Tarehe 18 Mei 1985: Shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama Directorate K

Hili swala la kuwa kipindi cha miaka ya uhuru ya nchi yetu tulikuwa sawa kimaendeleo na nchi ya China ni kweli? 1961 tumepata uhuru ni kweli miaka hiyo tulikuwa sawa kimaendeleo na china? Au propaganda tu maana china ndio waliopewa tenda ya kujenga reli ya tazara 1968 miaka 7 baada ya uhuru. Hao watu wa china ni kweli tulikuwa nao sawa kimaendeleo kipindi hicho ?

Kama tulikuwa nao sawa iweje wao wawe na uwezo wakuwa na wakandarasi na vifaa vya ujenzi WA mradi mkubwa kiasi hicho kwa kipindi hicho? Au tunaposema tulikuwa sawa tunalinganisha nn?
 
Apo tumepigwa tu
Kama tulivyopigwa kuwa binadamu alianza kuwa sokwe
 

CIA walichoka ama walikerwa kwa kile walicho kiita kupewa infor na washirika wao Mi6, "on need to know basis". Wao CIA walitaka direct access na source ambazo zilikuwa za hakika na valuable.

Kwa kutaka kujua hiyo source ya Mi6, ndio walimteua boss wa CIA anaye deal na Intel ya russia Mr. Aldrich Hazen "Rick" Ames. Aldrich kwa kile alichoogopa itafanya nayeye astukiwe na cia as a kgb mole, akataja majina mengi kwa KGB aliodhani wanatoa siri kwa Mi6, na jina la Giby likiwepo.

Kwahyo wakt Goby anaitwa ghafla kwenda russia kwa madai ya promotion, wao KGB hawakua na hakika kabisa kwamba Goby ni mole wa Mi6. Ndio maana walimtocha, hawakupata majibu, kisha wakamweka house arrest kwa uchunguzi mwingine. Ila wangekuwa na hakika kabisa, wangemuua.
 
Wanasiasa wapo wa kazi maalum lakini corruption ikishagusa hata maeneo nyeti uzalendo unaondoka na mnaishi kwa woga wa kuwindana. Inabidi tupate kichaa mwenye vision tuibadili nchi yetu isichezewe tena.
 
Wanasiasa wapo wa kazi maalum lakini corruption ikishagusa hata maeneo nyeti uzalendo unaondoka na mnaishi kwa woga wa kuwindana. Inabidi tupate kichaa mwenye vision tuibadili nchi yetu isichezewe tena.

Mwanasiasa akishakuwa corrupt hasa yule wa juu, atakacho kifanya ni kuwapa maslah bora na marupurupu organs zote nyeti kama takrima. Pili atateua viongozi wa huko nyeti watu wake wakaribu na watiifu Kwake. Kwahiyo ni rahisi kuwa na nyeti corrupt as a product ya wanasiasa corrupt.

Kwa africa na hasa Tanzania, hii taasisi ikijitegemea yenyewe kutoka kwny kuchakata taarfa hadi execution bila mwanasiasa hapo katikati, nchi ingenyooka.
 
Unazungumzia maendeleo kwenye angle Gani labda kwani kujenga reli tendor si yoyote anapata Kwa taarifa yako miaka ya uhuru na 1970 years tulikuwa tunalingana na nchi nyingi kimaendeleo na wao wameshapiga hatua kuwa developmental state na sisi bado tuko nyuma hata miaka ya 1970 na 1980 nchi hii ilikuwa na viwanda vingi tofauti na Sasa ikiwemo illiteracy level iliisha nchi ka malyasia, south Korea, so kuendelea ni maamuzi tu na sio swala la kupigwa au lah
 
cariha naona unafuatilia kwa karibu. Ila ukumbuke kuna mambo matatu hapa tuliyategemea kupatikana katika simulizi hii kuwa kwa vyovyote:-
1. Lazima ioneshe Marekani ni super power (walivyoomba M16 kujua informer lakini wakatiliwa ngumu ila mwishoni wakamjua na kumchoma
2. Lazima Uingereza nao si haba maana waliweza kumuokoa informer wao kuoka katika mdomo wa mamba mwenye njaa
3. Urusi imekuwa defeated.

Ila ni nzuri na ya kusisimua.
 
Brother hiyo wala siyo issue kabisaa! Mchakato wa kutunga sheria haufanyiki bungeni. Kwa katiba yetu sheria inayotakiwa kupelekwa bungeni inapaswa kupitia kwa wadau, wananchi nk, Bahati nzuri wabunge hawaandiki sheria wao wanapitisha tu Mambo ya msingi kwenye hiyo sheria inayokusudiwa. Wataalamu wetu ndiyo waandishi. Wabunge hata wakiwa darasa la saba, sheria hivi watashindwa kuamua kwamba mtu anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja afungwe Maisha au anyongwe!! Hii katiba tuliyonayo sasa ilitungwa kwa kiwango kikubwa na watu ambao hawakuwa na kiwango kikubwa cha elimu. Lkn yapo Mambo mengi sana waliyaweka ambayo ni mazuri. Sisi changamoto yetu siyo elimu, changamoto yetu ni kupangiwa Mambo na hao wakubwa...!! Na ndani ya serikali wale tunaowaamini ndiyo wanapa dikizwa kusimamia masilahi ya wakubwa.
 
Code:
3. Urusi imekuwa defeated.

AJABU NDIYE ALIYEFANYA UMAFIA WA KUMUWEKA DONALD TRUMP MADARAKANI!.
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
 
Wanasiasa wapo wa kazi maalum lakini corruption ikishagusa hata maeneo nyeti uzalendo unaondoka na mnaishi kwa woga wa kuwindana. Inabidi tupate kichaa mwenye vision tuibadili nchi yetu isichezewe tena.
La kutochezewa lilitaka kutokea TZ likaishia kati, subiri labda mika kama 50 hivi, sema na aliyetaka kubadili ni kama alitaka kuwa wa kudumu madarakani, watu wakashtuka
 
36

Rumours kuhusiana na kutoweka kwa bwana Jasusi zilianza kusambaa sana ndani ya corridor za makao makuu ya KGB kwenye jengo la lubyanka. Idara ya directorate K ambao walikuwa na jukumu la kumfuatilia Oleg kila mahali waliamini kwamba lazima atakuwa yupo Russia , either amelewa na kufa ,au labda kajiua na kujitupa mtoni. Msako ulianza kwenye maeneo ya mito na maziwa yaliopo jiji la Moscow. Maafisa wengine wakasema labda alitoroka kupitia Iran kwa kutumia passport feki. Nae bwana Budanov akasema atakuwa labda amejichimbia mahali kwenye safe house za uingereza. Mkewe , Leila alifuatwa huko kwa baba yake alikokuwa kwenye mapumziko kwenye fukwe za bahari ya Caspian Hadi kwenye gereza la lefortovo kwa mahojiano zaidi..... Swali alilokuwa akiulizwa mara kwa mara ni MUMEO YUKO WAPI. Lakini huyu mwanamama hakuweza kujibu zaidi aliwaambia kama nyie hamjui afisa wenu Yuko wapi ,basi Mimi sijui alipo huku akilia. Baadaye huyu mama alipokuja kuambiwa na hao wanaomhoji, kwamba mumewe alikuwa anafanya kazi na waingereza hakuamini hizo stori na alikataa katu.
Oleg alishawahi mwambia asiamini lolote atakaloambiwa kuhusiana na yeye [emoji28].
Kiufupi watu wengi waliokuwa na uhusiano wowote wa karibu na Oleg hapo Moscow walihojiwa intensively lakini bado haikujulikana haswa yupo wapi Hadi muda huo...,......

Siku ya jumatatu ,Oleg(Mr. Hanssen muda huo akiwa London) alijikuta yupo kwenye ukumbi wa south ormsby hall kwenye mji mdogo wa Lincolnshire akiwa ameandaliwa hafla fupi ya kumpongeza kama mgeni wa heshima. Hakutegemea kutokana na uchovu aliokuwa nao . Aliwauliza maafisa wa M16 kama anaweza kupiga simu kwa mkewe lakini hawakukubali kutokana na kwamba ingewapa alert KGB.ilikuwa ni mapema sana
Oleg alipelekwa kuhifadhiwa kwenye ngome Moja iliyoitwa fort Monckton kama safe house iliyopo kitongoji Cha Gosport . Na safehouse hii iliitwa Military Training Establishment. .iMTE. Pia ilitumika kama kambi ya mafunzo kwa majasusi wa M16. Hapo alipewa debriefings za hapa na pale na kupewa treatment za hadhi ya juu. Lakini hakusita kuuliza kuhusiana na familia yake . Eneo Hilo la fort Monckton lilikuwa linalindwa maradufu na mara ya kwanza haikuwa rahisi kumtambua huyu mgeni ni nani haswa kwa baadhi ya maafisa wengine wa M16. Lakini baadaye walikuja kumtambua ni nani huyu mgeni mpya waliyenaye.na alipewa jina la uficho la OVATION.
Kutoka SUNBEAM, NOCTON , PIMLICO Sasa ni OVATION. Kwa upande wa CIA wao walimtambua kama TICKLE [emoji28][emoji28].
Case ya Oleg ikawa imeingia rasmi kwenye phase nyingine. Kutokana na information alizowapa mashirika ya kijasusi ya nchi za west, zilisaidia sana kuepusha vita vya nuclear baina ya Soviet na west. Pia info hizi za Oleg zilisaidia kuwafichua Maafisa wa ngazi za juu wa kisiasa waliokuwa serikalini ambao walikuwa kwenye payroll za KGB wakiuza Siri.
M16 wakaanza kujiuliza maswali, Je wawaambie CIA na washirika wengine kuhusiana na hii operation ilivyofanyika na kufanikiwa? Au waitishe vyombo vya habari kwa ajili ya hii taarifa? Na Je baada ya mambo kutokea juu uhusiano wa uingereza na Russia utakuwaje? Uhusiano wa Thatcher na Mikhail Gorbachev utakuwaje? Na kingine M16 Walilopaswa kulifanyia kazi ni familia ya Oleg . Mkewe Leila na watoto wake . Haya maswali M16 Walikuwa wanajiuliza
Baadaye kupitia afisa mmoja wa KGB aliyeitwa vitaly virchenko aliyekuwa anatoa info kwa CIA ,aliwatonya kwamba Kuna jasusi wa KGB anayehusishwa kuifanyia kazi M16 yupo under house arrest akisubiri kesi yake itafikia wapi aliyeitwa Oleg . CIA kwakuwa walimjua kama tickle ,wakawapa info M16. Kupitia hii info M16 walituma maafisa wawili Hadi kwa bill Casey marekani kwenda kumpa A to Z ya Oleg Hadi kutoroshwa kwake. CIA walishangazwa na hizi taarifa zilipotuwa mezani kwao.
Bwana Casey aliamua kufunga safari Hadi fort Monckton kuonana na hii ASSET mpya ya M16 waliyokuwa nayo Ili kupata new infos za Russia kuhusiana na vita baridi na pia kutoa shukran zake binafsi kwa Oleg Kutokana na nondo zake alizokuwa anatoa kwa nchi za west na kuepusha uwezekano wa kutokea vita.... likapita
Miezi kadhaa baadaye Oleg alisafiri Hadi marekani chini ya ulinzi mkali ,Ili kufanya mkutano wa Siri na maafisa wa ngazi za juu wa Baraza kuu la usalama wa taifa la marekani . Maswali yote aliyoulizwa alijibu kwa ufasaha kuhusiana na Russia. Na pia alienda Hadi Langley makao makuu ya CIA kukutana na maafisa wa ngazi za juu wa kitengo kwa ajili ya kikao nao. Alipewa heshima zote alizopaswa kupewa na mambo mengine yakaendelea.....
Kipengele kikawa ni familia yake.
Kwakuwa M16 wanajua baadhi ya maafisa wote wa KGB wanofanya kazi under official diplomatic cover , waliamua kumtokea afisa mmoja wa KGB ambaye alikuwa ni mshauri kwenye maswala ya kisayansi kwenye ubalozi wa Soviet kwenye Jiji la Paris ufaransa. M16 Walimpa ujumbe wa Siri utumwe Hadi Moscow kuhusiana na kuiachilia familia ya Oleg. Mke na watoto wake. Ujumbe ulikuwa unawataka Soviet waiachilie familia la sivyo maafisa wote wa KGB London watimuliwe . Ilikuwa ni ultimatum kwa Russia na walikuwa na wiki mbili za kujibu. Huu ujumbe haukusema kama Oleg yupo uingereza au la .
Huku mkewe Oleg aliendelea kubananishwa kwenye geraza la lefortovo na maswali kuhusiana na alipo mumewe . Wanawe wakiwa shuleni walikuwa chini ya uangalizi wa KGB.Pia rafiki yake Oleg bwana lyubimov naye alitiwa ndani kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na alipo mwamba . Majibu ni Yale Yale . Hakuna aliyejua alipo. Kwa kifupi hili sakata liliwatia watu wengi lockup. Je wapi alipo Oleg?
Mke wa Oleg alipoona maswali yanazidi aliwatolea uvivu waliokuwa wanamhoji na kuwaambia . Nanukuu " Look. Let's be clear. I was a wife. My job was to clean,cook ,shop ,sleep with him, have children ,share the bed and be his friend. I was good at it. I'm grateful he didn't tell me anything. For six years ....I was a perfect wife. I did everything for him . You , the KGB, you have thousands of people with salaries whose job was to check up on people . They checked him and cleared him .. And you come to me and blame me ?. Don't you think that sounds stupid? You didn't do your job. It wasn't my job,it yours. You ruined My life".. Huyu mama alikuwa sahihi.

Ujumbe wa siri wa Ultimatum ulipowafikia KGB kuhusu kuiachilia hii familia Lakini wakatia ngumu wakisema huyo ni msaliti na familia yake lazima ibaki Russia.
Ujumbe huu uliporudi uingereza kwa M16 ,wakaamua kuujibu kibabe zaidi.
Ofisi ya wizara ya mambo ya nje wakaamua kutoa info kwa media kuhusiana na Oleg kutoroka Russia,ila info haikuwa na maelezo ya Zaidi kuhusiana na kutoroka huko. Magazeti ya uingereza kama kawaida Yao vichwa vya habari vikawa kama ifuatavyo.. " The biggest fish ever Netted",[emoji28][emoji28][emoji28] lingine likaandika " Friend Oleg, Master Spy" , lingine likasema " Russia's Ace of spy ;the Super-spy who went West". Lingine likaandika kwa mbwembwe "Our Man in KGB"[emoji38]. Na haikupita muda tokea taarifa kwa umma itoke , serikali ya uingereza ikatimua maafisa Zaidi ya ishirini wa Russia Waondoke ndani ya masaa 48.
Nao Russia wakaamua kufukuza maafisa wote wa uingereza waliokuwa wakifanya kazi Soviet ikiwemo akina Arthur gee na mwezake Ascot ambao walimtorosha Oleg.
Ndani ya KGB wakubwa walianza kutupiana Mpira wa lawama . Kila kitengo ndani ya KGB kilitupa lawama kwa mwenzake kutokana na aibu hii ya mwaka kuhusu Oleg aliyewatoroka . Maafisa wote wa KGB kwenye Jiji la Leningrad walilaumiwa pia kutokana na uzembe walioonyesha mpaka jamaa akawatoroka kizembe. Wengi wa maafisa walifukuzwa kazi au kusimamishwa . Na hili varangati lilimkuta Hadi Vladimir Putin akiwa afisa wa KGB kwenye mji wa Leningrad . Wengi wa maafisa wenzake walitimuliwa .
Kutokana na aibu hii KGB wakaamua kutunga uongo kwa ajili ya kuihabarisha umma wa raia kwamba Oleg alitekwa na kutoroshwa na sio kwamba alitoroka mwenyewe kama inavyodaiwa[emoji28][emoji28][emoji28].
Siku mbili baadaye rasmi sasa maafisa wa uingereza kwenye msafara wa magari nane waliondoka Russia chini ya conyoy ya KGB kwenye ulinzi mkali kupitia mpaka wa Vyborg Hadi nchini finland.

Hatimaye tarehe 14 November 1985 kwenye mahakama ya kijeshi ilimkuta Oleg na hatia alisomewa mashtaka ya uhaini na kuhukumiwa KIFO in absentia.
Mwaka 1986 Oleg alialikwa na Margaret thatcher kwenye makazi yake kwa ajili ya pongezi[emoji3578][emoji3578][emoji108]. Na mwaka huo huo Oleg alikutana na Ronald Reagan kwenye oval office marekani..
Huko Russia mke wa Oleg aliendelea kushikiliwa under house arrest kwa kisasi na KGB asije kutoroka kama mumewe.[emoji28][emoji3578]. Pia KGB walimwambia Leila endapo akitoa tamko la kuachana na Oleg au talaka Mali zake atarudishiwa zilizokuwa zimeshikiliwa .
Miaka sita ya mivutano kati ya Russia na uingereza kuhusiana na hii familia ya Oleg iliendelea. Uingereza ilitumia nchi washirika kuishinikiza Russia iachilie hiyo familia. Hata thatcher alipokutana na Gorbachev mwaka 1987 ,bado waliendelea kukaza.
Hatimaye ilipotimia 6 September 1991 Russia waliamua kuiachilia familia hii ya Oleg na kusafirishwa Hadi Heathrow London Kisha wakapelekwa na helcopter Hadi fort Monckton Oleg akiwa anawasubiri kwa hamu. Walifanyiwa homecoming ya kutosha . It was an emotional moment.
Miezi mitatu baadaye muungano wa umoja wa nchi za kisoviet ukavunjika RASMI.
Watoto wa Oleg waliendelea masomo shuleni na hawakutumia jina la Gordievsky kamwe .
Na mwaka 1993 Oleg na mkewe walivunja uhusiano wao wa ndoa RASMI. .......
 

Oleg akiwa na rais wa marekani Ronald Reagan walipokutana oval office 1987. Kwa ajili ya pongezi [emoji3578][emoji3578][emoji108][emoji3578].





Oleg akiipokea familia yake, baada ya Miaka sita ya kutengana.. hapa ni Leila na watoto wake wawili walishuka kwenye helicopter





Oleg akiwa na familia yake kwenye picha ya pamoja kama kumbukumbu souvenir photo [emoji108][emoji108][emoji108][emoji39]




Msafara wa magari nane ya maafisa wa ubalozi wa London waliotimuliwa Russia wakisindikizwa na convoy ya magari ya KGB baada ya sakata la Oleg.
Picha ya hii ilipigwa kwa siri na mmoja wa afisa wa M16 .
 

Attachments

  • IMG_20230508_181346_159.jpg
    59.6 KB · Views: 50

Mwamba akiwa anaishi nchini uingereza kwa jina la bandia kwenye kitongoji mojawapo nchini uingereza. Akilindwa Chini ya ulinzi mkali.


Mwaka 2007 Oleg Gordievsky alivishwa medani ya heshim ya juu ya CMG (Companion of the most distinguished Order of st Michael and St George) na malkia Elizabeth wa uingereza .Hii ni kutokana na kazi yake iliyotukuka kwa usalama wa uingereza na united kingdom [emoji3578][emoji3578][emoji108]
 
Kuna kipindi huyu jamaa alidai alipewa sumu na majasusi wa Urusi
👇
 
Halo hii Dunia Ina mambo mengi kweli ila ni kweli USA ilionyesha u supa power wake walimfatilia Oleg mpaka kumgundua, pia Uingereza walivoweza kumuokoa informer wao vizuri.
All In all hii story ni interesting na Ina mafunzo mengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…