Huwezi ku-formulate hiyo barua hapahapa Bongo? Wanathibitisha vipi kuwa barua imetoka nje?
Nchi zinazotuzunguka huulizwi unataka passport ya nini utajijua mradi una kitambulisho cha taifa wanakupa
Kifupi passport ni chanzo kizuri.cha uhakika cha kuingiza mapato ya serikali
Wangesema kila mwenye kitambuñisho cha NIDA achukue passport wangepata mabilioni ya pesa ndani ya muda mfupi tu
Passport haitakiwi tu kwa ajili ya safari wamekaa kizamani mno mitihani mingi ya online hutaka uwe na passport kuna sehemu ya kujaza pia ukiomba scholarship online zinataka ujaze passport details pia ukiomba kazi za nje au tenda nje ya nchi online unatakiwa kujaza passport details
Hata ukienda tu british council ukitaka kufanya mitihani yao online kuna sehemu ya kujaza passport details
Hata ukikutana na mwekezaji wa maonyesho ya biashara wanaokuja nchini ukita kuingia ubia naye au biashara atakudai nyaraka za biashara lakini pia lazima umuonyeshe passport yako achukue details
Uhamiaji wako nyuma mno wanadhani psssport kwa sasa unatakiwa kuwa nayo ukiwa na safari tu!!!
Wizara mpya ya teknolojia hebu nenfeni mkawaeleweshe hao uhamiaji kazi ya passport kwenye ulimwengu wa leo wa kidigitali kawapeni semina hawaelewi wako kule enzi za kutaka passport kwa ajili ya Safari.