Tarehe 17 March 2021, Makamu wa Rais akitangaza kifo cha aliyekuwa rais Ndugu Hayati Magufuli ulikuwa wapi?

Tarehe 17 March 2021, Makamu wa Rais akitangaza kifo cha aliyekuwa rais Ndugu Hayati Magufuli ulikuwa wapi?

Ilikuwa ni form 6, tunakaza msuli kukitafuta chuo
Mm nimelala zangu bwenini, jamaa kutoka bweni jingine wakaidaka taarifa Kwa kutumia simu. Wadau hawakuamini, ikabidi waende staff (mle Kuna tv, inayotumiwa na walinzi wa shule)
Kesho yake, Head Master anakuja kutangaza..Kila mtu ana taarifa [emoji23][emoji23]
Kilichobaki ni kujazana dining hall kuangalia TBC tu
Shule ilikuwa kama km 100 kutoka chato, wadau siku ya mazishi walitimba
Swadakta
 
Nilikuwa Arusha ......Majengo nimeshalala ,ghafla napigiwa simu na wife ile kupokea namsikia analia huku akitamka maneno "baba amekufa!.....baba amekufa", nikahamaki.

Nilipomhoji vizuri akanielezea kuwa Magu kavuta, nikamwambia tulia bas kwani hata ukilia itakusaidia nini? Nikakata simu nikapunguza sauti ya redio......laaaahaulaaaaa! Nilisikia shangwe la kufa mtu nje mtaani.

Nikaongeza sauti ya redio nikalala
 
Nilikuwa Arusha ......Majengo nimeshalala ,ghafla napigiwa simu na wife ile kupokea namsikia analia huku akitamka maneno "baba amekufa!.....baba amekufa", nikahamaki.

Nilipomhoji vizuri akanielezea kuwa Magu kavuta, nikamwambia tulia bas kwani hata ukilia itakusaidia nini? Nikakata simu nikapunguza sauti ya redio......laaaahaulaaaaa! Nilisikia shangwe la kufa mtu nje mtaani.

Nikaongeza sauti ya redio nikalala
Ukatili ni mbaya, hilo ndilo somo kubwa alilotuachia mwendazake
 
Taarifa nilipata nikiwa shule......... Kidato cha nne... Nakumbuka ilikua mda wa prepo🪝📖📝........ Saa kumi na moja Asubuhi🕚🕚🕚. Mlinzi alituletea taarifa ya kifo cha raisi🥺😰😥🥶. Daaaaa nakumbuka Darasa lilitulia kama dakika2.= Hakuna aliye toa neno wala kukohoa🎚️ Baadaye ndo mijadala ikaanza kwa makundi Swali lilikua ni nani kahusika na kifo cha raisi kila mtu alizungumza lake analo jua yeye, Tulihoji kwaniniRaisi afariki bila shida yoyote na kama alikua mgonjwa kwanini raia hawakuwekwa wazi juu ya afya ya raisi, Nakumbuka kuna wanafunzi wa kike walilia kabisaa. Nisiwe muongo shule nzima ilikua na simanzi. Hadi kunapambazuka wanafunzi walikua washajadili mambo mengi Nani atachukua nafasi yake na akichukua
Atakuwa mwamba kama magu😗😗😗😗😗😗
In short me mwenyewe niliumia sana........
Kumpoteza WEMBEJEMBE.
 
Mi nilikuwa nimetoka safari ..nimefika Babati ..hoiii
Nikala msosi kama SAA 3 usiku ..tupo watatu ...simu haina chaji ...sina hamu ya kunywa ..

Nikajiandaa kulala ...huku wenzangu wapo jirani kuna mziki kiasi wapo wanapiga bia mbili tatu ...
Baadae kama SAA tano hivi .. Nasikia kelele ....
Wooooi .....weeeeeh .....yalaaaah. ...
Mara yereuwiiiiiii ....

Nikasema hii mipira ya usiku na kelele hizi.... Nikagongewa room ...
Wee ..funguaaa ...nauliza nini ? Tumevamiwa na majambazi ?

Nasikia Jiwe kakata moto ....nikauliza toka wiki iliyopita tunasikia tetesi ...lakini hatuna uhakika ...
Wakasema washa simu ....kucheki nakutana na Breaking news kuu ...

Tulikula pombe mpaka SAA 10 ...na kesho yake tukaendeleza ....
Ila tuishi kwa upendo na sio kuumizana bila ushahidi ..
Jiwe Mungu amsamehe makosa yake
 
Hiyo siku nilikuwa nimelewa chakari nikafika home na bodaboda sikuingia ndani nikasema nipate upepo kidogo nje kwenye maua ila nikazima.

Nakuja kupata fahamu naona wapangaji wanalia, nikajua wananililia mimi labda.
Nikasimama kwa mbwembwe kuonesha niko fiti lakini nikaona hawana mpango na mimi.
 
Back
Top Bottom