Tarehe 18 Mei 1985: Shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama Directorate K

Acha ujinga wewe ni mwizi, swali ni kwanini umeileta sasa iv baada ya yeye kua ameileta? Means ulikua hauijui, umeiona hapa ndio ukaenda kuiiba na wewe, wewe ni mwizi na hata story zako hakuna unalolijua sana sana unawatafsiria tu watu kesi za mahakamani ambazo ni reported tayari hauna unyama wowote, na hapa jukwaani umeiba story nyingi sana na unajifanya kama zako. Stupid cow
 
Hongera mkuu, nna swali kwako una story zingine za kijasusi zenye kufikirisha ukiacha hii ya Oleg ?
 
Ukweli n kwamba umeona jamaa anatoa hii story ukaamua kwenda kuitafuta ukaipa kichwa kingine ili watu watoe 2.5k per monthly,na naimani hakuna mwenye hati miliki ya hii story kwan hata wewe mwenyewe umeikopi mahali,
Kwa hio jamaa anafanya biashara kupitia uanzilishi wa simulizi za watu ? Yaan kuna baadhi ya wabongo ni lala kweli unawezaje kufanya hivyo ndio maana yoga alipoona watu wanacopy story yake ya Dark Days aliacha mara moja kusimulia wabongo nyoso sana
 
Aione cariha kwenda kwa buyobe
 
Mwanaume gani anajisikia vile, bora tuu asepe dada wa watu, alafu huko nyuma faili lake lilivuja hapa hapa JF 2010 halikuwa zuri.
Na ana file chafu kweli yani Mungu amsaidie huyo mrembo
 
Hahaaaaaa [emoji1787] Koba mzaramu wa kisemvule kaingilia dili la baba maria.

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
24


Huyu Arkadi guk baada ya kusoma barua ile ya Siri aliona kama huu ni mtego ulioandaliwa na M15 Kama mpango wa kumkamatisha akijihusisha na ujasusi ndani ya uingereza kwa kushirikiana na afisa wa M15 na hatimaye kufukuzwa . Kwa mfano hiyo barua ya Siri ilimtaka kama atakuwa tayari kushirikiana na huyo aliyejiita Koba Atoe feedback .Bwana guk mpaka tarehe 25 April hakuwa ameonyesha Nia yoyote hivyo akaamua kuupuzia huo mwaliko. Guk pia alihisi nyumba yake itakuwa kwenye surveillance na makachero wa M15, lakini inakuwaje Tena kachero wa idara hiyo aje aache ujumbe kwenye sanduku la posta la makazi yake. Alihisi Kuna mchezo. Lakini huyu aliyejiita Koba baada ya kuona kimya kwa zaidi ya miezi miwili akaamua kutuma Tena ujumbe kwa kuuweka katika sanduku la posta kwenye makazi ya guk usiku wa tarehe 12 June . Baada ya guk kuupata ujumbe huu tena, ulimshtua kidogo kutokana na unyeti wake. Hii ilikuwa ni document ya kurasa mbili ikiwa Ina orodha nzima ya majina ya maafisa wa Soviet walioko hapo ubalozi wa London ambao walikuwa suspected na M15 Kama majasusi wa KGB. Na hayo majina ya hao suspect walikuwa kwenye category tofauti ,kama ,fully , identified,less or more identified na under suspicion. Pia maelezo yaliyoambatana na barua hiyo yalimtaka bwana Guk atoe signal kwa Siri kama atakuwa tayari kukutana na jasusi huyo wa M15.
Jambo hili alimshirikisha bwana Leonid nikitenko afisa mwenzake mkuu wa kitengo Cha counter-intelligence kutokana na unyeti wa taarifa aliyoipokea. Wakashauriana walisogeze kwa wakubwa wao makao makuu huko Moscow. Order ikatoka kwamba waachane na mpango kutaka kukutana na huyo anayejiita Koba. Lakini haikuwa hivyo. Walipuuzia
Hili swala bwana Oleg alianza kuhisi Kuna something unusual kinaendelea Chini kwa chini hapo ubalozini. Hii ni baada ya kuona Guk na Nikitenko wakiwa kwenye mazungumzo private mara nyingi huku wakituma ujumbe wa telegram huko Moscow. Vilevile hawa ma bwana walikuwa wanapotea masaa kadhaa muda wa lunch.
Asubuhi ya tarehe 17 June Oleg aliitwa ofisini kwa bwana Guk na kufunga mlango. Guk alimuuliza swali la kwanza tu Oleg baada ya kufika . Nanukuu " Would you like to see something exceptional?" Baada ya hapo Guk alimtolea photocopy ya kurasa mbili na kuweka mezani zilizotoka kwenye original copy kutoka kwa agent anayejiita Koba. Oleg hakuamini alipokutana na jina lake kwenye kurasa zile kama naye ni suspected KGB spy na shirika la M15. Jina lake lilikuwa kwenye category ya less or more identified.
Lakini baadaye alikuja kung'amua kwamba ingawaje alikuwa kwenye list hii, waliohusika kuiandaa hawakujua Kama yeye ni double agent anayeifanyia kazi uingereza. Pia naye guk mwenyewe hakufahamu kwamba Oleg tayari anatumika na M16 kwa Siri.
Baadaye Oleg alisaidiana na deputy report officer kuitafsiri taarifa hiyo copy kwa lugha ya ki Russia .
Baada ya report hii ,Oleg alizidi kujiuliza maswali yenye mafumbo ndani yake. Imekuwaje M15 hawakumtaarifu Oleg hapo kabla! Kwamba anafuatiliwa, na imekuwaje jina lake lipo kwenye list hiyo kama suspected KGB spy ilihali yeye anawafanyia kazi? Hili swala lilimtatiza Sana Oleg .
Hatimaye akampigia simu ya private mwanamama Oliver price kutaka kujua nini kinaendelea yeye hajui. Wakapanga kukutana kwenye safe house haraka iwezekanavyo.
Wakiwa na James spooner na Oliver price Oleg aliwauliza imekuwaje jina lake lipo kwenye list ile aliyoipokea guk , wenyewe wakamtuliza wakamwambia hakuna chochote kinaendelea ndani ya kitengo dhidi yake , hususan la kutaka kufichua identity yake kwa namna yoyote ile.Lakini kutokana na maelezo ya ujumbe ule alioupokea guk kwamba Kuna spy ndani ya kitengo ndani Ya M15 anayejitolea kuwapa info Soviet lilikuwa ni pigo kwao.
Kutokana na sintofahamu hii ,kuliwapa na kuwaacha maafisa wa ngazi za juu wa M15 @ M16 na mtanziko mkuu . Inasemekana kwamba endapo haya mashirika wangeanza kumsaka mchawi na traitor aliyejitolea kuwapa taarifa nyeti za kitengo maafisa wa KGB,ni kwamba msaliti huyo akijua anawindwa ,naye angemchomesha Oleg kwamba naye ni pandikizi la M16 kwenye ubalozi wa Soviet anayetoa info za urusi Kwa uingereza. Lakini hawakujali wakataka kuanzisha msako kimya kimya. Waliona pasipo kuchukua tahadhari za haraka, automatic Oleg angekuwa kwenye hatari ya kugundulika. Kwa kifupi ni kwamba kwenye maafisa zaidi ya 1000 wa M16 na M15 , kulikuwa na asilimia 100 kuwepo kwa huyo anayejiita Koba.[emoji3578][emoji3578][emoji3578].
M16 waliamua kujipanga kumu eliminate huyo Koba miongoni mwao kabla ya kufanya damage zaidi.
Maafisa wa ngazi za juu walianza kuzichanga karata zao za kutaka kumjua Koba ni nani. M16 waliamini kwamba huyu Koba hakuwa na access ya information za kutosha kuhusiana na NOCTON. Maana yake huyo msaliti hakuwa miongoni mwa hao maafisa wachache waliopaswa kujua file la NOCTON kama ni double agent. Maana huyu mtu lazima angezifikisha kwa guk na guk angeripoti kwa wakuu wa kitengo huko Moscow na mwisho Oleg angeingia matatizoni rasmi.
Hivyo maafisa wachache waliojua kuhusu NOCTON wakaanza kumwinda msaliti ndani ya vitengo vyote viwili yaani M16 na M15 .
Huu mpango wa kumsaka mchawi au msaliti ulikuwa chini ya John deverell mkuu wa kitengo Cha kijasusi Cha counter-intelligence ndani ya M15. Hii operesheni waliipa jina la ELMEN. kuchimba Siri kwenye taasisi ya Siri ya kumpata mchawi miongoni mwao anayetoa Siri.
Inasemekana kwamba nanukuu " For an intelligence service, there's no process more painful and debilitating than internal hunt for an unidentified traitor...." Hii Ina maana kwamba kumsaka msaliti kwenye taasisi za kijasusi haikuwa kazi nyepesi kutokana na wakati mwingine kumhisi mtu asiye sahihi.
Kikosi kazi wakaingia kazini na kuanza kumtambua msaliti ni nani , .walianza kwa kupitia mafaili ya maafisa wote waliofukuzwa hapo uingereza waliosadikiwa kuwa ni KGB . Pia wakaanza kuwafuatilia wale watu wote waliokuwa wanamjua na kukutana na Oleg personally.
Uchunguzi wa kumsaka msaliti ulishika Kasi pale Oleg na familia yake walipoenda Moscow kwa mapumziko . Risk ikiwa kwa huyu aliyejiita Koba alikuwa ana exist bado na endapo angewapa informations urusi kuhusiana na Oleg kama KGB agent anayeifanyia kazi uingereza , kabla ya Oleg kurudi automatic asingeruhusiwa kurudi uingereza na angekamatwa na kushtakiwa. Maafisa wa M16 Waliokuwepo Moscow walikuwa alerted na kuwa standby endapo Oleg angeshtukiwa akiwa huko.
Mwisho wa siku kikosi kazi Cha kumsaka msaliti kilianguka kwa jina la bwana mmoja afisa M15 aliyeitwa Michael John bettaney.
Huyu bwana alikuwa ni afisa mpweke na mnyonge muda wote akionekana Hana furaha asiye jiamini.Kwa kifupi huyu bwana alikuwa ni pro-soviet (nikisema pro -soviet au pro-russian naeleweka) kwa Siri pasipo kutumbuliwa na staff wenzake . Alikuwa anafanya kazi kwenye idara ya counter-intelligence ndani ya M15. Huyu bwana alifanyiwa upelelezi mzito na mwishowe ikaja bainika alikuwa anawasiliana na Guk kwa Siri na alikuwa anatuma taarifa kupitia sanduku la posta kwenye makazi ya guk.

Baadaye Oleg aliporudi kutoka likizo alihitajika kukutana na Oliver price pamoja na spooner kwenye safe house huko Bayswater Ili kupata update za kumsaka mchawi wake. Pia kazini kwake Oleg alianza kufanya enquiries kutaka kujua kama Koba aliwapa taarifa zingine potential kumhusu yeye kipindi akiwa likizo lakini hakuona lolote jipya. Ilimpa ahueni lakini Sasa rasmi alijua muda wowote atahisiwa tu Kama msaliti.

Huyu bwana bettaney walianza kimfuatilia kila nyendo zake na sehemu zote alizokwenda na wakaanza kugundua kumbe huyu bwana alikuwa anawapa informations maafisa wa KGB aliopanga kukutana nao huko Vienna Austria. Pia walipata picha zake za Siri akiwa na maafisa kadhaa wanaosadikika ni Agent wa KGB. Hatimaye tarehe 15 September bettaney alihitajika kufika mbele ya Baraza la wakubwa wake kazini . Hakutegemea kukutana na taarifa kumhusu yeye ndiye Koba . Baada ya hapo kwa siku kadhaa Bwana deverell na jopo lake walianza kumfanyia interrogation bettaney na hatimaye Alikiri shtuma dhidi yake . Baada ya hili swala kujulikana na Margaret thatcher ,alipongeza vitengo vyote viwili kutokana na kumpata MSALITI huyo.
Kutokana na uwezekano wa kuwepo msaliti mwingine ndani ya vitengo hivyo. M15 waliamua kufanya divertion na kutunga stori kwamba , mahusiano baina ya bettaney na maafisa wa KGB yalivujishwa na afisa aliyeko ubalozi wa Russia . Hizi shutuma zote Bwana Arkadi guk alizikana waziwazi na kusema ni propaganda zilizotungwa kutaka kudhoofisha mahusiano mema kati uingereza na Urusi.[emoji3578][emoji3578]. Lengo la hii story ni lilikuwa kumweka mbali Oleg kuwa suspect .
Bwana bettaney alitiwa ndani wakati huo na mamlaka za uingereza akikabiliwa na mashtaka kumi kwenye kukiuka Official secrets Act .
Lakini msaliti ni msaliti tu. Bado Oleg hakuwa salama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…