Tarehe/siku nzuri kwa mimba kuweza kutungwa

Wana jf wenzangu naomba mnifahamishe ni siku gani mwanamke anaweza kupata mimba,siku ya ngapi baada ya kutoka kwenye period?

Wanawake wengi wana mzunguko wa mwezi wa siku 28, japo kuna wengine wachache wana mzunguko mrefu wa siku 30 na wengine mzunguko mfupi wa siku 25 au 26. Katika mizunguko yote hiyo, yai huolewa (ovulation) siku ya kati ya mzunguko ina maana siku ya 14 kwa mzunguko wa siku 28, siku ya 15 kwa mzunguko mrefu na siku ya 13 kwa mzunguko mfupi. Manii za mwanaume zinaweza kuishi mpaka siku tatu, kwa hiyo iku za hatari kwa mwanamke kupata mimba kwa mizunguko yote mitatu ni kuanzia siku ya 11 tangu AANZE kupata hedhi, mpaka siku ya 18.
 
Jeee ni siku ngapi baada ya mwanamke kumaliza siku zake za hedhi anaweza kupata mimba?
 
Unataka kuchanishwa nyavu? Kama ndo hivyo fanya kila siku au ruka siku moja moja, kwa mfano, unafanya j'tatu, j'nne unaskip, J'tano unafanya na kuendelea
 
Unataka kuchanishwa nyavu? Kama ndo hivyo fanya kila siku au ruka siku moja moja, kwa mfano, unafanya j'tatu, j'nne unaskip, j'tano unafanya na kuendelea

ha hahahaaaaaa uwiiiiiiiiii ww acha kumpotosha mwenzio!! mh best unaumri gani ss hujui tar za kushika mimba? inaelekea husomi thread humu nafikiri niliona kwenye JF Dr. na hii thread yako kule ndio ingekuwa vizuri sana, nafikiri majibu ya hapa ndio kama unavyoyaona!!!
Nitarudi badae!!!
 
Uliza gynacologist itasaidia wewe. Bado kujua saa ipi manamke inapata mimba? Iko na miaka ngapi wewe?
 

Wala hakuna upotoshaji hapo. Kama shabaha yake ni kushika mimba hiyo fomyula niliyompa inafanya kazi ili mradi kusiwe na matatizo mengine.

Ila kama hataki kushika mimba hakuna cha safe days wala nini. Cha muhimu ni kutumia birth control iliyo reliable na abstinence ndio ya uhakika kwa asilimia 99.9.....
 

No comments!!!
 
Unataka kuchanishwa nyavu? Kama ndo hivyo fanya kila siku au ruka siku moja moja, kwa mfano, unafanya j'tatu, j'nne unaskip, j'tano unafanya na kuendelea

Utamchosha mwenzio bure. Ziko siku za kupata mimba, na anatakiwa akae siku kadhaa kama 3 hivi kusudi mbegu zikomae ndio ampande Mkewe. Usiseme hivyo, Jaribu kuwa mkweli zaidi.

Ni kweli atapata mimba ila, this is not TECHNICAL zaidi.
 

Suppose wanafanya tendo la ndoa siku moja au mbili hivi kabla ya hedhi kuanza, ambapo uterus tayari iko 'physiologically committed' to shed the endometrial layer...how is pregnancy possible there?
 
Utamchosha mwenzio bure.... Ziko siku za kupata mimba, na anatakiwa akae siku kadhaa kama 3 hivi kusudi mbegu zikomae ndio ampande Mkewe.. Usiseme hivyo, Jaribu kuwa mkweli zaidi...

Ni kweli atapata mimba ila, this is not TECHNICAL zaidi.

Hakuna kuchoka mtu unapo do every other day. Na kama mwanamme ni rijali mwenye mbegu zenye afya ya kurutubisha yai la mwanamke basi nyavu lazima ichanike.

Lakini kama wote mna matatizo, wewe una low sperm count kwa mfano, na yeye labda ana matatizo ya ovulation, hapo ndo mnaweza kuchoka.

Lakini every other day is a safe bet to get knocked up...trust me you!!!!
 
Nyavu lazima ichanikeeeee!!! jamani hembu hapa nieleweshe kidogo Mobile!!
 
Suppose wanafanya tendo la ndoa siku moja au mbili hivi kabla ya hedhi kuanza, ambapo uterus tayari iko 'physiologically committed' to shed the endometrial layer...how is pregnancy possible there?

Kuna mambo ambayo yako 'unexplainable' na ikija kwenye miili ya binadamu mambo ya exact science huwa haya apply kwa sana.

Wewe hujawahi kusikia mwanamke aliyekuwa anatumia birth control pills kupata mimba wakati hata hajaacha kumeza hivyo vidonge? Hujawahi kusikia wanawake wakipatwa na hedhi ingali ni wajawazito? Hujawahi kusikia wanawake waliokuwa na mimba bila hata ya kujua wana mimba? Hujawahi kusikia wanawake wanaopata hedhi mara mbili kwa mwezi?
 
Jeee ni siku ngapi baada ya mwanamke kumaliza siku zake za hedhi anaweza kupata mimba?

Kama alivyosema Susy, tulishajadili hili kule JF Doctor...lakini kwa msaada tu ni kuwa:

- Inategemea na mzunguko wako, wanawake wengi wana mzunguko wa siku 28, lakini wachache wana mzunguko mfupi wa siku 25 au 26, na wengine mzunguko mrefu wa siku 30.
- Yai la kike hutolewa katikati ya mzunguko (ovulation), ina maana kwa wanawake wenye mzunguko wa kawaida ni siku ya 14, mzunguko mfupi ni siku ya 13 na mzunguko mrefu siku ya 15.
- Yai likitolewa huwa lina siku 3 hadi 4 kurutubishwa ili litunge mimba. Lakini pia, mbegu za mwanaume zinaweza kuwa hai kwa siku 3.
- Kwa hiyo ukifanya tendo la ndoa ndani ya siku 3 kabla ya ovulation, na ndani ya siku 4 baada ya ovulation utapata mimba.

Kwa hiyo, siku nzuri za kupata mimba kuanzia siku ya 11 tangu UANZE hedhi, mpaka siku ya 18.
 
Sa Carina we hujui siku za mwanamke kupata mimba.

Mara nyingi siku ya kumi na nne kuanzia ile siku ya kwanza aliopata hedhi.
Wanasema akikutana na Mbegu siku ya kumi na tatu kuna uwezekano wa kupatikana mtoto wa like.
Na akikutana na Mbegu siku ya kumi na nne, kuna uwezekano wa kupatikana mtoto wa kiume.

Hebu ngoja tuone wataalamu zaidi huku wanasema je!!!!!
 
Jaribu kudu siku ya 13,14,15 na 16 toka ulipoanza MP, yaani kama umenza MP tarehe 14 March basi du kuanzia 26,27,28 na 29, ingawa huwa ni siku ya 14 but kutokana na mabadiliko mabadiliko just try hapo natumaini utapata matokeo
 

Unaweza kuwa unafahamu unachoongelea ama haufahamu but that does not matter. Naamini mbegu (sperms) ni tofauti na shahawa (semen) in that sperm huwa ndani ya shahawa. Isije ukadhani kuwa kama unapiga round kibao unamwaga tu utakuwa unamwaga sperms tu pale, unaweza kujikuta unamwaga maji tu yanayotengenezwa ktk seminal vesicles na prostate glands or even cowper's gland. Lazima ujua kama unafanya tendo hilo mara kwa mara epididymal reserve inakuwa depleted and you will need time to replenish it. Tell me, do you have an idea how long does the spermatogenesis cycle take?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…