Taratibu za mikopo ya chuo zinasemaje katika hali kama hii

Taratibu za mikopo ya chuo zinasemaje katika hali kama hii

Bra-joe

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
1,628
Reaction score
1,124
Habari wana jamvi?

Kuna ndugu yangu amemaliza chuo fulani. Mara tu baada ya kuanza chuo, aliniomba nimsaidie fedha za kujikimu kwani mkopo wake haujatoka. Nilimsaidia, baada ya muda kidogo aliniomba nimsaidie fedha ili alipe ada kwa kuwa wanakaribia kufanya mitihani ya semista ( alikuwa akizitaja mara ya 1 mara 3 mara 2) na asipolipa hataruhusiwa kufanya hiyo mitihani.

Nilifanya hivyo kwa kipindi chote alipokuwa chuo. Sasa amemaliza chuo, anadai chuo kinamdai milioni 3 na kimezuia vyeti vyake mpaka atakapolipa hizo milioni. Kaniomba tena nimsaidie, akipata kazi atanirudishia.

Maswali yangu kwa waliyopita vyuo:

1. Je, chuo kinapokea wanafunzi hata kama mkopo haujatoka?

2. Mkopo unaweza usitoke mpaka mwanafunzi anamalize chuo?

3. Je, chuo kinaweza kumruhusu mwanafunzi anaye daiwa ada kufanya mitihani yake ya mwisho?

4. Je, ni utaratibu wa vyuo kuzuia vyeti vya wanaodaiwa ada?

Ni hayo tu ndugu zangu. Natanguliza shukrani.
 
Kwanza kabisa chuo kinapokea mwanafunzi yeyote aliyechaguliwa kujiunga chuo husika regardless ana mkopo au hana.... wanachojua wao ulipe ada tu baaas... that means kama una mkopo utalipa ile sehemu yako iliyobaki (kama unalipiwa na bodi asilimia sabini utatakiwa kulipa asilimia 30 iliyobaki ndipo usajiliwe chuoni) ile inayobaki ni kazi ya bodi kuiingiza kwenye system ya chuo......

Huwa yanatokea makosa ya kiufundi bodi haiingizi ada ya mwanafunzi husika na mara nyingi mtu huyo atakuja kugundua mwishoni wakati wa clearence (kwa uzoefu wangu).

Ikitokea hivyo atatakiwa kufuatilia hela yake huko bodi lakini ni process ndefu hadi mtu ukafanikiwe sio leo ndio maana wengi huwa wanaamua kutoa hela yao ya mfukoni kama wanayo ili wachukue cheti.

Bila kumaliza deni cheti huchukui hakika.
 
Huyo jamaa muongo mbane akupe hela, haiwezekani toka umeanza hadi unamaliza chuo mkopo haujawahi kutoka? Labda kama yupo chuo cha mifugo SUA.
 
Wewe unasema labda chuo cha mifugo SUA umesikia SUA ni chuo cha ufugaji???????mtu kaomba msaada badala ya kumsaidia unaingizia jokes kwani SUA kimekufanyaje?au ulitamani kusoma hapo ukakosa nafasi???????

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Wewe unasema labda chuo cha mifugo SUA umesikia SUA ni chuo cha ufugaji???????mtu kaomba msaada badala ya kumsaidia unaingizia jokes kwani SUA kimekufanyaje?au ulitamani kusoma hapo ukakosa nafasi???????

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

Most likely ndugu yetu alikosa sifa za kupata admission kwa hiyo kaona mbora akandie (kabla mtu hajauliza; Mimi sijasoma SUA kwa hiyo sina sababu ya kukitetea ila naeleza ninachokijua kuwa ni ukweli mtupu).
 
Mkuu hapo fuatilia ,na yeye pia akiwepo yaa mfuatilie wote yawezekana ikawa ni true..bt anythng can be happening.
 
Back
Top Bottom