AFTERMATH.
Baada ya haya yote, kesi ya Oleg imebaki kuwa Case study kwa vyombo vya usalama vya nchi za magharibi Hadi Sasa. Kutokana na hadhi aliyopewa ,ameshasafiri nchi mbalimbali za dunia , ikiwemo New Zealand, South Africa, Australia, Canada, ufaransa, ujerumani, Israel, Saudi Arabia na nchi za Scandinavia Katika kutoa Somo kwa Mashirika ya kijasusi ya nchi hizo. Nchi nyingi duniani zililazimika kubadili muundo wa kiutendaji kwa taasisi za kijasusi za nchi hizo kutokana na hili swala la Oleg.
Maafisa mbalimbali wa M15 na M16 waliohusika na kesi hii ya Oleg wengine ni wastaafu ,na baadhi wametangulia mbele za haki na wengine bado kazini mpaka stori hii ilipowekwa kitabuni. Na wengi wa maafisa walibadilishwa vitengo waliohusika na Hili swala la Bwana Oleg Ili kuficha identity zao .
Na kwa upande wa bwana Aldrich Ames , madhara aliyoisababishia CIA ni kwamba ilipoteza majasusi wake wengi kwa Siri alizokuwa anatoa kwa nchi ya Russia. Na inakadiriwa Bwana Ames alipata kiasi Cha Dola milioni 4.6 kutokana na information alizokuwa anatoa kwa Urusi na wengi wa majasusi wa CIA waliokuwa Soviet walipotezwa mazima.
Yote kwa yote bwana Ames alikamatwa na maafisa wa FBI tarehe 21 Feb 1994 ,akiwa na mpenzi wake Rosario dupuy na kutiwa ndani.
Miezi miwili baadaye alikutwa na kesi ya kujibu kuhusiana na ujasusi na akafungwa kifungo Cha maisha jela . Mkewe Rosario dupuy alikutwa na hatia na kosa la ukwepaji Kodi na kosa la kutaka kufanya uhaini , na alipewa kifungo Cha miaka mitano baada ya plea bargaining. Kwa Sasa Ames ni mfungwa namba 40087-083 na anaitumikia adhabu yake kwenye geraza la federal correctional institution Terra Haute huko Indiana marekani.
Baadaye Ames alipohojiwa akiwa gerezani 1997 Alikiri na kusema aliwasaliti wengi kwa ajili ya pesa na akasema hakuwahi mjua Oleg na hakumsaliti.
Swala la nani aliyemchomesha Oleg mpaka Sasa limebakia kuwa kitendawili au fumbo la imani.
View attachment 2615407
Aldrich Ames akitiwa pingu na makachero wa FBI muda mfupi baada ya kukamatwa 1994. Hii ni baada ya kuvujisha Siri za CIA kwa KGB kwa zaidi ya miaka 10.
View attachment 2615409
Aldrich Ames na mkewe Rosario dupuy wakiwa kwenye arrest photography.muda mchache baada ya kukamatwa . Rosario aliachiliwa baada ya kukamilisha kifungo chake ,ila mumewe Aldrich still yupo jela.
Credit: ziende kwa
1.Ben MacIntyre@The spy and the Traitor.2018
2. Duka la vitabu la Elite Bookstore pale Shoppers Plaza Dodoma
3.wana jf wote na wale wote walionipa maua yangu[emoji39][emoji39][emoji39] Appreciation kwao for their encouragement.