Tarehe 18 Mei 1985: Shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama Directorate K

Tarehe 18 Mei 1985: Shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama Directorate K

Huwa najiuliza hizi signal wanazopeana za kuacha kitu sehem then mwengine anachukua na kuacha signal kuwa amepokea mzigo.. Hizo signals wanakuwa wamepewa kwenye training zao huko ujasusini collages au wanajiongeza tu juu kwa juu!?
Nahisi kuna maelekezo yanatangulia namna watakavyopeana signal
 
 
22


Mwezi mei mwaka 1981 , mwenyekiti wa KGB wakati huo bwana Yuri Andropov,aliwakusanya maafisa wenzake wakuu wa vitengo mbalimbali huko Moscow wa shirika Hilo kuzungumzia swala la tishio la marekani kutumia silaha za nyuklia dhidi ya umoja wa kisoviet. Kwa miaka zaidi ya ishirini kulikuwa na matishiano kati ya nchi za magharibi na nchi za mashariki /Soviet katika maswala ya kutumia silaha za nyuklia za mass destruction. Kwa mfano ilisemwa kwamba Soviet ilianza kufanya geopolitical survey kwa kutumia programu maalumu za kompyuta. Matokeo yalionyesha kwamba nchi nyingi sana duniani zilikuwa Zina wa wafavour West kijeshi . Hii ni kwa maana kwamba nchi nyingi zilikuwa upande wa NATO endapo kungetokea vita vya nyuklia kwa wakati huo . Pia matokeo ya utafiti huu yalionyesha kwamba Soviet iliingia gharama kubwa kwa kitendo chake Cha kuivamia Afghanistan, vilevile kuwekwa kwa makombora huko kyuba wakati wa Fidel Castro,kuliingiza USSR kwenye matumizi makubwa ya fedha yasiyokuwa ya lazima . Survey iliendelea kuonyesha matokeo yake kwamba marekani kipindi hicho ilikuwa ikifanya military build-up kwa Kasi sana. Hii iliwapa umoja wa Soviet kiwewe na hofu kuu.
Hivyo bwana Andropov kupitia survey hii aliona Kuna uwezekano wa Soviet kufeli kwenye hii battle iliyokuwa inaendelea ya vita baridi. Hii ni kutokana na personal experience aliyokuwa nayo kipindi akiwa balozi wa Soviet nchini Hungary kwamba hata taifa Liwe na nguvu kiasi gani linaweza kuanguka kwa namna yoyote na muda wowote . Hii aliliona kipindi akiwa huko Hungary kama balozi pale raia walipoinuka kupinga utawala wa kikomunisti nchini mwao. Hivyo bwana Andropov akapendekeza ianzishwe operation maalumu ya ku deals na vitisho alivyoamini yeye dhidi ya muungano wa Soviet.
Aliamini kwamba west walikuwa na mpango wa kuilipua Soviet muda wowote ule.[emoji38][emoji38]
Hivyo Andropov pamoja na KGB wakaanzisha operation kubwa ya kijasusi iliyopata baraka zote pia kutoka kwa Leonid Brezhnev . Kupitia operation hii kazi kubwa kwa KGB ni kutafuta viashiria vyote vilivyokuwepo vitavyoonyesha na ku confirm kwamba ni kweli marekani na washirika wake wa NATO kama uingereza walikuwa na mpango wa kuipiga Soviet , hivyo wao wangepata sababu za kujilinda kwa namna yoyote ile[emoji3578][emoji3578]. Hii operation ilijulikana kwa jina la operation RYAN. ( Raketno-Yadernoye Napadeniye) ikiwa na maana ya nuclear missile attack kwa kirusi. Hii kamati iliwahusisha pia GRU au shirika la kijasusi ndani ya jeshi la Russia. Hivyo mwezi November 1981 viongozi kadhaa waliosuka hii operation walitumwa kwenye nchi kama marekani ,ulaya magharibi, Japan na pia kwenye nchi kadhaa ikiwemo afrika katika kuhimiza hii operation ifanyike kwenye balozi hizo na kuifanya kuwa top priority. Kwa hiyo mpaka ilipofika 1982 kipindi Oleg anawasili huko uingereza ilikuwa imeshashika Kasi .
Lakini bwana Andropov katika kuanzisha operesheni hii alivunja kanuni Moja ya kijasusi
"Never ask for confirmation of something you already believe". Bwana Andropov aliamini kwamba west wanataka kuivamia Soviet ,yeye katika kutaka kudhibitisha anachokiamini akaanzisha operation hii ya kutafuta viashiria vya uwezekano wa kuwepo vita vya nyuklia.


Mwezi November 1982 huyu Andropov alichaguliwa kuongoza Soviet akimfuatia Leonid Brezhnev. Kuchaguliwa kwa Andropov kama rais kuliifanya operesheni hii iwe top priority kwa balozi zote za urusi duniani kote.
Hapo ubalozi wa London pia ilikuja telegram yenye ujumbe Yermakov. ikiwa imeandikwa juu "top secret" . Haya yalikuwa ni maelekezo maalumu kuhusiana na operation hiyo ya Ryan kwa mabalozi wote. Oleg alipopata blueprint ya hii taarifa nyeti ya Siri ya RYAN alimkabidhi kachero wa M16 na ikatua mikononi mwa wakubwa wa kitengo. Kwa mfano kwa mujibu wa maelezo ya taarifa hiyo kuhusiana na hii operation ,iliwaagiza maafisa wote wa KGB ndani ya nchi za west ikiwemo uingereza kufanya surveillance kwa so called "key nuclear decision makers" . Hii ilikuwa Ina maana kwamba majasusi walipaswa kuangalia movement za viongozi ikiwemo sehemu familia zao zinapoishi , vilevile kuangalia uwezekano wa kuwepo kwa vituo vya kukusanya watu endapo kutatokea vita,uwepo wa mahandaki n.k . Kwa kifupi majasusi walipewa jukumu la kuangalia kama haya yote yanafanyika kwenye hizo nchi basi watafanya hitimisho ni kweli Kuna vita vinakuja. Kwa Sababu Urusi iliamini endapo west watakuwa wanajitayarisha kwa vita vya nyuklia basi lazima waanze maandalizi ya kuwalinda Raia wao kwanza kwa kuwajengea mahandaki ,na kuhamisha familia zao sehemu salama.na vilevile vifaa vya kijeshi vingekuwa vimewekwa tayari kwenye kambi mbalimbali. Haya majukumu yalipaswa kufanywa na maagent wa KGB. Na la ajabu zaidi ni ku monitor hospitali mbalimbali. Maelekezo yalisema pia majasusi wawe macho kwenye hospital kama wakiona Kuna makusanyo makubwa ya damu basi wataamini moja kwa Moja damu zinakusanywa kwa ajili ya majeruhi wa wakati wa vita. [emoji38]. kiukweli Oleg na pia M16 waliona hizi taarifa kama kituko Cha mwaka na ni kama ndoto ya usiku iliyoandikwa kwenye karatasi. Hii operation ilionyesha ni kama kuku wa broiler aliyelishwa vyakula vya kiwandani na nyama yake Haina ladha yoyote. Kwa kifupi ni kwamba maelekezo haya yalikuwa ni kama utopian society.NCHI YA KUSADIKIKA
Kutokana na utawala wa Reagan ,hii operation ilizidi kupamba moto. Kwa mfano Reagan mwaka 1983 aliuita muungano wa Soviet kama "evil empire". Hii ni baada ya NATO ku test kombora la masafa mafupi aina ya Pershing II intermediate-range ballistic missiles huko west Germany kama majibu kwa Warsaw pact ambao nao walikuwa Wana test makombora Yao .hii iliongeza uoga kwa Soviet. Soviet waliamini makombora hayo yangeweza kuipiga Moscow na targets zingine muhimu ndani ya dakika sita kama maghala ya kijeshi . hivyo wa rusi wakaona option ni kuanza kujihami mapema
Kwa mfano mwezi march mwaka huo 1983 Ronald Reagan alitangazia umma Nia yake ya kutumia mfumo wa satellites na silaha za kisasa za anga za juu zenye uwezo wa kutengeneza shield angani na kutungua kombora lolote la urusi. Huu mpango wa Reagan ulijulikana Kama America's strategic Defense initiative. au " star wars". Na hiki kipindi ndipo ilipotengenezwa filamu za star wars kama propaganda ya mpango huo wa Reagan na Hollywood kuitisha urusi . Hii ilimkasirisha Andropov waziwazi ila kiuhalisia ilimtia uoga sana. Na hii ikazidi kupandisha homa ya vita vya nyuklia baina ya west na East.hii ilitokana na msemo kuwa, nchi iliyokuwa inaogopa uwezekano wa kutokea vita , ndio wa kwanza kuanzisha vita. Hili lilidhihirika waziwazi kwamba huenda Soviet ingeweza ku strike first kutokana na uoga na kupanick kwa wakati huo. Lakini haya yakiendelea uingereza na M16 walikwisha jua kelele zote za Russia kuhusiana na vita vya nyuklia zilikuwa ni FANTASY na ndoto kwa upande wa Soviet .. ni sawasawa kuota unakimbizwa na mbwa halafu ushtuke usingizini unapiga kelele ukisema mbwa mbwa ananifukuza walioko macho watakushangaa na kukuona tayari nati zimeanza kulegea za kichwani.
Tuachane na hili..........


Lakini wanasema ushirikiano kati ya CIA na M16 haukuwa mkubwa sana kivile hususan katika maswala ya kiintelijensia. Zilikuwa ni taasisi zilizokuwa karibu lakini zinaoneana wivu. Hii ni kutokana na kutafuta ushawishi duniani kwamba nani ni Bora kuliko mwingine. Hizi taasisi zilikuwa na matatizo yanayofanana kihistoria ,nayo ni kuwepo kwa MAPANDIKIZI ya kikomunisti ndani yake. Hivyo kutokana na mutual agreements walizojiwekea baina yao ilikuwa ni lazima ku share baadhi ya taarifa zitakazokusanywa endapo Zina maslahi kwa kila upande .
Kwa mfano kuwepo kwa hii operation ya kijasusi ya Urusi ya RYAN ,M16 walipaswa kuwamegea CIA nao. Swala na kipengele kikaja CIA wangezipokea hizo info lakini wangetaka kujua chanzo ,the source . Hili M16 hawakutaka mtu wao yaani NOCTON ajulikane zaidi ya maafisa kadhaa ndani ya M16 , M15 na pia kwa PET. Kuwashirikisha CIA kuhusu NOCTON kungeleta mtafaruku na pia uwezekano wa Oleg kugundulika ungekuwa mkubwa sana.
Nitarudi....
 
Back
Top Bottom