Tarehe 1 Aprili ni siku ya wajinga au ya waongo?

Tarehe 1 Aprili ni siku ya wajinga au ya waongo?

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Nashangaa bado kuna watu wanaiita tarehe 1 Aprili, "Fools' day," au siku ya wajinga. Siku hii ingefaa zaidi kuitwa siku ya waongo kwa sababu watu wengi wanaongea uongo ifikapo Aprili Mosi.

Kama umekuwa ukiitumia tarehe 1 Aprili kusema au kuandika habari za uongo basi ujue baba yako ni Ibilisi(shetani).
Yohana 8:44
Ninyi ni wa baba yenu Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa uongo.

Maandiko hayo yanaonyesha wazi kuwa mwanzilishi wa uongo ni shetani na wanaopenda kusema uongo ni watoto wa ibilisi.

Uongo ni uongo tu, hata kama mwandishi wa uongo anadai anaadhimisha siku ya wajinga. Uongo unabaki kuwa uongo tu, hata kama anayesema uongo analenga kuchekesha au kufanya mzaha.

Ndugu, jitenge na uongo. Midomo ya uongo ni chukizo kwa Bwana(Mithali 12:22) ndiyo sababu waongo adhabu yao ni kutupwa katika moto wa milele.
"Waoga, wasioamini, wachafu, wauaji, wazinzi, wachawi, waabudu sanamu, pamoja na waongo wote, mahali pao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.” (Ufunuo 21:8)
 
Madhara ya uongo:
  • Uongo unaweza kusababisha ugomvi, chuki, na hata kuvunja ndoa, urafiki, au uhusiano wa kifamilia.
  • Watu wakiamini uongo, wanaweza kufanya maamuzi mabaya
  • Habari za uongo zinaweza kusababisha hofu isiyo ya lazima kwa jamii nzima.
  • Uongo unaweza kusababisha chuki kati ya makundi ya watu, kuleta migogoro au hata vita.
  • Taarifa za uongo zinaweza kusababisha kuporomoka kwa biashara, kushusha thamani ya soko, au hata kusababisha watu kupoteza kazi.
Mithali 19:9 – "Shahidi wa uongo hatakosa adhabu, naye asemaye uongo ataangamia."
 
Wengine tutaendelea na shughuli zetu kama kawaida wala hapatakuwepo wa kutudanganya
 
Umeweka hoja yenye uzito wa kiroho kuhusu dhana ya kusema uongo hata kwa mzaha, hasa katika muktadha wa Aprili Mosi. Inaonekana una msimamo thabiti wa kidini kuhusu uaminifu na ukweli.

Kuna watu wanaochukulia siku hii kama burudani isiyo na madhara, ilhali wengine wanaiona kama uhalalishaji wa uongo, jambo ambalo halipatani na maadili ya kiroho. Biblia inasisitiza kuwa uongo ni chukizo kwa Mungu, na maandiko uliyotaja yanaunga mkono hilo.

Kwa hiyo, kwa mtu anayefuata mafundisho ya Biblia kikamilifu, Aprili Mosi haipaswi kuwa siku ya mzaha wa uongo, bali fursa ya kusimama katika ukweli daima. Ni jambo la kufikiria kwa kina kuhusu namna tunavyotumia maneno yetu na jinsi tunavyoshiriki katika tamaduni mbalimbali.
 
Umenena vema
 
Mtu akisema uongo kisha akasema alikuwa anafanya mzaha tu, mtu huyo anafananishwa na mwendawazimu!

Mithali 26:18-19
"Kama mwendawazimu atupaye mishale ya moto ya kufisha, ndivyo alivyo mtu amdanganyaye jirani yake na kusema, “Nilikuwa nafanya mzaha tu!”
 
Kutoka 20:16
Usimshuhudie jirani yako uongo.
 
Dini tu ndo kitu pekee sisi Waafrika tumekishupalia kwelikweli kutoka kwa wakoloni.
Umechanganya masomo, mkuu. Pitia pitia tena notes zako za somo la Historia. Ukristo ulianzia Israeli katika karne ya 1 BK, ukaenezwa na Yesu Kristo na wanafunzi wake. Waisraeli hawajawahi kuwa wakoloni kwa maana ya kuanzisha na kuleta ukoloni kama walivyofanya mataifa ya Ulaya(Waingereza, Wajerumani, Wafaransa, Wareno, na Wahispania).
 
Watu wengi wameshaikataa hii April Fool ila shetani kwa ubunifu wake kwa kuleta kitu kinaitwa PRANK ambayo ni mbaya kuliko uongo wa April Fool.
 
Zaburi 101:7
Mwongo yeyote hatakaa nyumbani mwangu; hakuna msema uongo atakayekaa kwangu.
 
Waefeso 4:25
Kwa hiyo, acheni uongo. Kila mmoja anapaswa kumwambia mwenzake ukweli, maana kila mmoja wetu ni kiungo cha mwili wa Kristo.
 
Wakolosai 3:9
Msiambiane uongo, kwa maana mmevua kabisa utu wenu wa kale pamoja na matendo yake
 
Mithali 6:16-19
Kuna vitu sita anavyovichukia Mungu, naam, viko saba vilivyo chukizo kwake: macho ya kiburi, ulimi udanganyao, mikono imwagayo damu isiyo na hatia, moyo uwazao mipango miovu, miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu, shahidi wa uongo asemaye uongo, na mtu anayechochea fitina kati ya ndugu.
 
Back
Top Bottom