Tarehe 18 Mei 1985: Shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama Directorate K

Tarehe 18 Mei 1985: Shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama Directorate K

27



Maisha yaliendelea kama kawaida kwa bwana Oleg na maisha yake aliyoyachagua DOUBLE LIFE.
Maisha yake na mkewe Leila pamoja na watoto wao wawili waliishi kama kawaida wakawa obsessed na lifestyle ya uingereza . Wanao walipelekwa kwenye shule za uingereza .
Kipindi Oleg akiwa holiday huko Moscow , walikuwa na deep discussion na mkuu wa kitengo Cha FCD wakati huo bwana Nikolai gribin kuhusiana na na position mbalimbali za siasa za Russia na pia viongozi wa kisiasa waliokuwa na ushawishi wakati huo. Kipindi hicho kulikuwa na mwanasiasa aliyekuwa anachipukia na kuwa na ushawishi kwenye chama chake Cha komunist party aliyeitwa Mikhail Gorbachev.
Huyu bwana Gorbachev alitarajiwa angekuwa kiongozi wa Soviet kwa wakati huo. Kutokana na aina yake ya uongozi na pia misimamo Yake kuhusu siasa za kimataifa ,alimvutia Margaret thatcher na ilitarajiwa angefanya ziara ya kitaifa nchini uingereza. Na hatimaye 1984 Gorbachev alikubali mwaliko kutoka uingereza.
Hapa majasusi wa pande zote mbili M16 na KGB wakacheza karata zao kwenye ziara hii . KGB waliamua kumpangia Gorbachev nini aseme akikutana na Margaret na vilevile M16 wakampangia thatcher ninj cha kuongea mbele ya mgeni wake kwa msaada wa Oleg.
Hili swala Oleg Gordievsky lilimpa ushawishi sana na umaarufu ,kwa pande zote mbili kinzani sio ndani ya M16 Bali pia hata kwa KGB. Bwana Oleg alicheza kwenye nafasi yake kama mkuu wa kitengo Cha political intelligence ndani ya ubalozi wa Soviet hapo London. Kwa mfano Moscow walipanga topic za kuongelewa na Gorbachev kwenye ziara hiyo ,kama vile maswala ya kijeshi ,uchumi na teknolojia. Pia pamoja ya yote haya Urusi walidhani huenda tukio la kudukuliwa kwa kiongozi wao wa nchi kwenye nchi ya kigeni.
Kwa mfano ilisemekana Nikita Khrushchev alipofanya ziara ya kitaifa nchini uingereza mwaka 1956 sehemu aliyofikia ilidukuliwa kwa kupandikizwa vinasa sauti . Tukio hili Urusi walipojua lilizusha sana Mgogoro wa kidiplomasia baina ya nchi hizi mbili. Hivyo kwenye ziara hii walijipanga. Kukutana kwa viongozi Hawa wawili kwa wakati huo kulizusha mijadala mikali miongoni mwa wachambuzi wa siasa za kimataifa. Hii ilitokana na haiba ya viongozi Hawa na misimamo waliokuwa nayo. Gorbachev alikuwa ni breeding ya mfumo wa communism uliobeba mfumo mzima wa Soviet huku Margaret thatcher akiwa ni mpingaji wa mfumo huo kandamizi na wa kinyonyaji. Lakini ilikuja kuonekana Gorbachev alikuwa na itikadi za kiliberali kwa mbali. Na ndio iliamua ziara hii kufanyika kwa msaada wa majasusi wa pande zote mbili.
Hatimaye Mikhail na mkewe Raisa Gorbachev waliwasili London tarehe 15 Dec 1984 na ziara hii ilikuwa ya siku nane. Alitarajiwa pia kufanya shopping,na pia kutembelea British library ambapo bwana Karl Marx aliandika kitabu Cha das kapital na mambo mengine mengi.
Ziara hii ilienda vizuri kama ilivyotarajiwa .



**********@*******

Turudi Hadi kwa CIA huko Langley Virginia.[emoji116][emoji116]
Bwana Burton Gerber aliyekuwa ndiye alikuwa mkuu wa kitengo ndani ya CIA kilichokuwa kinashughulika na ujasusi ndani ya Soviet.
Alikuwa mtaalamu katika kitengo hicho. Ni kwamba huyu bwana alitamani sana kujua taarifa za kijasusi walizokuwa wanapata M16 kutoka kwenye chanzo Chao . Kutokana na bwana huyu kuwa expert katika kukusanya taarifa nyeti za kijasusi ndani ya Soviet ,hakuwa anapata taarifa fresh na za moto kama M16 walizokuwa wanapata kutoka kwa NOCTON a.k.a Oleg.
Kiufupi CIA walitamani kujua chanzo hiki ,lakini M16 kamwe hawakutaka kumu expose Oleg Kwa CIA . Kuna nukuu inasema " The psychological gratification of all intelligence work lies in knowing more than your adversaries,but also more than your allies...... In the all- embracing global view from Langley,the CIA had a right to know anything and everything it wanted to know".
Ni kwamba kupitia info alizokuwa anatoa Oleg Kwa M16 , CIA aliona atapoteza ushawishi duniani hususan kwenye swala la ujasusi .
Linapokuja swala ujasusi CIA alikuwa ana share taarifa na mashirika mengine kwa makubaliano maalumu hususan kama Lina maslahi kwa wote. Lakini kwenye swala la Oleg ,M16 hawakutaka kutoa identity ya NOCTON kwa namna yoyote ile.
Bill Casey mkurugenzi wa CIA wakati huo alitumia ushawishi aliokuwa nao kwa M16 lakini bado uingereza iliendelea kukaza.
Basi kutokana na uingereza kuendelea kukaza, ikatoka order from above ( huenda kwa Reagan au bill Casey),kwa Siri kwa ajili ya kumtambua huyu source aliyekuwa anawapa info M16. Hii ilikuwa ni mapema mwaka 1985. Na hili swala endapo uingereza wangegundua wanafanyiwa ujasusi ingekuwa ni kukiuka mutual agreements walizojiwekea baina ya mashirika haya mawili na ingezusha mtafaruku mkubwa .Huu mpango alipewa Gerber. Ofisi hii ya kitengo Cha ujasusi ndani ya Soviet ndipo idara ya counter-intelligence ilikuwepo na ndio idara ambayo Aldrich Ames aliisimamia...........[emoji3578][emoji3578][emoji3578][emoji1].
Huyu bwana Ames mbali na kuwa mkuu wa idara hii lakini maisha yake binafsi yalikuwa yanashida kidogo.
Huyu mwamba alikuwa ni mlevi kupindukia ukizingatia alikuwa na mke au mchepuko ambao ulikuwa unatumia pesa vibaya mno. Huyu bwana kutokana na maisha yake kuwa broke alijikuta na deni la $47000. Inasemekana wakati mmoja aliwaza kuvamia benki kutaka ku settle mambo . Hii ilitokana na matumizi makubwa aliyokuwa nayo mkewe Rosario dupuy. Hili swala lilimletea mgogoro yeye na wakuu wake wa kazi hapo kitengoni Langley . Mbali na tabia zake hizi wakuu wake wa kazi hawakumtilia maanani wala kumhisi vibaya bwana huyu.. ... What A fatal mistake

Tukiachana na personal life la bwana huyu, ni kwamba kutokana na position aliyokuwa nayo alikuwa na access ya taarifa za kijasusi zote kuhusiana na urusi wakati huo . Pia alikuwa anajua taarifa zote za majasusi waliopandikizwa ndani ya urusi wa KGB wanaotoa taarifa za kijasusi kwa Marekani. Kazi hii ya CIA kutaka kujua au kumjua jasusi anayeipa uingereza taarifa za kiintelijensia uingereza alikuwa nayo bwana huyu pamoja na Gerber. Wazungu waliwahi sema "EVERY SPY LEAVES CLUES". Wamarekani walianzia kwenye msemo huu kutaka kusolve hili fumbo la huyu SOURCE ni nani??
Kitengo hichi alichokuwepo bwana Ames wakaanza taratibu kupitia taarifa zote za kijasusi walizokuwa wanazipata kwa M16 ambazo NOCTON au Oleg alizokuwa anawapa.
Kwa mfano kuhusiana taarifa za operation ya kijasusi ya Russia iliyokuwa inafanywa ya Kutaka kufahamu viashiria vya kutokea kwa vita ya nyuklia ,ilianza kutoa clue kwamba huenda huyu source atakuwa ni afisa wa KGB ,na huenda ana cheo kikubwa kiasi kwenye shirika Hilo kuweza kupata taarifa hizi[emoji848].
Wakaanza kupata clue nyingine ,kwamba huenda huyu SOURCE atakuwa na uwezekano wa kukutana na M16 mara kwa mara. Na wakaweza kung'amua kwamba huyu source huenda yupo nje Russia na possiblity ya source huyu kuwa ndani ya uingereza ilikuwa ni mkubwa . Vilevile CIA wakaendelea kupata clues zaidi ,kwamba kwa taarifa walizokuwa wanapata M16 kutoka kwa SOURCE zilikuwa zinatoa infos chache kuhusiana na maswala ya kijeshi au kiteknolojia lakini zilikuwa zipo based kwenye maswala ya politics kwa kiasi kikubwa. Na kwa vile CIA walikuwa wanajua organizational structure ya shirika la KGB , waliamini huyu source atakuwa anafanya kazi kwenye idara FCD (first chief directorate) kitengo kidogo Cha political intelligence.[emoji3578][emoji3578][emoji28].
CIA wakaendelea kufanya enquiries za kutosha kuhusiana na SOURCE . CIA wakajiuliza swali lingine muhimu . Ni lini nchi ya Soviet ilianza kupoteza majasusi au mapandikizi wake waliokuwa nchi za magharibi ? Na kweli wakaanza ku connect dot. Baadhi ya watu kadhaa hususan majasusi walishtukiwa wakihusishwa kufanya kazi na Russia, Arne treholt, na haavik wa Norway na vilevile berlig wa sweeden , na la Zaidi ni huyu bettaney au Koba aliyekamatwa nchini uingereza kwa tuhuma za kijasusi. Marekani wakapata clues kwamba huenda huyu SOURCE ndio aliyewachomesha .
Marekani wakaendelea kupata clues zaidi wakiamini kutokana na hao majasusi waliotuhumiwa na kukamatwa kwenye nchi za Norway, Sweden na uingereza , huenda huyu SOURCE alishawahi fanya kazi kwenye nchi mojawapo ya Scandinavia. Pia CIA wakaanza kuunganisha dot Zaidi kufukuzwa kwa balozi wa Russia nchini uingereza Bwana Arkadi guk baada ya kugundulika au kutuhumiwa alikuwa anafanya ujasusi ndani ya nchi hiyo.
Baada ya CIA kufanya enquiries hizi zote pamoja na kuchora pattern zote na kuunganisha matukio , zilimwangukia bwana OLEG GORDIEVSKY .[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38].
Wanasema kwamba kuhusiana na hili nanukuu" The Brits thought they knew something the Americans didn't know they knew.... But now the CIA knew something that M16 did not know they knew" . Hii ilikuwa ni gemu katika ulimwengu wa kijasusi.Ni kama unamwinda mtu ambaye naye anakuwinda ila hujui kama anakuwinda .

Kutokana na CIA majibu kuhusiana na mwamba NOCTON a.k.a Oleg au source. wao Walimpa jina la uficho au codename TICKLE.............

.........
[emoji23][emoji23][emoji23]nmependa sana akili kubwa ya CIA kweli kazi ya Intelijensia inahitaji watu wenye akili kung'amua mambo.
 
Hata kama wewe ni kipenyo Hakuna kitu kilichoniingia hapo na wala hujanishwawishi kuondoka nilipoegemea kile nilichokiingiza kutokana na kile alichokifanya Oleg. Labda tu unatania,kwa hapa tulipofikia kama nchi,kuanzia huko juu wanachokifanya, Kama hivyo kila repot ya CAG watu kwenye nafasi zao wanajipakulia tu asali kwa kipimo chao. Ufisadi kila kona. Huku chini mimi ni nani ikitokea nafasi kama ya Oleg nisichukue mpunga?.
At your own risk! Adhabu ya usaliti kwa Taifa bora uhujumu uchumi.
 
Na ukiweza kutoroka unakuwa ni mtu wa kujificha tu.
Labda utoroke Nchi yaani Tena ukimbilie Huko marekani vijijini kule mashambani kabisa au Huko visiwa vya Papua new guinea ukaishi Huko , unless wakijua upo karibu halafu ukute ishu yako ni nzito lazima utumiwe hit squad wakuondoe
 
[emoji2][emoji2]huyu buyobe Hana haya Wala aibu ni mkavu kweli kweli Bora basi aseme ameitoa JF hasemi hafu huko twirani watu hawajamshtukia tu hata story NZuri ya yoga, umughaka kaiba, jamani huyu mwanaume mwizi kwerikweri in jiwes voice
Kama anaweza kuiba stori ya Umughaka basi kachoka
 
Back
Top Bottom