Tarehe 18 Mei 1985: Shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama Directorate K

Tarehe 18 Mei 1985: Shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama Directorate K

Kwa shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama directorate K. Hii idara ilikuwa na kazi maalumu ya kufanya bugging , kile kitendo Cha kupandikiza vinasa sauti na video camera kwa Siri kwenye ofisi za walengwa maalumu waliokusudiwa , kusikiliza mawasiliano Yao ya simu au pia wakati mwingine kwenye makazi Yao binafsi.

Ilichukua nusu dakika kufungu vitasa viwili vya mlango wa mbele wa chumba namba 220 kwenye ghorofa ya nane katika mtaa wa Leninsky prospekt . Hili lilikuwa ni jumba la ghorofa lililokuwa linakaliwa na maofisa wa KGB pamoja na familia zao.

Kwa Siri sana wanaume waawili waliokuwa wamevalia overall pamoja na gloves kwa haraka haraka wangedhaniwa kuwa ni mafundi tu wa kawaida kwa ajili ya kufanya matengenezo madogo madogo katika jumba Hilo , lakini uhalisia haukuwa hivyo. Baada ya kufungua vitasa vya chumba hicho kwa ustadi na kuingia ndani wakaaanza kufanya kilichowaleta.wanaume hao wawili wakaaanza kuweka camera pamoja na vinasa sauti kwa Siri kwenye sehemu sehemu mbali mbali chumbani maeneo ambayo sio rahisi kushtukiwa. Vinasa sauti viliwekwa ukutani kwenye maiki za simu ya mezani ,pamoja na kwenye Kona za kitanda ,jikoni ,maliwatoni n.k.

Pia kamera ndogo za Siri ziliwekwa kwenye taa za kila Kona ya chumba hicho ,baada ya hapo wakavaa mask usoni na kuanza kunyunyiza vumbi lenye mionzi kwenye nguo na viatu vilivyokuwa kabatini katika Hali ambayo isingeweza kushtukiwa na mlengwa wao. Hili vumbi lingewasaidia ku track movements za huyo mlengwa wao popote aendapo kwa kutumia kifaa kilichojulikana kama Geiger counte. Baada ya kumaliza kilichowaleta wakaurudishia mlango na kuufunga kama walivyoukuta na wakatokomea.

Masaa machache baadaye ,afisa wa ngazi za juu wa KGB alishuka kwenye uwanja wa ndege wa Moscow na shirika la ndege la Aeroflot akitokea London. Kanali Oleg antonyevich Gordievsky alikuwa katika kilele Cha mafaniko ya kazi Yake katika idara ya KGB. Mpaka kufika kuwa afisa wa ngazi za juu kwenye shirika Hilo alipitia vyeo mbalimbali ,amefanya kazi kama balozi kwenye nchi za Scandinavia, uingereza pamoja na hapo Moscow.

Akiwa na miaka 46 aliteuliwa kuwa mwakilishi wa KGB kwenye ubalozi wa USSR hapo London. Kwa kuwa alikuwa jasusi mbobevu alipanda vyeo kwa haraka ndani ya idara kiasi kwamba akawa na uwezo wa kujua Siri nyingi za kijasusi (Disclassfied material) pamoja na mtandao wa kijasusi kwenye mataifa mbalimbali ikiwemo mataifa ya magharibi.

Mwenye muonekano wa mwili wa mazoezi,akiwa hana hofu Wala wasiwasi huku akitabasamu alikatiza katikati ya umati wa watu hapo uwanja wa ndege kwa ajili ya kutafuta teksi imuondoe hapo impeleke anapoishi.
Bwana Oleg afisa wa kijasusi mtiifu wa shirika la KGB aliyependwa na mabosi wake kama asset muhimu waliokuwa nayo kipindi hicho ,pia alikuwa ni JASUSI MTIIFU WA UINGEREZA. Kwa kifupi alikuwa ni double agent.

Akiwa afisa wa KGB tayari alikuwa ni mwajiriwa rasmi wa shirika la kijasusi la uingereza la MI6 kwa miaka takribani 12 .na alipewa jina jina la uficho (codename) la NOCTON.

Na baadaye ikaja semekana alikuwa ndiye JASUSI wa thamani sana enzi zile za vita baridi. Taarifa za Siri alizokuwa anazivujisha kutoka KGB na mipango ya Siri ya USSR zilibadilisha kabisa mkondo wa vita baridi kwa wakati ule. Bwana Oleg aliweza kutoboa Siri ikiwemo mikakati ya nyuklia za USSR..mtandao wa majasusi uliokuwa kwenye nchi za magharibi,pamoja na sera za nje za urusi kwa wakati huo kwa wakubwa wa MI6.

Taarifa alizokuwa anazivujisha bwana Oleg ziliwafanya MI6 na CIA ku share kwa pamoja baadhi ya taarifa, lakini ajabu ni kwamba DG na top officials wa MI6 hawakutaka kutoa identity ya Oleg kwa Margaret thatcher Wala Ronald Reagan waliemwajiri ndani ya Kremlin kwa maaana ya USSR kwa kuwapa sensitive Disclassfied informations. Na kulikuwa na sababu maalumu ya kufanya hivyo.
Pia mkewe bwana oleg hakuwahi kujua mumewe ni spy wa uingereza.

Lakini imekuwaje amekuja ghafla Moscow kwa kuitwa na wakubwa zake? . yaani ni kwa mfano balozi polepole kateuliwa balozi Tz Cuba, lakini ghafla hajamaliza hata miezi mitatu anaitwa nyumbani ghafla ,lazima hata kama ni wewe utajiuliza tu.

Lakini wanasema JASUSI ni jasusi tu . bwana Oleg aliweza kunusa hatari iliyokuwa mbele Yake ,akiwa anakatiza katikati ya watu hapo uwanja wa ndege baada ya kutua ndani ya nafsi yake alihisi upweke uliochanganyika na mashaka . Baada ya kukaguliwa nyaraka zake na hati ya kusafiria na wale maafisa wa passport uwanjani hapo alikabidhiwa akaagwa akaondoka.

Kikawaida kwa wakati huo afisa yoyote hususani mwakilishi akitokea nje ya nchi lazima kunakuwa na courtesy ya maafisa wenzake kuja kumpokea mwenzao airport lakini haikuwa hivyo. Akiwa anaangaza huku na kule asione dalili yoyote ya mapokezi alinotice jambo lisilo la kawaida, kulikuwa na wanaume na wanawake wamesimama hapa na pale uwanjani hapo pasipo jambo la muhimu waliokuwa walikilifanya zaidi ya kushangaa huku na huko.

Lakini bwana huyu akiwa ndani ya teksi alijiambia ikiwa KGB wanajua ukweli kumhusu yeye muda huo angekuwa tayari amewekwa chini ya ulinzi muda huo punde alipokanyaga ardhi ya Russia,aburuzwe Hadi kwenye cell za KGB ahojiwe,ateswe mwisho wa siku auliwe kwa kupigwa risasi ya kichwani .

Mpaka anaingia kwenye teksi Hadi kufika yalipo makazi yake mtaa wa Leninsky prospekt hakuwa anafuatiliwa kwa namna yoyote ile.alikwea lift Hadi ghorofa ya nane kwenye jumba Hilo kitasa Cha kwanza Cha mlango wake kilifunguka na Cha pili vilevile lakini kitasa Cha tatu Cha mlango kilikuwa locked bwana Oleg hakuwahi tumia kitasa Cha tatu kwa kuwa hakuwa na funguo zake, lakini ajabu ni kwamba alikuta kitasa kimefungwa na hapo hapo akahisi Kuna watu waliingia na kutoka wakajisahau wakafunga Hadi kitasa Cha tatu. Alikuwa sahihi . Alikuwa anatiliwa wasiwasi. The spy was being spied upon by his fellow spies.
Ujasusi
 
23.

Taarifa za Siri alizokuwa anatoa bwana NOCTON kwa M16 ,na kuwamegea CIA zilianza kuwatamkia lakini kamwe M16 walificha identity ya source hawakutaka CIA wajue. Ingawaje marekani walikuwa na muscles in terms of money na resources lakini hawakuweza kupata information ambazo ziko valuables kama za Oleg .


Lakini humuhumu CIA bwana Ames taratibu alianza kuinuka tena. Baada ya kurudi kutoka mexico kikazi akiambatana na mchepuko wake Rosario dupuy, waliamua kuanzisha makazi mapya huko falls church , Virginia katikati ya vitongoji vya Washington 1983. Kutokana na rekodi ya kazini kuwa mbovu , hususan umalaya na pombe alipandishwa cheo akawa mkuu wa idara ya counter-intelligence ndani ya CIA. Baadaye Rosa alikubali kuolewa naye baada ya kuona mzee baba kapanda cheo. Hatimaye akapata credit card mpya akatumia kununulia fanicha za $5000 .. na kulipa bili ya simu ya mkewe huyo kwa mwezi kama $400. Kwa mshahara wa $45000 kwa mwaka na hayo matumizi ni kwamba usingemtosha hata kidogo. Kwa kifupi huyu Ames alikuwa na uhitaji mkubwa wa fedha za matanuzi na mkewe huyu mpya.
Ni kwamba kipindi hiki boss mpya wa CIA chini ya utawala wa Ronald Reagan alikuwa bill Casey.Huyu Casey alikuwa amepandikiza baadhi ya majasusi ndani ya Russia aliokuwa ana operate nao kupata taarifa za Soviet. Ames alikuwa anajua identity ya baadhi ya hao maagent waliopandikizwa ndani ya Russia. Kwa mfano Ames alikuwa anajua taarifa kwamba Kuna watu walioko huko Russia wanafuatilia treni zilizokuwa zinasafirisha nuclear warheads kupitia reli ya trans-siberia huko mashariki mwa Urusi. Na kubwa zaidi Ames alikuwa na info kwamba shirika la M16 wanajasusi wao ndani ya KGB anayewapa informations za urusi lakini uingereza wanaficha identity yake ................... .......... Zaidi bwana Ames alikuwa broke na alihitaji pesa ..... [emoji848].

Ngoja turudi huku uingereza kidogo

Mwishowe M16 waliona ni busara kumshirikisha Margaret thatcher kwenye case ya file la NOCTON. Ikawa swala la NOCTON linajulikana na wanasiasa watatu pekee uingereza kwa wakati huo yaani P.M . Thatcher, mshauri wake na private secretary wake pekee .
Tarehe 23 December 1982 M16 Walimpa Margaret thatcher file la NOCTON ,hii ni kutokana na thamani ya taarifa nyeti za Siri alizokuwa anatoa bwana Oleg. Hii ni baada ya miezi sita tokea Oleg atue hapo uingereza kikazi kama afisa wa ubalozi wa Soviet hapo London. Ni kwamba Margret thatcher aliambiwa na maafisa wa ngazi za juu wa M16 kuwa Wana agent wao special ndani ya KGB kwenye ubalozi wa Soviet hapo London. Lakini hakuambiwa jina lake ni nani kuepusha leakage . Maana wanasiasa ni ropo ropo muda wowote anaweza ropoka.
Upande wa pili ingawaje Oleg na ushirikiano wake na M16 ulikuwa unanoga ,huku ubalozini kwake kulikuwa kwa moto.. waliosema huwezi kuwatumikia mabwana wawili hawakukosea.
Guk balozi na msaidizi wake walianza kumtilia wasiwasi Oleg na ikaanza vitimbi.
Kwa mfano mara ya kwanza baada ya Oleg kutua hapo ubalozini Hawakumpenda . Hii ni kwa sababu Oleg alikuwa smart muda wote hakuwa mnywa vodka kama wao halafu alikuwa anaonyesha umagharibi umagharibi Fulani hivi ambao wenzake hawakumwelewa . Kwa mfano hafla zilizofanyika hapo ubalozini ,yeye Oleg alikuwa na ule u gentle man wakuwamiminia watu vinywaji ,na hata chakula chake alipendelea kula sandwiches na matunda na kingine vijisikukuu vya mashujaa wa huko Russia hakuvizingatia kivile kama wenzake ,na pombe aliyokuwa anaitumia ni wine tu. Sasa bwana Oleg akawa anasemwa kiaina na wenzake kwamba huyu mwenzetu vipi haeleweki.
Oleg alijua yaliyokuwa yanaendelea nyuma ya mgongo wake. Kwa kifupi Oleg umaarufu wake ulikuwa unaporomoka kwa Kasi sana. Hii ni kutokana na ubize wake kuwa feed M16 taarifa za kiintelijensia . Kumbuka kila mfanyakazi au afisa wa ubalozi lazima kunakuwa na annual report kumhusu yeye ambayo Huwa inatumwa huko Moscow. Swala likawa linamtatanisha Oleg Je what if atarudishwa nyumbani kutokana na poor performance kazini?.
M16 wakaona ni busara kuongeza reputation ya Oleg kazini kwa kucheza mchezo mmoja . Maana ikitokea akarudishwa Moscow haraka au kubadilishwa kituo Cha kazi nje ya. Uingereza itawagharimu wao.
Ni kwamba kutokana na info za kijasusi waliopenyezewa na oleg wakaona kikwazo kikubwa ni Igor titov boss wa Oleg ambaye ndio alikuwa balozi wa Russia . M16 waliamua kumuondoa . Magazeti ya uingereza yakaandika na kumtuhumu titov kwamba anajihusisha na maswala ya ujasusi nchini humo. Mamlaka ya serikali ikachukua hatua na ikamfukuza pamoja na maafisa kadhaa wa Russia walioko nchini humo. Na baadaye maafisa wengi kwenye nchi mbalimbali za magharibi zikatimua baadhi ya maafisa wa Soviet. Hii ikatengeneza njia kwa Oleg kuendelea kupanda rank Kwa maana ilitarajiwa angechukua nafasi ya titov. Ila nafasi ya titov akapewa arkadi guk na yeye akawa deputy. Mpaka katikati ya mwaka 1983 Oleg umaarufu wake uliongezeka maradufu ndani ya ubalozi huo. Na hii haikuzua wasiwasi wowote. Hatimaye akawa na access ya taarifa nyeti za kiintelijensia . Oleg alikuwa na kila sababu ya kuwa na ujasiri . Kwa maana Sasa hata information anazotoa zinatua Moja kwa Moja kwa Margaret thatcher. Lakini biblia ilishasema adhaniaye amesimama na aangalie asianguke[emoji3578][emoji3578][emoji3578]

Mwezi April 1983 ,bwana Arkadi guk balozi wa Soviet wakati anarudi kwenye makazi yake mtaa wa 42 Holland Park, alikuta barua imeachwa kwenye sanduku la posta la nyumba hiyo . Hii barua ilikuwa ni ya top secret mwandishi akitaka kushirikiana na urusi na kuwapa info za sababu za titov kufukuzwa uingereza na pia contact number za yeye kupatikana na mwisho wa barua ilisainiwa Koba.

Nini nani huyu anayejiita Koba?
 
IMG_20230501_213820_967.jpg

General Arkadi guk kulia akiambatana na mkewe pamoja na bodyguard kwenye mkahawa mmoja kwenda kupata Moja moto Moja baridi[emoji28].

IMG_20230501_213835_192.jpg

Makazi ya balozi wa Russia hapo uingereza yaliyoko mtaa 42 Holland Park ambayo bwana guk alikuta barua ya Siri imeachwa hapo na afisa aliyesadikiwa kuwa ni Wa M15
 
Muda mwingine unaweza ukawa wewe ni rais ,na taasisi za kiusalama hususan za usalama wa taifa zikawa zinawajibika kukupa info zote kwa kadiri sheria inavyotaka. Ila wasikupe taarifa zote nyeti za nchi kwa sababu ya maslahi mapana ya nchi. Point ni kwamba mostly wanasiasa hawaaminiki . Muda wowote anaropoka[emoji848]
 
Silaha kubwa ya jasusi/kachero ni kuwa invisible, wana mafunzo ya combat n.k, japo wengi hudhani jasusi ni kama James Bond kuvaa suti za bei kali na kila aina ya gadgets za ajabu n.k.

Kuna majasusi hata Mandonga mtu kazi anawatwanga lakini kwenye ulimwengu wa kijasusi ni watu hatari na nusu.

Japo kuna wings ndani ya idara za kijasusi zenye agents kazi zao ni mauaji na utekaji hawa wana mafunzo ya combat ya hali ya juu. Jasusi wanao ogopwa zaidi ni hao ma spy, ukiwaona huwezi dhani tukiachana filamu kama Kingsman na James Bond.
Kuna hili kachero la cia ambalo limeshikiliwa na Moscow kwa kuji disguise Kama mwandishi wa wall Street journal.... sijui hatima yake itakuwaje .

Japo kwao wanakataa kwamba sio kitengo lkn kwa jicho la kawaida mwamba anaonekana ni mwewe kabisa na sio mwandishi.
 
Muda mwingine unaweza ukawa wewe ni rais ,na taasisi za kiusalama hususan za usalama wa taifa zikawa zinawajibika kukupa info zote kwa kadiri sheria inavyotaka. Ila wasikupe taarifa zote nyeti za nchi kwa sababu ya maslahi mapana ya nchi. Point ni kwamba mostly wanasiasa hawaaminiki . Muda wowote anaropoka[emoji848]
Uko sahihi mno
 
Back
Top Bottom