Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 1,679
- 2,123
Kuna watu wanajiuliza kwanini Wakristo wanasherehekea Christmas tarehe 25 Desemba? Imeandikwa wapi? Na wengine wanaenda mbali kwa kusema kusherehekea Christmas tarehe 25 Desemba ni ibada ya upagani. Naomba nitoe majibu ya maswali hayo kwa ufupi: Tarehe 25 December ilichaguliwa na Wakristo wa mwanzo iwe siku rasmi ya kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu, kwa sababu hizi mbili kuu:
1. Iwe kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo, ambaye aliletwa kuwa Mwokozi wa wanadamu (Isaya 9:6; Mathayo 1:21). Ingawa tarehe halisi ya kuzaliwa kwa Yesu haijatajwa katika Biblia, Wakristo waliichagua tarehe hii ili kuheshimu tukio hilo la kipekee la kuja kwa Mwokozi wa ulimwengu.
2. Nyakati za mwanzo kulikuwa na sherehe za kipagani kama Saturnalia (ya Warumi) na Sol Invictus (Kuzaliwa kwa Jua). Sherehe hizi zilifanyika mwishoni mwa Desemba, zikihusisha nuru ya jua na mzunguko wa maisha. Kanisa likaona vema kuleta mtazamo mpya wa Kikristo unaomheshimu Yesu kuwa ndiye "Nuru ya Ulimwengu" (Yohana 8:12). Hivyo likateua tarehe 25 Desemba kuwa siku rasmi ya kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu(Krismasi). Hiyo ilikuwa mnamo mwaka 336 BK chini ya utawala wa Mfalme Konstantino, Kaisari wa kwanza wa Kikristo.
Kuchaguliwa kwa tarehe hiyo kulihamasisha ukristo miongoni mwa Warumi waliokuwa wakiadhimisha Saturnalia.
Kuchaguliwa kwa tarehe hiyo kuliunganisha jamii ya waumini wote duniani chini ya tarehe moja ya kusherehekea nuru mpya ya Yesu Kristo.
Ni kweli haijaandikwa tusherehekee Krismas tarehe 25 Desemba. Lakini je, kila tunachokifanya duniani kimeandikwa au kimeagizwa katika Biblia? Imeandikwa wapi mtu akitaka kupika chakula atumie jiko la gesi? Imeandikwa wapi tukitaka kusafisha meno tutumie Colgate? Mtu kama haoni sababu ya kusherehekea Christmas tusimhukumu. Na yeye pia asiwahukumu wanaoona vema kusherehekea Christmas tarehe 25 Desemba.
Umuhimu wa kusherehekea Christmas umeelezwa kwa kina katika uzi huu:
www.jamiiforums.com

Kwanini tunasherehekea Christmas? Sababu 10 za kiroho na kiafya
1. Kuzaliwa kwa Yesu ni habari njema ya furaha kuu(Luka 2:10-11). Malaika walipoleta habari ya kuzaliwa kwa Yesu walisema hiyo ni habari ya FURAHA KUU. Na kwamba furaha hii kuu itakuwa kwa watu wote. Kusherehekea Christmas ni udhihirisho kuwa tumeipata furaha kuu katika mioyo yetu. 2. Kutimizwa...