Taratibu za utumishi wa umma zinaruhusu mwalimu kufanya biashara darasani kwa wanafunzi anaowafundisha?

Habari za asubuhi wanajamvi,

Samahani naomba kujuzwa ikiwa kanuni na taratibu za utumishi wa umma zinaruhusu Kwa waalimu kufanya biashara darasani Kwa wanafunzi anaowafundisha?

Kwa ufupi ni kwamba kuna shule moja ipo mkoani Morogoro, wilaya ya Morogoro DC ambapo mwezi January niliwahamishia wanangu wakitokea Mkoani Rukwa tulikokua tukiishi.

Tangu wameanza shule hapo kumekua na mabadiliko kidogo ya kitabia kwa wanangu, wamekua na tabia ya kuomba sana pesa asubuhi wanapotoka kwenda shule kitu ambacho hawakua nacho mwanzo na usipowapa wanakosa amani kabisa.

Sasa katika kufuatilia nini chanzo cha mabadiliko hayo kitabia nikagundua kuwa Kuna mwalimu wa chekechekea anauza maandazi na vitu vingine humo darasani Tena anaweka juu ya meza pale ndo anapendelea kufundisha huku anauza tena kwa kupromote biashara yake.

Sasa hili limenifikirisha nimeona nililete hapa tulijadili Kwa pamoja 🙏🙏🙏
Muache mwalimu atumie fursa. Maana anayatumia madhaifu yako, kuwasaidia watoto wako kusoma bila njaa.

Kama hao watoto wako wangekuwa wanapata breakfast nzito asubuhi kabla ya kuondoka kwenda shule, nadhani wasingehangaika na hayo maandazi ya mwalimu.
 
Habari za asubuhi wanajamvi,

Samahani naomba kujuzwa ikiwa kanuni na taratibu za utumishi wa umma zinaruhusu Kwa waalimu kufanya biashara darasani Kwa wanafunzi anaowafundisha?

Kwa ufupi ni kwamba kuna shule moja ipo mkoani Morogoro, wilaya ya Morogoro DC ambapo mwezi January niliwahamishia wanangu wakitokea Mkoani Rukwa tulikokua tukiishi.

Tangu wameanza shule hapo kumekua na mabadiliko kidogo ya kitabia kwa wanangu, wamekua na tabia ya kuomba sana pesa asubuhi wanapotoka kwenda shule kitu ambacho hawakua nacho mwanzo na usipowapa wanakosa amani kabisa.

Sasa katika kufuatilia nini chanzo cha mabadiliko hayo kitabia nikagundua kuwa Kuna mwalimu wa chekechekea anauza maandazi na vitu vingine humo darasani Tena anaweka juu ya meza pale ndo anapendelea kufundisha huku anauza tena kwa kupromote biashara yake.

Sasa hili limenifikirisha nimeona nililete hapa tulijadili Kwa pamoja 🙏🙏🙏
Kila siku Serikali inapiga marufuku haya mambo lakini Walimu hawaelewi tuu zwakifukuzwa watasema wamwonewa.
 
Si rahisi kuukimbia Uzi , lengo lilikua ni kutakua kuelewa miongozo inasemaje lakini nilichogundua wote waliojibu hapo hawajui miongozo Bali wamejibu tu Kwa mihemko
Sasa kama hiyo miongozo na sheria ingefuatwa kama unavyotaka kwenye hii nchi, basi rushwa na ufisadi visingetamalaki.
 
Wapeleke wanao private schools.
Beer moja Ni sh 2000 unakunywa bia tano lkn unashindwa kumpa mwanao pocket money Mia tano.
 
Back
Top Bottom