pesa kwa % vile vile, cha kushangaza huko manispaa unaweza ukapeleka vikorokoro vyote na ukasubiri hadi ukasahau, uchekeweshwaji ni mkubwa, ila ukitoa grease tu, unashangaa zoezi la miezi linachkua dakika 10 tu umeshapewa control number, na ukilipa tu kibali unapewa hapo hapo, kwanini pasiwe na kanuni, kwamba mtu akileta application isizidi masaa 24 apewe control number alipie na apate kibali, pawe na kanuni, isiwe utashi wa watumishi, inachochea watu kutoa rushwa!
3.) Ukitoka hapo jiandae na TRA, kama mkataba ni wa 2022 kurudi nyuma, basi kama valuer alisema kiwanja ni milioni 200, hata kama ulinunua milioni 30, hapo ujue 10% inakuhusu, yaani ulipe 20 milion! Kwa style hii mnatoa mshawasha wa watu kutoa grease na kuneemesha watumishi, na hata ukilipa kama hutoi grease, hiyo Tax clearance utaisikia kwenye ndoto tu.., ni too much..,
3.) Ardhi ndio sina hata hamu ya kuwazungumzia, nawaacha tu.., mwisho wa siku ni bora hata ulipe mtu milioni 5 afanye ike kazi ya nenda rudi kila siku hapo Ardhi, ili angalau wewe uendelee na shughuli zako za kukuinguzia kipato.
Soma Pia: Umuhimu wa Kumuunganisha Msajili wa Hati Miliki (Registrar of Titles) Kwenye Kesi ya Ardhi Ambayo Kiwanja Kimesajiliwa na Kina Hati
Mimi nashauri hizi taasisi zote za kuhamisha hati miliki ziwekwe chini ya ofisi moja maalum yenye maafisa toka taasisi zote hizo, mtu ukiingia isizidi wiki uwe na hati yako, tunatesana mno.