Bra-joe
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 1,628
- 1,124
Habari wana jamvi?
Kuna ndugu yangu amemaliza chuo fulani. Mara tu baada ya kuanza chuo, aliniomba nimsaidie fedha za kujikimu kwani mkopo wake haujatoka. Nilimsaidia, baada ya muda kidogo aliniomba nimsaidie fedha ili alipe ada kwa kuwa wanakaribia kufanya mitihani ya semista ( alikuwa akizitaja mara ya 1 mara 3 mara 2) na asipolipa hataruhusiwa kufanya hiyo mitihani.
Nilifanya hivyo kwa kipindi chote alipokuwa chuo. Sasa amemaliza chuo, anadai chuo kinamdai milioni 3 na kimezuia vyeti vyake mpaka atakapolipa hizo milioni. Kaniomba tena nimsaidie, akipata kazi atanirudishia.
Maswali yangu kwa waliyopita vyuo:
1. Je, chuo kinapokea wanafunzi hata kama mkopo haujatoka?
2. Mkopo unaweza usitoke mpaka mwanafunzi anamalize chuo?
3. Je, chuo kinaweza kumruhusu mwanafunzi anaye daiwa ada kufanya mitihani yake ya mwisho?
4. Je, ni utaratibu wa vyuo kuzuia vyeti vya wanaodaiwa ada?
Ni hayo tu ndugu zangu. Natanguliza shukrani.