Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Aaa Mkuu hivi wewe tukio la Oleg utafananisha na kuingilia huo uchaguzi wa US? Urusi pigo walilopata kwa Oleg ni kubwa sana mkuu yaani waliumizwa sana. Kwao ilikua ni pigo sana kwa taasisi yao hiyo maana miaka michache badae Soviet ilibomoka vipande vipande na rasmi vita baridi ikawa imeisha. Sasa ukisema kwamba nae Russia ameonesha umwamba kwa kuingilia uchaguzi eti kuwa ndio ametoa pigo kwa Us ahaaa no sidhani kama zinalingana kwa uzito mkuuCode:Hivyo Russia alijaribu tu kuingilia mifumo ya uchaguzi ili kumsaidia Trump
Kwanza hapo situkwamba arijaribu kuingilia mifumo,bali ni aliingilia na kufanikisha kumuweka Trump madarakani.
Lakini pia suala la Trump kuwa ni pandikizi au siyo pandikizi wa Urusi,bado ni CODE ambayo haijafunguliwa na haiwezi funguliwa hii leo mapema hivi.Uwenda vizazi vijavyo huko mbele wakafunguliwa CODE hizo na suala likiwa wazi.
Turudi kwenye ishu ya KGB tukilinganisha na mashirika mengine.Baadhi ya wadau wanaona kupitia Oleg kuwa KGB ni wachovu ukilinganisha na CIA na M16 kwa tukio hilo la kisaliti katika miaka hiyo 85 na huku wakiendelea kuamini hivyo mpaka leo.
Sasa swali linakuja kuwa,ni vipi KGB wachovu waweze kuingilia mifumo ya uchaguzi na wafanikiwe dhidi ya CIA wasio wadhaifu ukilinganisha na KGB?.[emoji16][emoji38][emoji28]
Mbona pameshapita kiongozi! au ulikua kwenye fungate?Kitasa ndo basi tena?
Okay patiently waitingBado hatujamalizana naye[emoji28]
Usaliti ni kitu kibaya sana hasa tukiaminiwa na Ina damage mbaya usaliti ndio uliofanya USSR kuvunjika loh.Inawezekana huu uzi ndio umekwisha, shukrani kubwa kwa mleta mada kwa jinsi alivyojitahidi kuleta episodes mfululizo hadi kuleta raha kufatilia.
My take kuhusu huu uzi, kwa njia moja ama nyingine mimi au wewe msomaji unaweza kuingia mazingira ya watu fulani, kampuni ficho za kijasusi kukutumia kwa fedha kuuza taarifa nyeti za nchi kutoka na wadhifa wako. Usidhubutu kutoa ushirikiano hata chembe, usaliti kwa ardhi uliyotwaliwa ni laana kwako na kizazi chako lakini ikitokea idara za usalama zikaja kushtuka utalipia gharama kubwa wewe na familia yako yote.
Ni vizuri kubakia na somo hili maana hii habari ya Oleg imempa ushujaa na pengine kuishi kama executive citizen wa UK na kuleta ushawishi wa kuwa double agent [emoji23] lakini pengine hatujafikiria kiwango cha damage aliyofanya kwa Taifa lake hadi leo. Oleg kusaidia kuepusha vita ya nyuklia inawezekana ni kachumbari tu ila hiyo vita iliepukwa na mambo mengi wakati ule.
Nimeona niangalie kwa jicho tofauti hasa somo nyuma hii stori.
Na kwa nini West wafurahie sana kuepushwa kwa vita wakati USSR aliitaka kwa hamu sana hiyo vita?.Inawezekana huu uzi ndio umekwisha, shukrani kubwa kwa mleta mada kwa jinsi alivyojitahidi kuleta episodes mfululizo hadi kuleta raha kufatilia.
My take kuhusu huu uzi, kwa njia moja ama nyingine mimi au wewe msomaji unaweza kuingia mazingira ya watu fulani, kampuni ficho za kijasusi kukutumia kwa fedha kuuza taarifa nyeti za nchi kutoka na wadhifa wako. Usidhubutu kutoa ushirikiano hata chembe, usaliti kwa ardhi uliyotwaliwa ni laana kwako na kizazi chako lakini ikitokea idara za usalama zikaja kushtuka utalipia gharama kubwa wewe na familia yako yote.
Ni vizuri kubakia na somo hili maana hii habari ya Oleg imempa ushujaa na pengine kuishi kama executive citizen wa UK na kuleta ushawishi wa kuwa double agent [emoji23] lakini pengine hatujafikiria kiwango cha damage aliyofanya kwa Taifa lake hadi leo. Oleg kusaidia kuepusha vita ya nyuklia inawezekana ni kachumbari tu ila hiyo vita iliepukwa na mambo mengi wakati ule.
Nimeona niangalie kwa jicho tofauti hasa somo nyuma hii stori.
Mkuu!Ishu ya 85s huko,imekuwa wazi leo 2020.Ishu ya 2015s hivi,haiwezi kuwekwa wazi leo kwa kina.Aaa Mkuu hivi wewe tukio la Oleg utafananisha na kuingilia huo uchaguzi wa US? Urusi pigo walilopata kwa Oleg ni kubwa sana mkuu yaani waliumizwa sana. Kwao ilikua ni pigo sana kwa taasisi yao hiyo maana miaka michache badae Soviet ilibomoka vipande vipande na rasmi vita baridi ikawa imeisha. Sasa ukisema kwamba nae Russia ameonesha umwamba kwa kuingilia uchaguzi eti kuwa ndio ametoa pigo kwa Us ahaaa no sidhani kama zinalingana kwa uzito mkuu
Yaani mkuu mimi nadhani udhaifu ama uhodari wa hizo agency ni kutokana na faida na hasara wanazosababisha kwa nchi zao kwa ujumla.... kwamba Mi6 hasara waliopatia Kgb ni kubwa mno lknFSB hasara walioipatia CIA/US ni ndogo na pengine hata hatujui wao walipata faida yoyote hapo.
Ila Oleg nae miaka miwili mbele mbususu yake akaidirvoce tena aiseee
Umesoma yote lakini????Kitasa ndo basi tena?
Hv unafikiri jamii itakuchukuliaje ukiwa unagombana na kichaa, kichaa ni kumuepuka tu au ukiamua kukabiliana nae basi uchukue tahadhali.Mkuu!Ishu ya 85s huko,imekuwa wazi leo 2020.Ishu ya 2015s hivi,haiwezi kuwekwa wazi leo kwa kina.
SMO inaendelea huko Ukraine na ndani yake kunatuhuma juu ya U.S.A kuweka lebo za kikemikari huko.
Kupitia suala la Oleg,west ndiyo waliofurahia sana na kuepushwa na vita.Kwa nini furaha iwe kubwa kiasi hicho kama kweli hawakumuogopa USSR?.
Nikichojifunza ni kwamba ukiisaliti nchi yako kwa namna yoyote ,lazima utalipa high price even the blood price of your loved ones.
Oleg naweza kusema ni bahati ilikuwa upande wake ,kama ilivyo tu kwa ilivyokuwa kwa Kim Philby ambaye naye yupo huko Russia kwa Siri .
Yote Tisa KGb itabaki kuwa Moja ya taasisi nyeti ya kuigwa kama mfano kwa nchi nyingi duniani mpka sasa japokuwa Ili collapse mwaka 1991.
View attachment 2615422
Asante mkuu [emoji122] [emoji122]AFTERMATH.
Baada ya haya yote, kesi ya Oleg imebaki kuwa Case study kwa vyombo vya usalama vya nchi za magharibi Hadi Sasa. Kutokana na hadhi aliyopewa ,ameshasafiri nchi mbalimbali za dunia , ikiwemo New Zealand, South Africa, Australia, Canada, ufaransa, ujerumani, Israel, Saudi Arabia na nchi za Scandinavia Katika kutoa Somo kwa Mashirika ya kijasusi ya nchi hizo. Nchi nyingi duniani zililazimika kubadili muundo wa kiutendaji kwa taasisi za kijasusi za nchi hizo kutokana na hili swala la Oleg.
Maafisa mbalimbali wa M15 na M16 waliohusika na kesi hii ya Oleg wengine ni wastaafu ,na baadhi wametangulia mbele za haki na wengine bado kazini mpaka stori hii ilipowekwa kitabuni. Na wengi wa maafisa walibadilishwa vitengo waliohusika na Hili swala la Bwana Oleg Ili kuficha identity zao .
Na kwa upande wa bwana Aldrich Ames , madhara aliyoisababishia CIA ni kwamba ilipoteza majasusi wake wengi kwa Siri alizokuwa anatoa kwa nchi ya Russia. Na inakadiriwa Bwana Ames alipata kiasi Cha Dola milioni 4.6 kutokana na information alizokuwa anatoa kwa Urusi na wengi wa majasusi wa CIA waliokuwa Soviet walipotezwa mazima.
Yote kwa yote bwana Ames alikamatwa na maafisa wa FBI tarehe 21 Feb 1994 ,akiwa na mpenzi wake Rosario dupuy na kutiwa ndani.
Miezi miwili baadaye alikutwa na kesi ya kujibu kuhusiana na ujasusi na akafungwa kifungo Cha maisha jela . Mkewe Rosario dupuy alikutwa na hatia na kosa la ukwepaji Kodi na kosa la kutaka kufanya uhaini , na alipewa kifungo Cha miaka mitano baada ya plea bargaining. Kwa Sasa Ames ni mfungwa namba 40087-083 na anaitumikia adhabu yake kwenye geraza la federal correctional institution Terra Haute huko Indiana marekani.
Baadaye Ames alipohojiwa akiwa gerezani 1997 Alikiri na kusema aliwasaliti wengi kwa ajili ya pesa na akasema hakuwahi mjua Oleg na hakumsaliti.
Swala la nani aliyemchomesha Oleg mpaka Sasa limebakia kuwa kitendawili au fumbo la imani.
View attachment 2615407
Aldrich Ames akitiwa pingu na makachero wa FBI muda mfupi baada ya kukamatwa 1994. Hii ni baada ya kuvujisha Siri za CIA kwa KGB kwa zaidi ya miaka 10.
View attachment 2615409
Aldrich Ames na mkewe Rosario dupuy wakiwa kwenye arrest photography.muda mchache baada ya kukamatwa . Rosario aliachiliwa baada ya kukamilisha kifungo chake ,ila mumewe Aldrich still yupo jela.
Credit: ziende kwa
1.Ben MacIntyre@The spy and the Traitor.2018
2. Duka la vitabu la Elite Bookstore pale Shoppers Plaza Dodoma
3.wana jf wote na wale wote walionipa maua yangu[emoji39][emoji39][emoji39] Appreciation kwao for their encouragement.