Asante kwa kuniona kama Ahlul Kitaab. Ni kweli, naamini Maandiko matakatifu yaliyoletwa na Mungu.
Hata hivyo, imani yangu haikomei tu kwenye 'kitabu' au maandiko – bali iko kwa Yesu Kristo aliye Neno la Mungu aliyefanyika mwili. Naamini kwamba Mungu alijifunua kwetu mwenyewe kwa njia ya Yesu Kristo – aliye zaidi ya nabii. Yesu ni Mwana wa Mungu aliye hai.